SoC02 Kidonda kilichopata mkunaji

SoC02 Kidonda kilichopata mkunaji

Stories of Change - 2022 Competition

Pink L

New Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
2
Reaction score
1
Mfumo wa elimu katika nchi yetu umekuwa ni changamoto kubwa sana. Namna unavyoendeshwa unakuwa ni tatizo kwa wanafunzi wengi kuweza kufikia malengo yao. Wanafunzi wengi wamejikuta wakisomea fani ambazo si chaguo lao na inawalazimu kufanya hivyo ili tu kwendana na upepo wa Ajira. Vipaji vingi vinakufa kabla hata havijaanza hata kitambaa. Ni jukumu la serikali na wadao wote wa elimu kupitia upya mfumo na mitaala kwa ujumla ili kuweza kuzalisha mazao yaliyo bora. Lakini pia, wazazi au walezi wanatakiwa kupewa elimu ili wasiwe mstari wa mbele kuwapeleka watoto njia wanazoona zina manufaa kwao na si kwa watoto.

---
Wanakijiji wa kijiji cha Inyika walitahamaki baada ya kusikia taarifa mpya masikioni mwao kutoka kwa waziri wao mteule, wengi wao hawakuelewa kilichomaanishwa na wengine walipatwa na butwaa wakijua hatima ya elimu ya watoto wao ilifika kikomo. Walisemezana kwa makundi ili kueleweshana. Wengine walioona kama maneno ya wenzao yalikingana waliamua kumfuata diwani wa kata ili aweze kuwaelewesha maana waliamini kuwa yeye alikuwa majibu ya uhakika tofauti nay ale waliyoambiana wao kwa wao. Diwani aliwaeleza kile alichokisema waziri wa elimu kuwa, mtaala wa elimu ulikuwa umebadilika. Wanafunzi walitakiwa kusoma kwa vitendo zaidi kuliko nadharia, wanafunzi walitakiwa wasome kulingana na vipawa vyao, endapo kama mwanafunzi alikuwa na kipawa cha kuimba, kucheza ngoma na kutunga hadithi pamoja na kuigiza basi walitakiwa waende shule ambayo ilitengwa maalumu kwa ajili ya vipawa vya sanaa. Wale waliobobea katika michezo kama vile: mpra wa miguu, mpira wa pete, mpira wa kikapu na mingine walitakiwa waende kwenye shule ambazo zilitakiwa zitoe mafunzo hayo tuu. Halikadhalika wale ambao walipendelea kujihusisha na kilimo kwa ujumla walitakiwa waende katika shule zilizotoa mafunzo hayo bila kuhusisha mafunzo mengine yoyote yale. Na wale waliopenda fani za uuguzi, ukandarasi, sheria na kadharika walitakiwa kwenda kulingana na fani zao. Lengo kuu lilikuwa ni kuwaandaa watoto na kuwajengea misingi toka chini ili kuwajengea uwezo wasije kupata shida hata pale ambapo watakuwa katika ajira.

Na mtaala huo uliwahusu wale ambao walikuwa walienda kuanza ngazi ya sekondari lakini, ngazi ya msingi iliwajumuisha wote huku walimu wao wakiwa na kazi ya kuwaainisha kila mwanafunzi na kipawa chake ili kurahisisha kazi. Wanafunzi walitakiwa kuchagua shule kulingana na vipawa vyao, halikadhalika waalimu walitakiwa kupewa mafunzo kwa kuendana na mtaala mpya kwani enzi wao wanasoma haukuwepo. Diwani alimalizia kwa kuwaelezea kuwa mtaala huo hautawaathiri wale ambao walikuwa wamekwisha anza masomo yao ya sekondari. “ahaaaa kumbe!” Wanainchi waliitikia kwa vichwa vyao kuashiria kuwa walielewa walichoambiwa.

“mwenzio hata sijaelewa hata kimoja kwa hiyo mwanangu akimaliza anatakiwa akalime maana sisi wazazi wake ni wakulima au alimaanisha nini” mama semeni alimuuliza mama ashura “shoga yangu nawe una kichwa kama cha panzi, kichwa kikubwa ila huelewi, amesema hivi, waziri wetu amesema matala yamebadilika sasa hivi watoto wetu hawaendi tena shule na madaftari ila wanaenda kusomea usanii kuwa kama kina mpoto heheee na hivi mwanangu anajua kuimba yaani baada ya mwaka tuu utaniona naendesha gari yangu na unaanza kutuona kwenye tv, hehehe haloo! Ngoja nikamwambie mwanangu ajaze kabla nafasi hazijaja. Nyie mtaishia kulima tuu hukuhuku si mlikuwa mnanicheka eti mwanangu atakuwa muhuni kiko wapi sasa eeh?!” Mama ashura alitokwa na maneno kama filimbi ya mwizi na kumwacha mama semeni akimshangaa.

