Kiendacho kwa mganga hakirudi, Rwanda yasema haitarejesha bilioni 824 za Uingereza baada ya Serikali mpya kughairi mpango wa kupeleka wakimbizi

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Serikali ya Rwanda imesema haitarejesha pesa ilizopewa na Uingereza kwenye mpango walioingia awali wa Uingereza kupeleka wakimbizi nchini Rwanda. Mpaka sasa Uingereza imeilipa Kigali dola za kimarekeani milioni 307.

Awali Rais Kagame wakati wanaingia mkataba alipendekeza kurejesha fedha endapo wahamiaji wasingekubali kwenda Rwanda pamoja na kwamba hawakuwajibika kufanya hivyo.

Waziri mkuu mpya wa Uingereza, Keir Starmer alisema Jumamosi mpango huo ambao Rwanda iliingia na serikali iliyopita ya Conservatives umekufa na kuzikwa.

Pia, soma=> Mwombaji hifadhi wa kwanza apelekwa Rwanda baada ya kukubali kwa hiari kuondoka Uingereza. Apewa Pauni 3,000 (Tsh milioni 9.6)
 
Safi sana mkataba ukiuvunja imekula kwako
Hata PM mpya alisema wakishika nchi jambo la kwanza anafuta haya ya Rwanda

Dili la wahindi limekufa
Alianza aliekuwa waziri wa mambo ya ndani wa zamani Priti Patel na Sunak
 
Serikali ya Rwanda imesema haitarejesha pesa ilizopewa na Uingereza kwenye mpango walioingia awali wa Uingereza kupeleka wakimbizi nchini Rwanda. Mpaka sasa Uingereza imeilipa Kigali dola za kimarekeani milioni 307.

Awali Rais Kagame wakati wanaingia mkataba alipendekeza kurejesha fedha endapo wahamiaji wasingekubali kwenda Rwanda pamoja na kwamba hawakuwajibika kufanya hivyo.

Waziri mkuu mpya wa Uingereza, Keir Starmer alisema Jumamosi mpango huo ambao Rwanda iliingia na serikali iliyopita ya Conservatives umekufa na kuzikwa.

Pia, soma=> Mwombaji hifadhi wa kwanza apelekwa Rwanda baada ya kukubali kwa hiari kuondoka Uingereza. Apewa Pauni 3,000 (Tsh milioni 9.6)
🤔🌜Tusubiri wao watasema nini
 
Nilisema PK katia kibindoni nilimaanisha hazirudi.

Uingereza ndo walowafuata Rwanda kueleza shida yao na Rwanda wakasema leta pesa tupige kazi.

Lakini pesa hiyo kurudishwa haikuwa sehemu ya makubaliano.
 
Back
Top Bottom