Tafakari yetu
JF-Expert Member
- Apr 19, 2021
- 1,505
- 4,427
Miongo mitatu sasa, lugha inayongumzwa na wapinzani ni kufa kwa CCM, lakini mpaka ukimuuliza yeyote akuambie kitatokea lini na wapi au kitasababishwa na nini, hakuna mwenye uhakika. Wengine wanasema ni 2025, 2030, n.k, lakini ni heri wao wanaosema pengine ni 2100, na wanaosema haiwezekani wanahoja za msingi kwa sababu mpaka sasa ni jambo la kufikirika tu.
Yeyote anayetazamia kutokea kifo cha CCM ajijibu maswali yafuatayo ufahamu wake kwa sababu hakuna kifo kisicho na sababu. Je, sababu ya kifo cha CCM iwe nini? Ni lini kifo cha CCM kiwe? Je, kifo cha CCM kiwe cha ghafla kama ajali au cha taratibu kama ugonjwa?
Sio rahisi kujibu maswali hayo kwa sababu CCM sio mgonjwa wa kutegemewa kufa kwa ugonjwa ila ni ugonjwa wenyewe, CCM sio abiria wa kutegemea kufa kwa ajali ila ni ajali yenyewe. Ingekuwa ni kweli kifo cha CCM kipo, basi tungesikia nabii nyingi makanisani, ila kwa kuwa manabii wapo kimya, ina maana kubwa. Kifo cha CCM ni fumbo la imani.