Semeni akiwa na kaka yake kisimani wakichota maji alimuuliza “hivi kaka unahisi huu mtaala utatusaidia au utatugawa kimatabaka na vipi wazazi ambao hawatakuwa na uwezo wa kuwalipia watoto wao katika shule ambazo watoto wao watatakiwa kwenda si watakuwa wamepotezewa muda wakati wangesoma masomo yote huko mbele wangekuja kuchagua kwenye unafuu” kijigo kaka wa semeni alimwangalia mdogo wake kasha akatabasamu akamtikisa kichwa akamwambia “mdogo wangu una akili sana, ila tu napenda utambue kuwa, serikali mpaka kufikia hatua hiyo ishaona hayo yote na nahisi imefanya hivyo ili kuwajengea uwezo wa kujiajiri nyie wenyewe pindi mmalizapo ili msingoje ajira kama sisi tuna mwaka wa nne nyumbani kila tunachoshika hakifanikiwi kwa kuwa hatuna msingi mzuri, hivyo hutakiwi kusita kwenda kusomea kitu unachokipenda kwa kuhofia kiasi. Kwani wee ulitaka usomee nini mdogo wangu?” Semeni alichukua kata na kunywa maji kidogo kasha akamwambia kijigo “mi nataka nikasomee sheria ingawa mama anataka eti niende kwenye sanaa na baba naye anataka niende udaktari” semeni aliongea kwa masikitiko. Kijigo alimuahidi kuwashawishi wazazi wao ili akasomee kile anachotaka.

Maneno ya mama semeni yalimkosesha raha mama ashura kwa siku kadhaa. Alimwita binti yake na kumuuliza kitu ambacho alitaka kwenda kusomea. Ashura alimwambia mama yake kuwa alitaka kwenda kusomea masuala ya mifugo ili aje awe mtaalamu wa maswala mbalimbali ya mifugo. Jibu la ashura halikumridhisha mama yake “kwani hakuna fani zinazoweza kukufanya ukapata pesa haraka sasa hayo mamifugo mwanangu ya nini wakati hapa nyumbani hata kuku tuu hatuna?” Mama ashura alimuuliza mwanaye kwa unyonge. “mama nawe bwana hebu acha ushamba sasa kwani nani anaenda kusomea kitu cha kumpa pesa haraka? Yaani hapa kuanzia mwakani ndo tunaenda kwenye hizo shule baada ya hapo tuje twende chuo baada ya chuo ndo ajira kwa hiyo hesabia miaka kama kumi mbele ndiyo uanze kuwaza pesa” ashura aliendelea kumwelezea mama yake kwa kina zaidi kwani wao walielekezwa shuleni na walimu wao “ahaa! Hapo sasa nimeelewa mwanangu nakupa baraka zangu zote ufanikiwe kwa kile unachoenda kusomea” ashura alifurahi sana kwani mama yake alikuwa tofauti na wazazi wengine waliowalazimisha watoto wao kwenda kusomea fani ambazo hawakuwa na uwezo nazo na alimuahidi mama yake kusoma kwa bidii.

Mwaka uliofuata wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza, walienda katika shule zilizoendani na fani zao huku zilizokuwa sehemu finyu zikipanuliwa zaidi ili kuwapa uwigo mpana wanafunzi kujifunza kwa vitendo. Maandalizi ya kuandaa vyuo kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya wanafunzi yalianza mara baada ya mitihani ya muhula wa kwanza ambapo wanafunzi walifanya vizuri katika masomo yao. Waliokuwa hawaamini kama mradi huo ungefanikiwa walianza kushuhudia wenyewe huku wakibaki vinywa wazi na kukosa maneno ya kuongea “dah! Huu mpango ungeanza enzi zetu nadhani nchi ingekuwa mbali sana hongera sana muheshimiwa” aliongea raisi kumpongeza waziri wake aliyekuja na mpangoa ambao hata yeye mwanzoni aliutilia mashaka kama ungefanikiwa. “nashukuru sana mkuu, pongezi zirudi kwako uliyeniruhusu kuyafanya kwa vitendo mawazo yangu, nina imani sasa elimu yetu itapanda kwa kiwango cha juu na nasikia majirani zetu nao wana mpango wa kuiga mtaala wetu, mi nimewaambia waige tuu ila wakichanika msamba watajishona wenyewe” aliongea waziri wa elimu huku anamtoa nje raisi aliyeenda kumtembelea nyumbani kwake. “hahahahahahaha!” Walicheka wote.
 

Attachments

Upvote 0
Back
Top Bottom