Kifo Cha Balozi Paul Rupia: Dar es Salaam Tumefiwa

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
KIFO CHA BALOZI PAUL RUPIA: DAR ES SALAAM TUMEFIWA

Sidhani kama kuna mtu ana ujasiri wa kunyanyua kalamu yake pale Abdallah Tambaza atakapoandika historia yoyote inayuhusu Dar es Salaam iwe matukio au iwe taazia.

Naitazama taazia ya Balozi Paul Rupia baada ya kumaliza kuisoma na kuna kitu kinachogonga kichwani kwangu kama vile kuniuliza, ''Hivi kweli huna lolote la kusema kuhusu Balozi Paul Rupia?''

Najijibu mwenyewe, ''Vipi nitakosa la kusema kuhusu Balozi Rupia ilhali nimemfahamu kwa miaka mingi na kwa mbali ni jamaa yangu kwa nasaba ingawa ya mbali kwangu binafsi?''

Haya nitakayosema hapa huenda yakawashtua na kuwashangaza wengi.

Ishatokea hivi mara nyingi.

Udugu wetu na ukoo wa Rupia unatoka mbali sana kutoka kwa bibi yetu mkuu Bi Christina mama ya bibi yetu Bi. Deborah Mgone (1890 - 1995).

Bibi zetu hawa ndiyo waliotuunganisha na ukoo wa Rupia.

Sisi leo ni kizazi cha nne kutoka kwa bibi yetu mkuu Bi. Christina.

Hapa unazungumzia historia inakaribia miaka 200.

Kama walivyo akina Rupia kuwa wana nyumba Misheni Kota nasi pia tuna nyumba mbili Misheni Kota hadi leo.

Nyumba nyingine tatu ziko Mtaa wa Swahili moja, Sikukuu zilikuwa mbili sasa imebaki moja.

Moja bibi aliuza.

Hii ilikuwa jirani sana na Saigon Club.

Nyumba hizi tumezaliwa tumezikuta.

Hatujui lini zilijengwa.

Naamini hizi nyumba sasa zina umri zaidi ya miaka 100.

Nyumba hizi zinatukumbusha utoto wetu na kututafsiria mengi katika maisha yetu.

Bi. Christina na Bi. Deborah niliowataja hapo juu hawa wote mimi nimewaona kwa macho yangu na wameondoka duniani mimi nina fahamu zangu kamili.

Na katika dada zetu alikuwapo Christiana kapewa jina la bibi yetu mkuu maarufu tukimwita ''K'' (apumzike kwa amani).

''K'' alikuwa mkubwa kidogo kwangu na alinipokea St. Joseph's Convent School 1967 na yeye alipokewa hapo na kaka yetu Charles Mgone 1965 au 1966.

Ndani ya historia hii vipi nikose la kusema kuhusu Balozi Paul Rupia na ukoo wa Rupia wenyewe na historia ya wazee wetu waliokuwapo wakati sisi tunazaliwa na kaka zetu tuliowakuta mfano wa marehemu Albano, Balozi Rupia na Steven maarufu kwa jina la Mpuya?

Hawa walikuwa watu maarufu bila ya hata kujikwaza.

Nimehudhuria shughuli nyingi na Albano akiwepo lakini huwezi kusikia sauti yake.

Yeye siku zote alikuwa mtu wa kusikiliza.

Mzee Albano alikuwa mtu wa maneno machache mno.

Wakati nafanya utafiti wa kitabu cha Abdul Sykes nilikutana na barua iliyoandikwa na Makata Mwinyimtwana anamwandikia Ally Sykes kuhusu mwanae Makata ambae alikuwa anakwenda kusoma Liberia pamoja na Paul Rupia kwa scholarship ya TANU.

Barua hii nasikitika sana leo kuwa sikuitia maanani asilani.

Nimeisoma nikapita.

Ninachokumbuka ni kuwa Mzee Makata Mwinyimtwana alikuwa anatafuta ushauri kutoka kwa Ally Sykes kuhusu hali ya baadae ya vijana hawa waliokuwa wanakwenda nje kupata elimu ya juu.

Katika msafara huu wa kwenda Liberia alikuwako Ngombale Mwiru.

Huyu Makata Mwinyimtwana kama alivyokuwa John Rupia alikuwa Mwafrika tajiri sana Tanga.

Inafahamika na wengi kuwa Balozi Rupia hakuwa anapenda kueleza si historia yake wala ya baba yake.

Naamini kabisa kama angenyanyua kalamu kuandika kumbukumbu zake hakuna wasiwasi kuwa historia ya baba yake ingefahamika na mengi ambayo leo yanababaisha watu yangekuwa hadhir.

Naikumbuka Misheni Kota ya 1960s na kilichokuwa kinanipeleka ni kuwa hii ilikuwa miaka ya ''Soul Music'' - James Brown, Aretha Franklin, Ottis Redding, Wilson Pickett, Sam and Dave halikadhalika Erick Burdon and The Animals, Mick Jagger and The Rolling Stones, The Beatles nk.

