Kifo cha CHADEMA: Magufuli aliichukua Nguvu ya Umma na Sera ya Chadema na kutembea nayo

Kifo cha CHADEMA: Magufuli aliichukua Nguvu ya Umma na Sera ya Chadema na kutembea nayo

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2021
Posts
1,117
Reaction score
3,153
Jambo moja ninalolilkumbuka ni Chadema kusema kuwa Hayati Rais John Pombe Magufuli alikuwa anaongoza kwa kuiga sera za Chadema, wakati Hayati Rais John Pombe Magufuli akiendelea kutekeleza sera zao.

Chadema wakajitenga na matokeo ya utekelezaji wa sera walizoziita za Chadema, wanadamu kazi, Chadema wakaanza kupinga kila jambo alilotenda Hayati Rais John Pombe.

Sera kuu ya Chadema ikawa Magufuli ni dikteta,kazuia mikutano ya kisiasa.

Niliwauliza swali Chadema kama mnakiri kuwa Rais Magufuli anatekeleza sera zenu, kwa nini msitulie wakati akiendelea kutekeleza sera zenu?

Wakasema wao wangefanya zaidi ya anayofanya Rais John Pombe Magufuli,


Hapo ndio Ukawa mwanzo na mwisho wa Chadema

Punde tutauona mwisho mzuri wa Chadema.

Niliona jinsi wananchi walivyoielewa lugha na matendo ya Hayati Rais John Pombe Magufuli. Sera mpya ya kupinga kila kitu ya Chadema dhidi ya aliyoyafanya Hayati Rais Magufuli ilianza kuidhoofisha Chadema, na mioyo ya Watanzania ikahama taratibu kutoka Chadema kwenda kwa Rais Magufuli.

Hili lilitarajiwa, kwa sababu wananchi waliweza kuielewa lugha ya miradi na maendeleo, pamoja na jitihada za kupinga ufisadi alizozitekeleza Hayati Rais Magufuli.

Aidha, mahusiano kati ya masikini, mnyonge, na Serikali ya CCM aliyoiendesha yalikuwa ya kipekee.

Ni ukweli usiopingika kwamba binadamu hawezi kupata mbadala wa kile kilicho ndani yake, na hicho ndicho "human nature."


Kila kinachofanyika hupimwa na mfumo wa kibinadamu, unaobidi urejeshe mamlaka ya juu kabisa kwa ubinadamu.


Katika utekelezaji wake wote, Hayati Rais Magufuli alihakikisha nafasi ya wananchi ilikuwa ya kwanza.

Hayati Rais Magufuli aliwekeza kwenye mioyo ya Watanzania. Muunganiko kati ya wananchi na Rais Magufuli ulikuwa dhahiri katika mikutano yake yote, iwe aliposimama njiani kuzindua miradi au kutembelea ofisi za umma kufuatilia utendaji wa watumishi wa umma.


Wananchi hawakukosa taarifa za habari kila saa mbili usiku; kila kilichofanyika kilikuwa dhahiri kwao.

Tofauti kubwa kati ya Chadema na Hayati Rais Magufuli ni kwamba Chadema walitaka wao wawe watekelezaji wa sera hizo kwa kutumia demokrasia, huku Rais Magufuli akitekeleza sera hizo bila kujali kama ni kwa demokrasia au la.

Kwa Magufuli, zege halilali, na historia ilionyesha kuwa kila iliposubiriwa demokrasia mambo yaliharibika. Kwa namna ya pekee, wananchi walikubaliana naye.

Unaweza kurejea jinsi wananchi walivyopokea utekelezaji wa Magufuli na miradi aliyoianzisha kwa ajili yao, pamoja na mahusiano ya umilikishi na ushirikishwaji wao kihisia na kimatendo.

Tangu siku ya kwanza ya utawala wa Hayati Rais John Pombe Magufuli, tuliona nia ya dhati ya Rais kulipigania taifa lake.


Kipindi chake kilidhihirisha uzalendo wa kiwango cha juu, cha asilimia 120%. Kiongozi wa aina hiyo Chadema hawakupaswa kumpinga, kwani Magufuli alionesha kwa dhati nguvu ya umma kwa kuunganisha mioyo ya Watanzania.

Mitazamo ya wananchi ilionyesha wazi kuwa Hayati Rais Magufuli alikuwa akifanya mambo makubwa.


Wananchi waliona dhamira ya ujenzi wa Bwawa la Umeme la Rufiji (Julius Nyerere Hydropower Project) na walifahamu kuwa bei ya umeme itashuka bwawa hilo litakapokamilika.


Walishuhudia kwa vitendo Rais Magufuli akihamisha makao makuu ya serikali kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma, wakiona uwajibikaji ukirudi kwa watumishi wa umma, na mafisadi wakitumbuliwa hadharani.


