Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 3,978
- 6,739
Ebu nikuulize swali Je, Maisha yako yana Thamani ya Kiasi gani? Moyo unaweza kununuliwa kwa kiasi gani?, Je Ini lako lina thamani ya kiasi gani? Je hiyo figo hugharimu kiasi gani? Kama mtu una tamaa ya pesa ya haraka haraka unaweza kuingia mtandaoni na kuanza kuuliza bei ya viungo vyako.
Ila kama binadamu na tukiwa viumbe wenye utashi basi tunahitaji kuibua maswali mbalimbali ya kimaadili na kifalsafa tunapojaribu kujibu swali: thamani ya maisha ni kiasi gani? Wengi tutasema thamani ya maisha ni kubwa sana na haina mfano.
Mataifa kama India, Bangladesh, Pakistan, Uturuki, Brazil pamoja na Kosovo ndo yanayoongoza kwa kuwa na kesi kadhaa za mara kwa mara za watu kutolewa viungo vya miili yao na kuuzwa kwa pesa ndefu. Sio ajabu kusikia nchi kama Marekani, Uchina pamoja na nchi za Ulaya zipo mstari wa mbele sana katika mahitaji haya ya viungo kama figo, bandama, utumbo na kadhalika.
Ila kama binadamu na tukiwa viumbe wenye utashi basi tunahitaji kuibua maswali mbalimbali ya kimaadili na kifalsafa tunapojaribu kujibu swali: thamani ya maisha ni kiasi gani? Wengi tutasema thamani ya maisha ni kubwa sana na haina mfano.
Mataifa kama India, Bangladesh, Pakistan, Uturuki, Brazil pamoja na Kosovo ndo yanayoongoza kwa kuwa na kesi kadhaa za mara kwa mara za watu kutolewa viungo vya miili yao na kuuzwa kwa pesa ndefu. Sio ajabu kusikia nchi kama Marekani, Uchina pamoja na nchi za Ulaya zipo mstari wa mbele sana katika mahitaji haya ya viungo kama figo, bandama, utumbo na kadhalika.
Kutokana na ukakasi wa mada sitoweka picha za matukio halisi!
Ingawa kuna kitu kinaitwa organ harvest ambapo hufanyika mara baada ya jopo la madaktari kuwa na uhakika kuwa mtu fulani atafariki dunia na hakuna namna ya kumuokoa basi hutoa viungo kadhaa ili vipate kwenda kusaidia watu wengine.
Mfano mzuri ni watu waliopo kwenye coma pamoja na wale ambao ubongo unashindwa kufanya kazi na mwili ukiwa kwenye hali nzuri basi hufanya organ harvest. Kitaalamu hii wameipatia jina la “Killing on Demand”, Uchina wao ndo wana hifadi kubwa ya viungo zaidi ya maelfu ya viungo.
Ila kitu ambacho ni ajabu sana ni uwepo wa madaktari ambao sio waaminifu na weledi wa kazi yao, kwani hufanya kazi za kuwatoa viungo baadhi ya wagonjwa bila ya ridhaa zao wala wao kufahamu kuwa wametolewa viungo.
Waliopo kwenye hatari kubwa ni wale wagonjwa wanaopelekwa kwenye mahospitali na wanakosa ndugu mathalani kutambulika, basi mara kadhaa hujikuta ni wahanga wa michezo hii pasipo hata wao kufahamu kinachoendelea.
Ukikaa chini na kuzungumza na Daktari Sam Kazemi ambaye ni mtaalamu haswa wa kutenganisha viungo vya watu kwa ajili ya kwenda kwenye mahospitali mengine ili wahitaji wapate kuwekewa na kupona. Biologal Resource Center wao walikuwa wakiingia makubaliano na watu ambao mara kadhaa ni wazee.
mMakubaliano ya Biologal Resource Center kuchukua maiti zao na kutenganisha viungo kadhaa na kuvifanyia biashara maeneo kadhaa yenye uhitaji, ajabu ni kwamba mpaka sasa watu zaidi ya elfu tano wameshaingia makubaliano na Biologal Resource Center na maiti zao zimeshafanyiwa maelekezo ya kitabibu na hawa watalaamu.
Ukiachana na wazee, kundi jingine ni kina mama wajawazito hususani ni wale ambao wanajifungua kwa njia ya C section. Hili ni kundi ambalo lipo kwenye hatari endapo Mama mjamzito akifanyiwa upasuaji pasipo kuwepo na mtu wa karibu na mtaalamu akiingia tamaa basi anaweza kuondoa baadhi ya viungo kutoka kwenye mwili wa mama husika.
Hawa Biologal Resource Center walikuwa na na mikataba mingi ya kupeleka viungo vya miili ya watu sehemu tofauti totauti:
- Kichwa pamoja na Uti wa mgongo vilipelekwa jeshini kwa ajili ya tafiti za kisayansi.
