Kificho ndiye Speaker wangu.

magiri

Member
Joined
Apr 10, 2011
Posts
40
Reaction score
21
sasa nimeamini juu ya usemi unaosema usimdharau usiyemjua. mimi na kificho wote ni watanzania lakini nikiri kwamba sikumfahamu uwezo wake wa kuongoza kwa sababu yeye ni speaker wa baraza la wawakilishi zanzibar ambalo kimsingi ni ngumu kupata vikao vya baraza la wawakilishi kwa sababu ya miundo mbinu ya mawasiliano. Nimemkubari sasa kificho kwamba ni speaker bora kwa jinsi alivyotawala vikao vya awali kama mwenyekiti wa muda wa bunge. Ni mtulivu, hana jaziba hata anapopata misukosuko ya maneno makali, ( kumbuka mch. mtikila na mkosamali walipomwinukia) bado alitulia na kuonyesha roho ya uongozi. Nimependa pia anavyoweza kusoma hali ya mazingira (Audience atmosphere). Ni mahiri kujua mawazo yanayoendelea katikati ya watu, lakini anaweza kujifanya kama haelewi ili kuwapata watu wote. ushauri wangu kwa sita ambaye amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa kudumu wa bunge la katiba, ni kuchukua creterias kadhaa za mzee kificho ili tuone majadiliano yenye tija ktk bunge hili. Tatizo ninalopata sasa ni kwamba makami mwenyekiti wa bunge atatoka zanzibar na awe mwanamke. bila sharti hilo ambalo kwa maoni yangu siliafiki, Mzee pandu kificho alistahili sana kuwa makamu mwenyekiti. Ntamissi umakini, upole, busara, kuchukuliana, ambako kificho ameonyesha. hata hivyo umeandika historia mzee.
 
Ni kweli Mzee Kificho angeendelea hata kwa umakamu tuu!wazanzibar wamekomaa kisiasa ndiyo maana wameweza hata kutuingiza king ktk muungano
 
Alianza vema hapa mwisho naona mashinikizo yalianza kumchanganya
 
...dosari ni kushindwa kushinda shinikizo la ccm kuhusu kura ya siri...
 
Umemaliza maneno yote..kwa kifupi umenifilisi ....itoshe kusema hakika mzee kificho nafasi anayoiacha ndo yake haswaaaaa
 
Mzee wa "salfasa". Yuko juu kiukweli, hata mimi nimemkubali ingawa ni mara ya kwanza kumuona akiwa kazini.
 
Hata miye nimemkubali Kificho sioni sababu ya kumtafuta makamu, wakati Mzee Kificho anatutosha.
 
Tatizo la Kificho alifichwa Zanzibar asingefichwa kifichoni tungemjua mapema Kificho wetu...nitammiss sana.
 
kweli wazanzibar wana spika wa nguvu
 
Alipaswa kuwa makamu wa sitta, ingawa anatoka nchi jirani ya zanzibar!
 
Nimemkubali sana huyu mzee. Maana 6 anazungumza mno na mbwembwe nyingi mpaka anaboa. Kwa mwendo wa hili Bunge anaweza kususiwa vikao hasa katika masuala ya muungano na muundo wa serikali ameanza kutangaza misimamo mapema na kuwashambulia maadui wake mapema.
 
Nami nimemkubali Kificho katulia sana ktk maamuzi na msikivu asie na jazba wala majibizano
 
Mzee wa "salfasa". Yuko juu kiukweli, hata mimi nimemkubali ingawa ni mara ya kwanza kumuona akiwa kazini.

Dah, dada FF, nitakosa hekima za huyu mzee! Kama wachangiaji walivyosema alipaswa awe angalau makamu, lakini hizi gender balance, anyway, mzee ana hekima sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…