Mchezo wa ndondi na shughuli zote nchini Ghana vimesitishwa kufuatia kifo cha bondia wa uzani wa kati,
Ernest Akushey, maarufu kama
Bahubali, aliyefariki siku 11, ikiwa ni baada ya pambano lake mjini
Accra.
Bahubali, mwenye umri wa miaka 32, alifariki dunia siku ya Jumanne. Ingawa chanzo halisi cha kifo chake hakijathibitishwa, taarifa za awali zinaashiria kuwa huenda kilihusiana na majeraha ya ndani aliyoyapata wakati wa pambano lake la hivi karibuni.
Akushey alipambana na
Jacob Dickson katika Ukumbi wa Ndondi wa
Bukom Boxing Arena, jijini
Accra, Septemba 12.
Katika taarifa rasmi,
Mamlaka ya Michezo ya Taifa (NSA) ilielezea kusitishwa kwa shughuli zote za ndondi nchini kama
“hatua muhimu” ya “kulinda maisha, kuhifadhi heshima ya mchezo na kuhakikisha mustakabali wake.”
Mamlaka pia imetangaza mpango wa miaka mitano wa kuanzisha viwango salama vya kitaalamu na vinavyolingana na viwango vya kimataifa kwa ajili ya mchezo wa ndondi.
Vyombo vya habari vya Ghana na vyanzo vingine katika mitandao ya kijamii zinasema kisa hicho ni cha pili nchini Ghana ndani ya kipindi cha miezi sita, hali inayochochea upya mjadala kuhusu viwango vya usalama katika mchezo huo.
Rest In Peace Champ 🏆