Muziki wa Wamarekani Weusi na Misheni Kota kulikuwa na vijana wapigaji muziki huu katika bendi maarufu za vijana Sparks na The Rifters - akina Sauti Plantan, Lameck Nicodemus Ubwe na wadogo zake Jacob na Esau.

Nikishinda Misheni Kota siku za likizo - ''jam sessions.''

Nikifika hadi nyumbani kwa Mzee Rupia kwa hili au lile na naikumbuka sana ile mikungu iliyokuwa pale nje.

Lakini sikuwa naijua historia ya nyumba ile kuwa ndipo mkutano wa kuunda African Association ulipofanyika mwaka wa 1929 na wakati ule nyumba ile ilikuwa ya Cecil Matola John Rupia akaja kuinunua baadae.

Haya nilikuja kuyajua baada ya kumsoma Daisy Sykes katika kitabu alichohariri John Iliffe.

Nilipokuwa mazikoni tena niko na Abdallah Tambaza nimemuona Ayoub Sykes na dada zake Guru na Miski, Said Mpango na dada yetu Bi. Baya kutoka Msasani wamekuja mazikoni wamebaba maua wamekuja kumzika kaka yao mkubwa Balozi Rupia.

Babu yao Kleist Sykes alikuwa rafiki mkubwa wa John Rupia ndani na nje ya siasa za African Association na barza yao kubwa ilikuwa nyumbani kwa Keist Mtaa wa Stanley na Sikukuu jirani na nyumba ya bibi yangu Bi. Deborah na jirani ya nyumba ya Mzee Maleta na Mzee Kubbe.

Sasa miaka 73 imepita baada ya kifo cha Kleist na kuvunjika kwa ile barza.

Wajukuu ni sisi na tumeihifadhi historia hii ndani ya vifua vyetu.

Paul Rupia kwangu alikuwa ni kaka mkubwa wala sina maingiliano yoyote na yeye.

Wala sikuwa najua kuwa kuna ujamaa baina yetu.

Haya nilikuja kuyafahamu baadae sana.

Mimi na wenzangu Paul Rupia alikuwa ni kaka tu kama walivyokuwa kaka zetu wengine wa Misheni Kota kama Kurwa na Doto Plantan, Malombe, Denis Nicodemus Ubwe kwa kuwataja wachache, wakati ule anasoma Chuo Kikuu Cha Nairobi.

Dar es Salaam tumefiwa.
Balozi Paul Rupia ni sehemu ya historia ya Dar es Salaam.

Tumefiwa na mtu ambae kaona yote kwa macho yake na kaishi maisha ya nyakati zile na kwa hakika alikuwa hazina kwetu lau kama alikuwa kimya katika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.

Ingawa baba yake alikuwa mmoja kati ya waasisi wa TANU na wafadhili wakubwa Balozi hakupenda kueleza haya.

Balozi Rupia yeye kwa ile tabia na hulka yake ya unyofu hakupenda kueleza historia ya Rupia katika kupigania uhuru wa Tanganyika na kuwa baba yake alikuwa mmoja wa nguzo kuu za Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Kaka yetu Balozi Rupia huyu hakutukataza kuandika historia hii yetu kwa faida ya vizazi vijazo ingawa yeye mwenyewe maisha yake yote alikuwa kimya.

Balozi Paul Rupia katuachia funzo.

Kaka yetu Paul Rupia ni hadithi nzuri ya kuhadithiwa, chembelecho Rais Ali Hassan Mwinyi.

PICHA:
Picha hizo hapo chini nimempiga Balozi Paul Rupia akiwa na mkewe Bi Rose Desta na kaka yangu Charles Mgone akiwa na mkewe Bi. Joyce Bakuname siku ya harusi ya mwanetu Harold.

Picha hiyo ya chini wa kwanza kulia ni shangazi yetu Bi. Flora Mgone.

1663971122055.png
1663971149567.png
 
Shekh ningependa kujua kuhusu hii shule ya st joseph covent .
Je ni hii ambayo ipo inatazama bandarini?
Tungependa kupata uzi wa shule hii na asil yake ya mwanzo ilikua ni nini
 
Ndiyo hiyo hiyo

Ila wakati tunasoma sisi vidudu hapo ilikuwa ikiitwa St Joseph,kulikuwa na primary school pia ambayo ni forodhani
Kuna sister wakat tuko tunasoma pale
Alikuwa taliano anaitwa sister Salvina

St Joseph convent ilikuwa inaitwa enzi za wakina Mohamed Said

Ova
 
Kwani huyu Rupia ndio alikuwa kamishina wa magereza? Gereza ukonga?
 
View attachment 2366116View attachment 2366117
mungu akubariki
 
uzuri wa vijiji na mitaa kutokosa wazee

Japokua kwasasa tuendako ni kinyume chake
 
Safi
Posta ya miaka hiyo, ilikua na vijana wazalendo. Miaka hii Vijana machawa
 
Back
Top Bottom