- Viungo vya uzazi vilipelekwa kwenye vyuo vikuu kama Arizona State University, University of Arkansas for Medical Sciences na kadhalika
- Miguu na Mikono ya marehemu vilipelekwa huko Chicago Orthopaedic Laboratory, Stanford University, Orthopaedic Research Laboratories.
- Maini, figo, bandama pamoja na Moyo huwa waliviuza kwa watu ambao hawatakiwi kufahamika kwa umma (huwa ni confidential)
Mwili wa binadamu ndani ya kituo cha Biologal Resource Center ulikadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya mpaka milioni 16 huku ndugu wa marehemu wakipewa fomu na mikataba ambayo hutakiwa kutia saini na wakati mwingine huwa na maelezo mengi yenye kuhitaji umakini mkubwa kwani ndani ya mikataba hiyo, ndugu wa karibu wa marehemu wanakuwa wametoa ruhusa ya Biologal Resource Center kuutenganisha mwili wote na kuuza sehemu ya viungo vya marehemu.
Sheria za matumizi ya viungo hivi imekuwa changamoto kubwa huku wengine wakiona kama kuna matumizi yasiyo rafiki ya viungo hivi. 2013 kulikuwa na Bwana Mmoja anaitwa Arthur Rathburn ambaye alikuwa afanya kazi haramu za Biologal Resource Center, ambapo maafisa usalama wa FBI walikutana zaidi ya tani 10 za maiti zikiwa zimegandishwa kwenye barafu, viungo zaidi vya binadamu 1,755 ikiwemo vichwa 281, mikono 241, miguu 337 pamoja na uti wa mgongo 97.
Ili kuvibeba kutoka eneo la tukio walihitaji kuwa na mifuko 142 ambapo kila mfuko ulibeba viungo visivyopungua 36 vya marehemu hao, tukio hili lilikuwa kubwa sana kiasi cha kwamba iliwabidi polisi kuhifadhi viungo vyote hivi kwenye kambi ya kijeshi kwa ajili ya usalama.
Walipokwenda kwa Arthur Rathburn ndo waliishiwa nguvu kabsa kwani walikuta miili mingi ikiwa imeoza pamoja na vijusi vinne ambavyo vilikuwa vimehifadhiwa vizuri. Polisi walipojaribu kumhoji Stephen Gore alionekana kuwa jamaa alikuwa akiuza baadhi ya viungo kama viungo vya watoto kwa watu binafsi ambao hakutaka kuwataja, alidai kuwa ni watu wakubwa sana serikalini na wengine ni viongozi wa dini, hata karatasi na mikataba ya mauziano yao ya viungo hivyo alichoma punde tu baada ya makabidhiano yao.
Binafsi yeye Gore alidai kuwa alichotaka kufanya ni kusaidia familia kiuchumi huku akisaidia pia harakati za maendeleo ya sayansi na teknolojia kwani viungo kama ubongo na moyo alikuwa akivitoa bure kwa maabara za kitafiti pamoja na vyuo vikuu duniani.
Mwaka 2019 katika ofisi za Stephen Gore walikuta dhakari zaidi ya ishirini zikiwa kwenye fridge zimehifadhiwa huku kukiwa hakuna taarifa za wapi haswa wanataka kupeleka hivi viungo. Baadhi ya miili imekuwa ikitumia kwenye tafiti ya milipuko ya kijeshi haswa wakiwa kwenye majaribio ya silaha za moto, pia baadhi ya miili imekuwa ikitumia kwenye tafiti za madawa na tiba kwenye maabara za kijeshi huku tafiti hizi zikiwa ni siri kiasi kwamba Stephen Gore hawezi kuuliza wanakwenda kuzifanyia nini maiti hizi.
Maafisa wa FBI walipoingia kwenye ofisi hizi walibaki kushangaa kwani baadhi ya maiti zilikuwa mfano wa Frankenstein, kwani miguu, shingo pamoja na mikono ilikuwa imeshonwa, kama una roho nyepesi lazma urudishe chenji au kuzima kabsa. Kwa sasa kituo hiki hakifanyi kazi tena na kifungwa huku Stephen Gore akiwa chini ya ulinzi akikabiliwa na kesi takribani tano za kujibu.
Thamani ya maisha ni kubwa sana, maisha hayana spare tyre! Maisha ni moja pekee na hakuna timeout kwamba uende water break! Maisha ni sasa! Maisha ni wewe! Wapo watu wanaouza figo ili wapate pesa na mwishowe kujituka wakitumia pesa zao ili kupata figo nyingine kwa ajili ya ustawi wao.
Maisha yako ni jukumu lako! Usipuuze wala kuchukulia poa kitu chochote ambacho kinatokea kwenye maisha yako! Maisha ni zawadi tosha ambao Mungu amekupatia wewe, usijichukulie poa hata kidogo.
Ubarikiwe sana! Na uwe na wakati mwema!