Kisiasa wazanzibar ni makini sana kuliko kwetu huku tanganyika. Hii ni kwa sababu ya mikiki mikiki ya CUF iliyozaa serikali ya umoja . Serikali ya umoja kati ya CCM na CUF imewaunganisha sana wanasiasa wa visiwani na kuona umuhimu wa kushirikiana kama nchi na kupunguza maslahi ya itikadi za vyama badala ya maslahi mapana ya nchi . Ndio maana kwa Mhe. Pandu Kifucho imekuwa ni rahisi kuliendesha hili bunge maalumu kwa sababu wao zanzibar hizi siasa za bunge la muungano walisha ziacha siku nyingi. Ni kwa sababu ya ugeni tu uwezo wake anaonekana ni mahiri hata zaidi ya Samwel Sitta kwa sababu yeye ni mstaarabu na mvumilivu na hana jazba hata kidogo. Pamoja na speed na standards za Mhe Sitta, mbwembwe na majivuno yasiyo na maana ya kibongo yanampunzia sifa muhimu kama mzee Mhe. Kificho.