Kidebe cha Dogo Janja

Hii inanikumbusha msiba wa Amina Chifupa nilikuwa nje sasa kurejea nimekaa napitia magazeti ya kitambo kwa sister nakuta Amina kaaga dunia nilishtuka kwa sauti haaa! Amina kafariki kila aliyekuwa jirani alinishangaa coz walikuwa hawajui kama sikuwepo na sikutaka kufafanua kwa nini sikujua
Hiyo kidebe ya mda kidogo mkuu sema ni wimbo mzuri sana audio na video zote dogo kajitahidi sana.
 
Huwa inatokea. Mi nilipatwa kama wewe, nilisafiri kidogo, huku nyuma Temba ft Dully nampenda yeye ikatoka, sina hili wala lile, nimerudi, nimeenda kusalimia jamaa, tupo sebureni, mara eatv wanaipiga, bila kujijua nikaropokwa: DAAH, TEMBA KATOA BONGE LA NGOMA! Kumbe ngoma ina miezi kama mi5!
 
Dah, wee jamaa wa zamani kishenzi,
mi enzi hizo ndo kwaanza kinda
 
Duh kweli laiti tungekuwa tunaonana kumbe watu tunabishana tuna gombana na wadogo zetu humu.
Ndio maana watu wenye umri mkubwa humu tunatakiwa tuongeze kuwa wastahmilivu kwa threads zinazoletwa na comments pia inafika mahala unajiuliza huyu mtu alieandika hapa yukoje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…