sasa nimeamini juu ya usemi unaosema usimdharau usiyemjua. mimi na kificho wote ni watanzania lakini nikiri kwamba sikumfahamu uwezo wake wa kuongoza kwa sababu yeye ni speaker wa baraza la wawakilishi zanzibar ambalo kimsingi ni ngumu kupata vikao vya baraza la wawakilishi kwa sababu ya miundo mbinu ya mawasiliano. Nimemkubari sasa kificho kwamba ni speaker bora kwa jinsi alivyotawala vikao vya awali kama mwenyekiti wa muda wa bunge. Ni mtulivu, hana jaziba hata anapopata misukosuko ya maneno makali, ( kumbuka mch. mtikila na mkosamali walipomwinukia) bado alitulia na kuonyesha roho ya uongozi. Nimependa pia anavyoweza kusoma hali ya mazingira (Audience atmosphere). Ni mahiri kujua mawazo yanayoendelea katikati ya watu, lakini anaweza kujifanya kama haelewi ili kuwapata watu wote. ushauri wangu kwa sita ambaye amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa kudumu wa bunge la katiba, ni kuchukua creterias kadhaa za mzee kificho ili tuone majadiliano yenye tija ktk bunge hili. Tatizo ninalopata sasa ni kwamba makami mwenyekiti wa bunge atatoka zanzibar na awe mwanamke. bila sharti hilo ambalo kwa maoni yangu siliafiki, Mzee pandu kificho alistahili sana kuwa makamu mwenyekiti. Ntamissi umakini, upole, busara, kuchukuliana, ambako kificho ameonyesha. hata hivyo umeandika historia mzee.