Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imepanga Januari 15, 2025 kuanza kusikiliza ushahidi katika kesi ya kuchapisha taarifa za uongo kwa lengo la kupotosha umma, inayomkabili meya wa zamani wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob maarufu Boni Yai.
Mshtakiwa mwingine ni katika kesi hiyo ya jinai namba 11805/2024 ni Godlisten Malisa, mkazi wa Moshi mkoani Kilimanjaro.
Jacob, mkazi wa Mbezi Msakuzi na Malisa wanakabiliwa na mashtaka matatu, mawili kati ya hayo yamkabili Jacob pekee.
Kesi ilipangwa kuanza kusikilizwa leo Alhamisi, Desemba 19, 2024 lakini imeshindikana kutokana na kifo cha Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Maximillian Malewa, aliyefariki dunia Desemba 17, 2024.
Soma Pia: Kesi ya Boni Yai, Malisa yapigwa kalenda, kusikilizwa Desemba 19
Wakili wa Serikali, Asiat Mzamiru ameeleza mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Ushindi Swallo kuwa kesi imeitwa kwa ajili ya kuanza usikilizwaji na upande wa mashtaka tayari una shahidi mmoja.
"Upande wa mashtaka tuna shahidi mmoja ambaye amekuja kwa ajili ya kutoa ushahidi na yupo ndani ya Mahakama yako," ameeleza.
Hakimu Swallo amesema kwa kuwa kuna msiba wa hakimu mwezao na wanajiandaa kwenda msibani, hawataweza kuendelea na usikizwaji wa shauri hilo, hivyo kuiahirisha hadi Januari 15, 2025 itakapoanza kusikilizwa. Washtakiwa wapo nje kwa dhamana.