SteveMollel
JF-Expert Member
- Jul 12, 2015
- 8,797
- 25,177
- Hili ndo' sakata la 'wanted man' wa Uingereza na kupotea kwa wanawake wawili huko mji wa Aba, Nigeria.
Mwezi ulopita, mkuu wa jeshi la Polisi la Nigeria, IGP Kayode Egbetokun, hakuwa na namna nyingine zaidi ya kuivaa kesi hii matata kwakuwa ubalozi wa Ghana, familia ya wahanga pamoja na wanaharakati wa haki za binadamu walikuwa wamemkalia kooni.
Anamvutia simu Kamanda wa kikosi maalumu cha kiintelijensia (IRT), DC Sanusi Mohamed (pichani), na kumpa maelekezo ya kutuma kikosi chake kwenda jimbo la Abia, mji wa Aba, kushughulikia kesi ya kupotea kimiujiza kwa mabinti wawili; mmoja mnaijeria na mwingine kutokea nchini Ghana.
Kesi hii inajivuta mno, sasa ikiwa ni wiki mbili zishapita ila hamna mrejesho wowote ingali mtuhumiwa mkubwa tayari yupo mikononi mwa polisi tangu mapema May 8.
Hali hii inazua mashaka kwa polisi wa jimbo hili, kuanzia mji wa Aba mpaka Umuahia alipokuja kuhamishiwa chini ya kitengo cha Anti-kidnapping Force, ya kwamba kuna kitu wanakificha ama kuna jambo wanalijua.
Hata mazingira ya mtuhumiwa akiwa hapa kizuizini yanajenga mashaka sana. Bwana huyu anakula anachokitaka muda anaotaka, anatumia simu yake kama kawaida tena kwa 'free access of data'.
Sasa yupo rumande ama kabadili makazi ya kuishi?
Kikosi cha IRT, ndani yake akiwemo afisa Ugochukwu Oguobu, ndo' kinatumwa kikamchukue mtuhumiwa huyu pamoja na makabrasha yake yote ya kesi aletwe hapa makao makuu, Abuja.
Kesi inahamishiwa makaoni.
Hivyo siku ya Jumanne, tarehe 21 May, kikosi cha IRT kinamchukua mtuhumiwa toka kituo cha polisi pamoja na mafaili yake ya kesi na kila aina ya ushahidi unaoweza kubebeka, safari ya kwenda Abuja inaanza.
Safari hii ya kutoka jimbo la Abia mpaka Abuja, makaoni, ni ya kugharimu masaa nane tu lakini ikachukua karibu wiki mbili njiani bila ya kufika.
Kama isitoshe, waliotumwa kumleta mtuhumiwa huyu, IRT, wanaishia kumuua wao wenyewe kwenye eneo fulani ndani ya jimbo la Benue.
Sasa nini kilitokea?
Na mtuhumiwa huyu, mbali na majina yake yanayofahamika; Andrew Amechi au David Okorocha, alikuwa ni nani haswa?
Pia alifanya nini kwa mabinti hawa wawili (Celine na Afiba) ambao wamepotea katika mazingira ya kutatanisha isijulikane walipo mpaka leo hii?
Twende Uingereza, mwaka ule 2019, mwezi June. Hapo ndo' kwa mara ya kwanza Andrew Amechi anakamata vyombo vya habari kwa taarifa za uhalifu.
Konstebo Rob Buchanan, afisa wa upelelezi toka kituo cha polisi cha Thames Valley huko mji wa Milton Keynes, ananukuliwa na tovuti ya wanajamii wa eneo hili akiomba msaada wa hadhara kutoa taarifa kumhusu bwana Andrew ambaye anatuhumiwa kwa makosa ya unyanyasaji wa kingono kwa mwanamke fulani hapa Uingereza.
Afisa anamfafanua Andrew kwa mwonekano wake kama mtu mwenye mwili mpana, umri miaka 51, ana kovu dogo kwenye nyusi za jicho la kushoto na urefu wake ni futi tano.
Afisa Buchanan anatahadharisha, "if you see him, do not approach him and call 999."
Baada ya hapa, hamna aliyesikia tena kuhusu Andrew Amechi nchini Uingereza, ardhi iliyomlelea tangu utotoni kwenye mikono iliyomuasili na kumpa maisha mazuri.
Anakimbilia nchini Nigeria na kuweka makazi yake katika jimbo la Abia, na hapo ndo' anakuwa ameikanyaga ardhi ya Nigeria kwa mara ya kwanza.