Aidha, waliona miradi mikubwa ya usafiri kama reli ya umeme (SGR) ikijengwa kwa kasi, hali iliyowafanya waungane naye na kuzalisha nguvu ya umma (social power) katika miradi ya kijamii.

Hali hii ilijenga dhana ya maendeleo na fursa ya mahusiano ya kipekee kati ya mtekelezaji wa miradi, ambaye ni Rais Magufuli, na wanaopokea miradi hiyo, ambao ni Watanzania.


Kutokana na hali hiyo, nguvu ya miradi hii katika akili na mitazamo ya wananchi iliongezeka hata kama ilihusisha gharama kubwa.


Hii ilikuwa kwa sababu ya mahusiano mazuri ambayo yalikuja kuwa turufu muhimu wakati wa kampeni za mwaka 2020, na hatimaye tukashuhudia ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi huo.


Hakukuwa na uchawi wala wizi wa kura; jibu lilikuwa muunganiko wa Hayati Rais Magufuli na wananchi.

Katika hili, tunajifunza kuwa ubinadamu (humanity) una nafasi muhimu sana katika siasa.


Thamani ya miradi kwa pesa zilizotumika ilionekana na wananchi, kwa kuwa walihusishwa kwenye umilikishwaji kupitia muunganiko wa hisia kati ya Rais Magufuli na wananchi.

"A sense of ownership in the projects was in people's hands, and they saw how it can be theirs."

Wananchi waliona miradi hiyo kama mali yao, mali ya umma.
.

Viongozi wa Chadema walikiri hadharani kuwa Rais John Pombe Magufuli alikuwa akitekeleza sera za Chadema, huku Magufuli akionekana kuteka hisia za Watanzania wengi.


Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zanzibar, Salum Mwalimu, alikiri kwamba wakati wa kampeni za Chadema walieleza jinsi ya kupambana na ufisadi, kuimarisha utaratibu bora wa utendaji kazi, uadilifu, na kupunguza uzembe wa watumishi wa umma—mambo ambayo baadaye yalifanywa na Dkt. Magufuli.


Alisema kuwa Chadema ilikuwa tayari kutoa ushauri ikiwa ingeombwa, lakini baada ya muda wakaanza kumkosoa Magufuli na kujiapiza mioyoni mwao. Swali linabaki: je, walielewa kweli sera za chama chao?


Jibu linaonekana wazi sasa, ambapo Tundu Lissu anasema kuna ufisadi mkubwa ndani ya Chadema. Inaonekana ndio sababu walipingana na Hayati Rais Magufuli alipokuwa akikabiliana na mafisadi na wadhalimu. Salum Mwalimu aliwahi kusema kuwa mambo aliyokuwa akifanya Rais Magufuli yalikuwa miongoni mwa yale yaliyokuwa yakipigiwa kelele na Chadema na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).


Kabla na wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa 2015, Chadema ilikuwa imewasilisha ajenda hizo mbele ya Watanzania, ikiahidi kuzitekeleza iwapo ingepewa mamlaka.

Akihutubia mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo mwezi Januari 2017 katika Kata ya Isagehe, Wilaya ya Kahama, Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Tluway Sumaye alidai kuwa utendaji kazi wa Rais Magufuli ulitegemea sera na mikakati ya Chadema.


Hata hivyo, alisema licha ya sera hizo kuwa za Chadema, utekelezaji wa sera ya kubana fedha haukuwa miongoni mwa mambo ambayo chama hicho kilipanga kuyasimamia.


Sumaye alidai kuwa Rais Magufuli hakujiandaa kuwa Rais, hivyo sera ambazo angezitumia hazikuwa tayari, lakini alizitumia sera za Chadema kwa faida ya wananchi.

Kutokana na hali hii, wananchi walitembea na Rais Magufuli, wakiacha Chadema iliyobaki kulalamika na kupoteza mvuto.


Muasisi wa Chadema, Edwin Mtei, aliwahi kusema kuwa alifurahishwa sana na mwenendo wa Serikali ya Rais Magufuli.


Alisema Magufuli alikuwa akifanya kila jambo ambalo Chadema lilikuwa likilipigia kelele kila siku, akisisitiza kuwa Rais aendelee kuchapa kazi kwa sababu Watanzania walimpenda na kazi yake.

Hata hivyo, Mwenyekiti Freeman Mbowe aliongoza juhudi za kupinga utawala wa Hayati Rais Magufuli.


Wakati huo, Chadema ilianza kupoteza mvuto, huku lawama zikielekezwa kwao. Tundu Lissu leo anatoa ushuhuda kuwa ndani ya Chadema kuna ufisadi mkubwa, jambo linalothibitisha kwa nini walipingana na sera za kutumbua majipu alizotekeleza Magufuli.
 
Back
Top Bottom