Kidogo chochote unachopata, kitunze tafadhali

Kidogo chochote unachopata, kitunze tafadhali

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,587
Maisha yetu (watu wa level ya chini) yamekuwa hayatabiriki kabisa, hatuijui kesho yetu. Hata kula ni ya changamoto sana.

RAI YANGU:
Kidogo unachopata, hata kama ni kidogo, tumia kiasi then kitunze, kirundikane na vyenzie ili viisaidie kesho yako.

Kuna wakati mwanaume mzima unaamka huna hata 1,000 ya kupandia bajaji uingie maeneo ya mjini. Ni hatari sana kwa ustawi wa jamii.
 
Mungu ni mwenye kurehumu sana... kila anayeteseka kifedha kwa mfano, Mungu ana sababu zake kukubali apitie magumu hayo... kwani ni kuamua tu na inakuwa kwa muumba wetu... kuna matendo yetu (sio lazima madhambi), kuna mazingira, kuna binadamu mwingine ana sababisha (mmoja kwa mmoja au la), n.k

Kwa ujumla, tusipoteze imani kwa alietuleta duniani kwa malengo maalum. Katika kuifikia hili lengo maalum (kila binadamu na uelewa wake) ni muhimu kukumbushana kwamba Mungu hamtupi hata kwa sekunde kila alichoumba.

yote ni mitihani, anayepata kidogo na anayepata nyingi pia.. kwani anayepata nyingi pia anawajibika... na ambao tunaamini kwamba anayepata anawajibika kikweli kweli, sio mchezo, tunapata faraja kwamba Mungu hakosei.

Tuombeane sote!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante mkuu. Na umenikumbusha kabla ata mshahara haujatoka. Asante.
 
Mungu hausiki hata kidogo... Amini amini nakwambia.
 
Tumia muda kwa kupambana sana na usiwe mtu wa kulalamika sana.

Ni ku hustle tu.

Usipoteze mda wako mwingi kwa kukaa na washkaji bila faida.

Lazima utafute kwa nguvu zote ila upate hizo za kuficha pembeni
 
Back
Top Bottom