Ardhi ya asili yake.
Lakini hakufika hapa kwa nguvu ya mikono yake pekee.
Abadan.
Alipata mwaliko toka kwa mwanasiasa mkubwa nchini Nigeria ambaye mpaka kifo kinamkuta hajapata kutajwa jina lake wala sababu ya mwaliko huo.
Akafungua account yake ya Facebook kwa jina la Andrew Ameichi na hapo ndo' akaanza kututhibitishia ya kwamba, chui habadiliki madoa.
Akatuma picha zake mbalimbali; picha akiwa ndani ya nyumba kubwa, ndani ya ofisi kali, ndani ya magari ya chapa ya thamani, ndani ya nguo za gharama.
Ukimtupia macho hauchukui dakika kujua hapa pesa ipo. Na yeye hakusita kuzionyesha kwa kutuma vijizawadi na vijimsaada vya hapa na pale kwa wanawake walokuwa na uhitaji.
Na akalijua hili vema, kwenye kula huku yapasa kukaa mbali na mkono wa kipofu. Hivyo hakuona tabu kupita polisi kutoa pesa za brashi ya kufutia viatu na leso za kufutia jasho, polisi wakawa watu wake wa karibu.
Wakati huo picha zake za mtandaoni, kingereza chake cha mdomoni na pesa yake mfukoni inaendelea kuwavuta wasichana lukuki katika kasri yake kama kuku anayetupiwa punje za mchele.
Anadonoa punje na punje, anasogea, punje na punje, mara ndani.
Mlango ukifungwa ndo' unaifahamu rangi halisi ya Andrew. Hapa hayupo wa kukutetea. Ni kubakwa, kuteswa, na hata kuuawa kwaajili ya viungo vya mwili.
Haya yote hayakuwa story mpaka pale yalipokuja kuwafika wasichana hawa wawili, Celine na Afiba, Jumapili ya 27 April, 2024.
Tukio hilo lilianzia mwaka 2022, miaka miwili nyuma, ambapo Celine alianzisha urafiki na bwana Andrew katika mtandao wa Facebook. Wakajuana kwa kuchat bila ya kuonana na hata ukapita muda mrefu wa ukimya baina yao kabla ya kuja kukutana tena mtandaoni na bwana Andrew kumtaka Celine amtembelee nyumbani kwake.
Kwenye video (hapo chini) Andrew anamwambia Celine, njoo na rafiki yako kwenye jumba langu lenye vyumba sita vya kulala, tutafurahia kwa pamoja weekend hii.
Rafiki huyu ni nani? Afiba, dada mwenye utaifa wa Ghana ambaye ameolewa na mzungu (Mr. Tony) mwenye asili ya Ujerumani na Lebanon wakiishi zao huko Dubai.
Afiba anamuaga mumewe kuwa ana safari ya kwenda Nigeria kuhudhuria harusi ya rafiki yake Blessing, mume anamruhusu, anaenda zake na wanakuwa wakiwasiliana kwa njia ya 'calls' na whatsapp kupeana update.
Baada ya masaa kumi angani, anafika uwanja wa Lagos kisha baada ya lisaa limoja, uwanja wa Porthart Court anapokutana na rafiki yake Celine.
Muda huo Celine ashapokea naira laki moja kutoka kwa Andrew ili aje kuitumia kama nauli ya kuwatoa mji wa Porthart Court jimbo la Rivers, mpaka mji wa Aba, jimbo la Abia anapoishi yeye.
Ajabu, ile harusi ya Blessing ikahairishwa. Afiba hakuhudhuria tena kama alivyomuaga mumewe kule Dubai na basi anaungana na rafiki yake Celine kwenda kuonana na bwana Andrew siku ya tarehe 27, April.
Mtoko huu hakumwambia mumewe.
Na hapa inabidi tufahamu, Mr. Tony (mume wa Afiba) alishawahi kukwaruzana na mkewe juu ya urafiki wake na hawa 'single ladies' Celine na Blessing (pichani). Urafiki huu haukuwa unampendeza machoni pake lakini bahati mbaya jambo hili halikuwahi kuzaa matunda kwa mkewe.
Celine na Afiba wanaingia kwenye bolt, safari ya kwenda mji wa Aba inaanza.
Baada ya masaa mawili kasoro, wanaingia mji wa Aba, na mwenyeji wao anawataka wafikie Panyu Hotel & Resorts.
Kwanini hakuelekeza waende nyumbani kwake moja kwa moja?
