Kiepe kimeisha, faida 10! Nakosea wapi?

Nkwe2RG

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2014
Posts
231
Reaction score
224
Nimejaribu kuwekeza kwenye matumbo ya wapenda chips na kwa bahati 'goli' liko eneo poa kabisa. Sasa kali ya mwezi Mei ni pale kijana wangu na kwa ufuatiliaji wangu wa karibu, mauzo ya siku 6 yalipofikia elf 80 tu na huku nikibakiwa na elfu 10 tu kama faida baada ya kutoa elfu 55 ya viazi na zagazaga zingine kama sehem ya mtaji.
Hii ina maana kwa mwezi ni sawa na kiasi hicho (elfu 10) mara tano sawa na elfu 50 tu kama faida. Nauza chips mayai tu.

Tafadhali naomba maujanja zaidi ya biashara hii kwa maana nilianza kusoma nyuzi mbalimbali humu kabla sijafungua goli
 
ngoja walioko vibandani waje....hata mm nahitaji kujua zaidi hapa. Wapi panakosewa???...ngoja wadau waje
 
Hhaaaa vident hapana boss, ila labda kwa vile nachomoa hela kidogo ya msos, sasa jee nisile ili tu nipate faida?
 
Embu elezea vizuri ili niku elewe mana kama nime kuelewa vzr baada ya hapo unatoa hela ya kununulia mzigo sasa kila siku una nunua mzigo.. Gunia dogo lina kaa ndoo 4 na visado viwili... Ndoo moja kubwa ina toa sahani kuanzia 25 hadi 30.. Ukiuza kwa 1500 sahani kavu zidisha una pata kiasi gani.. Na kama ukiuza chips yai unatoa sahani nyingi zaidi ya hizo na bei n kubwa.. Mm watu wangu nime wapa uhuru kila siku kuna kiasi cha pesa nime wambia wawe wana niletea arafu wao wata juwa wata jilipa vipi na hapo hapo wata toa hela za kununulia mzigo
 
Hhaaaa vident hapana boss, ila labda kwa vile nachomoa hela kidogo ya msos, sasa jee nisile ili tu nipate faida?
Ukiwa mfanyabiashara lazima ujue hela ya biashara ni ya biashara tuu,.kama unatumia hela ya biashara kula,kuvaa,vocha,sijui usafiri n.k huwezi kuiona faida ya hiyo biashara,..lazima uwe serious kidogo na kitu unachokifanya.
 
Pia ongeza na mishkaki na kuku wa kukaanga.. Mishkaki ina hela sana wanunulie steki nusu ya 3500 hiyo ina uwezo wa kutoa hadi mishakaki 20 ya jero jero.. Kingine wachunguze kwenye kipimo wasi jaze sana wala wasipunje sana..
 
afate huu ushauri,mimi pia yalinkuta mtaji wa laki 8 naondoka na jero faida kwa sikunikatumia njia iyo ikansaidia maana vijana wezi sana wanauza wanasema hawauzi,hata tray za mayai zinaisha wanakuambia hatujauza mayai yalienda wapi sijui,nikatimua nikaweka wingine kwa makubaliano hayo na tukafikia lengo na soda maji wakawa wananiuzia
 
Subiri wenyewe waje mkuu
 
Pia ongeza na mishkaki na kuku wa kukaanga.. Mishkaki ina hela sana wanunulie steki nusu ya 3500 hiyo ina uwezo wa kutoa hadi mishakaki 20 ya jero jero.. Kingine wachunguze kwenye kipimo wasi jaze sana wala wasipunje sana..
Kwa minimum kwa siku anatakiwa alete sh ngapi?Just to know kwa mtu anaetaka shift kwa mfumo huu
 
Nami ili kuwa hivyo hivyo nishapata sana hasara kwenye biashara ya chips lakini siku kata tamaa nikawa naji funza taratibu mwisho nika shauriwa nifanye njia hiyo.. Sasa hivi nashukuru Mungu hela naiona.
 
Kwa minimum kwa siku anatakiwa alete sh ngapi?Just to know kwa mtu anaetaka shift kwa mfumo huu
 
Kwa minimum kwa siku anatakiwa alete sh ngapi?Just to know kwa mtu anaetaka shift kwa mfumo huu
Fanya hivi wanunulie kila kitu wape arafu wambie kila siku wawe wana kupa 20,000/= wao wata juwa wata jilipa vipi na hela ya kununulia mzigo wata towa wao na siku wakiona hawa wezi kuendelea na biashara wananunua mahitaji yote uliyo wakabidhi mna achana kwa amani na weka mtu mwingine njia hii ina kufanya uwe na mda wako mwingi wa kufanya mambo yako mengine na una wapa wao uhuru wa kufanya mambo yao mradi wewe jioni una kwenda chukua hela yako.. Pia roho isiwe ina kuuma unapo ona wana uza sana wakati wewe wana kupa 20,000/= ridhika na hicho mlicho kubaliana mana 20,000/= kila siku si haba kwa mwezi 600,000/= kama una ndoto nyingine una weza fungua biashara nyingine..
 
Thank you....
 
Elfu kumi faida kwa siku ni kidogo? Acha tamaa kijana
Hapana. Sio elf 10 kwa siku. Hii elf kumi ni baada ya kuuza chips kwa siku 6. Ni kile kigunia kidogo cha nadhan ndoo nne na ushee cha viaz
 
Nashkur mkuu. Hivi, ili ionekane umeuza sana kwa siku upige atleast kiasi gan cha viaz. Maana huenda siioni faida kwa vile nimechukua muda mrefu kumaliza mzigo (siku 6) tena ni ule mdogo(nusu gunia wa sh50,000/-), sio gunia la laki na ngapi sjui
 
Biashara ya chipsi inalipa ukiwa eneo ambalo unaweza kuuza walau gunia 2 kwa siku vinginevyo ni moja kati ya biashara pasua kichwa.
 
Mkuu, kijana anatumia elfu 5 tu ili apate nguvu ya kupiga kazi ila matokeo ndo kama hivi siku 6 faida elfu kumi. Hata watumwa walipewa chakula angalau waishi, wapige mzigo.
Ukiwa mfanyabiashara lazima ujue hela ya biashara ni ya biashara tuu,.kama unatumia hela ya biashara kula,kuvaa,vocha,sijui usafiri n.k huwezi kuiona faida ya hiyo biashara,..lazima uwe serious kidogo na kitu unachokifanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…