KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,789
- 4,951
Mioyo ya nyama imeumizwa na kusikitishwa mno na kifo cha Binti mwenye ualbino Asimwe aliyeuawa kikatili na viungo vyake kunyofolewa na kila kona tunasikia maoni ya watu wakionesha kuumizwa sana.
Kifo cha Asimwe kimetufundisha jambo moja kubwa ,kwamba bado Taifa lina uhitaji mkubwa wa adhabu ya kifo Ili kukomesha ukatili. Hili litukumbushe kama Taifa kwamba kama kusipokuwa na adhabu za vifo, bado wakina Asimwe wataendelea kuumizwa kikatili.
Huu ni ushauri wangu katika utekelezaji wa adhabu ya kifo. Baada ya adhabu ya kifo kutolewa na hakimu au jaji na baada ya rufaa zote kusikilizwa na mstakiwa kushindwa rufaa ,Rais asipewe mamlaka ya kusaini adhabu ya kifo pekee yake maana itaonekana kama Rais ndio kaamuru na Rais anaweza kujisikia vibaya kufanya hivyo na ndio ugumu wa utekelezaji wa adhabu ya kifo unapokuja.
Baada ya mhukiwa kushindwa rufaa, bunge lipewe mamlaka ya kupiga kura kama utekelezaji ufanyike ama laa. Kwa Nini bunge? Kwa sababu wabunge ni wawakilishi wa wananchi hivyo wanakiwa kuamua badala ya wananchi wengi.
Au njia nyingine ya utekelezaji wa adhabu hii ni kutengenezwa mfumo àmbao utaruhusu wananchi kupiga kura mtu aliyehukumiwa adhabu ya kifo itekelezwe au isitekelezwe. Wananchi wengi wakishiriki itasaidia wahalifu kuogopa jukumu ya Umma.
Nasimama na haki ya Asimwe, Mungu amlaze mahali pema peponi.