Simple.
Andrew hakutaka kuacha rekodi ya kupatikana kwa anwani ya mahali anapoishi. Kama Bolt ingelikuja moja kwa moja mpaka getini kwake, basi ingelikuwa rahisi kuwa-track wanawake hawa walipotokea mpaka walipofikia.
Hivyo anakutana na wanawake hawa hotelini alafu ndo' anawachukua kuwapeleka kwake yeye mwenyewe.
Wanapofika ndani, Celine anachukua video ya mazingira kuonyesha kuwa wamewasili (tazama pichani) lakini baada ya muda mchache, Celine anatuma ujumbe mfupi wa sauti kwa dada yake ya kwamba wametekwa.
Afiba naye anajaribu kuwasiliana na Blessing kumwomba msaada wa haraka. Anamtumia location ya eneo walipo. Anasema Andrew ametoka na anapomsikia akirudi anamwonya asimpigie simu kwani ataisikia.
Lakini baada ya hapo simu zao hazikupatikana tena.
Dada yake Celine, kwa uzito wa habari hizi, anafunga safari ya haraka kwenda mji wa Aba. Anaripoti kituo cha polisi maramoja akisema ndugu yake ametekwa akiwa pamoja na rafiki yake Afiba katika makazi ya bwana Andrew Amechi.
Hata location ya makazi hayo anayo.
Ila huwezi amini, toka siku hiyo ya tukio tarehe 27 April 2024, jeshi la polisi la mji wa Aba lilikuja kumtia nguvuni bwana Andrew baada ya kupita siku kumi mbele, Jumatano ya tarehe 8 May.
Just imagine.
Siku hiyo polisi, baada ya shinikizo kubwa, wanafika nyumbani kwa Andrew na kufanya msako. Humo wanapata begi, simu na kadi ya benki ya Celine. Pia wanapata hati ya kusafiria ya nchi ya Ghana.
Kuhusu Celine na Afiba, haijulikani wako wapi.
Andrew anapoulizwa anakiri ni kweli walikuja kumtembelea nyumbani kwake lakini walishaondoka na hajui wameelekea wapi.
Sasa waliondokaje wakaacha begi, simu, kadi na hati ya kusafiria nyumbani kwako?
Kimya.
Mdogo wake Celine kule nyumbani, Porthart Court, naye akasema siku ya tarehe 27 April, siku ya tukio la utekaji, ujumbe wa muamala uliingia kwenye iPad ya Celine aliyoiacha nyumbani.
Ujumbe huu ulihabarisha kutolewa kwa kiasi cha Naira milioni moja kutoka kwenye akaunti ya Celine kwenda kwenye akaunti ambayo ilimtumia Naira laki moja hapo awali.
Hii ndo' ile laki moja aliyotuma bwana Andrew kama nauli ya Celine na Afiba. Unaikumbuka?
Sasa ndo' hapa Andrew anatiwa ndani katika kituo cha polisi cha mji wa Aba, baadae anahamishiwa katika kituo cha mji wa Umuahia, yote ndani ya jimbo hili la Abia.
Kwa wiki mbili tena mbele, kesi hii inakwama, haisogei, mpaka inapokuja kutiwa shinikizo la mwanaharakati na mwanasheria toka 'BEHIND BARS HUMAN RIGHT FOUNDATION', bwana Harrison Gwamnishu na pia ubalozi wa Ghana nchini Nigeria.
Ndipo Tarehe 21 May, Andrew anakabidhiwa kwa kikosi cha IRT (Intelligence Response Team) ili asafirishwe kwenda Abuja, makao makuu, kwaajili ya mahojiano zaidi.
Safari hii inayoanzia hapa mji wa Aba, jimbo la Abia, itakatiza jimbo la Enugu, Benue kisha kuingia Abuja. Mwendo wa masaa nane tu.
Lakini wakiwa njiani, ikiwa ni siku ya kumi sasa wanatembea tu, ripoti inatoka tarehe 1 June ya kuwa Andrew ameuawa alipojaribu kuwatoroka askari.
Mauaji yake yametokea jimbo la Benue, jimbo la mwisho kabisa kulikabili kabla ya kuhitimisha safari ya makao makuu, Abuja.
TUSUBIRIE SEHEMU YA PILI.

- Sasa nini haswa kilitokea?
- Hatma ya Celine na Afiba ni nini katika sakata hili?
- Polisi wamefikia wapi?
- Wahanga wengine je?
TUSUBIRIE SEHEMU YA PILI.