Kifo cha Iddi Faiz Mafungo 1987

Kifo cha Iddi Faiz Mafungo 1987

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
KIFO CHA IDDI FAIZ MAFUNGO 1987

Naamini bila ya chembe ya wasiwasi kuwa kwa sasa historia ya Iddi Faiz Mafungo inafahamika na wengi.

Iddi Faiz Mafungo Mweka Hazina wa TANU na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika aliyesimamia ukusanyaji wa fedha za safari ya kwanza ya Mwalimu Nyerere UNO mwaka wa 1955 na mmoja wa watu waliohudhuria mkutano wa kwanza wa TANU Ukumbi wa Arnautoglo Agosti 1955 alifariki tarehe 9 Januari, 1987, akiwa na umri wa miaka 75.

Mwaka 1959 alichaguliwa kuwa mweka hazina wa TANU ngazi ya taifa wakati huo huo akiwa mjumbe wa Kamati Kuu.

Ilikuwa kutokana na uadilifu wake ndiyo alichaguliwa kusimamia hazina ya TANU wakati ambapo uhuru ulipokuwa unakaribia chama kikiwa na fedha nyingi.

Idd Faiz alikufa mtu masikini na aliyekuwa na kinyongo.
Mategemeo yake kwa uhuru alioupigania hayakutimia.

Katika siku zake za mwisho baada ya kustaafu kutoka TANU Press alikuwa akitumia muda wake mwingi akisoma Qur’an Tukufu.

Alipokufa, Mzalendo gazeti la kila Jumapili la chama alichokiasisi mwenyewe na kukijenga, lilitangaza kifo chake siku mbili baada ya kuzikwa.

Makala ndogo iliyotolewa ilieleza kifo cha mfanyakazi wa zamani na mchango wake katika harakati za kudai uhuru haukugusiwa hata kidogo.

Katika mazishi yake chama hakikupeleka muakilishi kutoa rambirambi.

Kile kilichompata Abdulwahid kilimfika Iddi Faiz Mafungo; na kwa bahati wote wawili walikuwa viongozi katika Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na TANU.

Father James Lynch, muasisi wa St. Francis College alikufa Uingereza siku chache kabla ya Idd Faiz.

Kifo chake kilitangazwa katika gazeti la chama Uhuru (8 January, 1987) na gazeti la serikali, Daily News 8 January, 1987).

Magazeti hayo yakaandika kwa urefu mchango wake katika elimu wakati wa ukoloni.

Iddi Faiz, aliyeasisi TANU, akamuunga mkono Nyerere na kupigania uhuru wa Tanganyika, mauti yalimkuta katika hali ya ufukara nyumbani kwake Magomeni na si chama alichokijenga wala serikali aliyoiweka madarakani ilikuwa na habari ya kifo chake.

Huyu Father Lynch ndiye aliyemuandikia barua Mwalimu Nyerere ya kumtaka achague TANU au ualimu.

Picha: Kwanza kushoto ni Iddi Faizi Mafungo, Sheikh Mohamed Ramia, Julius Nyerere, Saadan Abdu Kandoro na Haruna Taratibu.

Picha ya pili aliyesimama kulia kwa Julius Nyerere ni Iddi Faiz Mafungo.
 

Attachments

  • IDD FAIZ MAFUNGO.JPG
    IDD FAIZ MAFUNGO.JPG
    14.3 KB · Views: 14
  • SAFARI YA JULIUS NYERERE UNO 1955.jpg
    SAFARI YA JULIUS NYERERE UNO 1955.jpg
    33.5 KB · Views: 16
Huyo mwanamke kwenye picha ya pili anaitwa nani? Kwako Mohamed Said
 
Najaribu kuvuta kumbukumbu nilikuwa wapi miaka hiyo maana sikuwa mbinguni wala duniani
 
Ni Mafungo, au Mafongo!
Gagnija,
Ni Mafungo.

Mimi nilipokea jina kama Mafungo na kwingi na kwenye kitabu ndivyo nilivyoandika.

Mwanae Faiz tukakutana baada ya miaka mingi kupita na kitabu kuchapwa akanisahihisha.
 
Hawa watu ilikuwa inatakiwa Historia zao ziandikwe kwa wino wa dhahabu.
 
Hawa watu ilikuwa inatakiwa Historia zao ziandikwe kwa wino wa dhahabu.
Maccm si yanamtukuza Nyerere tu kama vile alikuwa Mungu katoka pori kwetu huko Mamusoma kakuta watu wanaendelea na mapambano lakini kila sifa anapewa yeye... Najiulizaga sana hivi hiyo T.A.A alikuja nayo ya ukoo ama alikuta watu !!??mbona hawasikii!!?? By the way am good christian R.C lakini na hisi kuna kaubaguzi kakubwa sana kwa hawa waumini wenzetu wa imani nyingine
 
Maccm si yanamtukuza Nyerere tu kama vile alikuwa Mungu katoka pori kwetu huko Mamusoma kakuta watu wanaendelea na mapambano lakini kila sifa anapewa yeye... Najiulizaga sana hivi hiyo T.A.A alikuja nayo ya ukoo ama alikuta watu !!??mbona hawasikii!!?? By the way am good christian R.C lakini na hisi kuna kaubaguzi kakubwa sana kwa hawa waumini wenzetu wa imani nyingine

Kwani hauoni kama historia zao zinaandikwa hapa JF akili zako sijui zikoje ? Kaslimu basi uwaache wakatoliki unaosema ni wabaguzi
 
Asantee Mwalimu wangu kwa Historia nzuri Sichoki kukufatilia... Mungu atakulipa kwa kuweka ukweli hadharani... Na usichoke kutupa Historia Kama hizi ndo kuwaenz wazee wetu walotangulia mbele ya haki
 
Asantee Mwalimu wangu kwa Historia nzuri Sichoki kukufatilia... Mungu atakulipa kwa kuweka ukweli hadharani... Na usichoke kutupa Historia Kama hizi ndo kuwaenz wazee wetu walotangulia mbele ya haki
Alwayz...
Amin.
 
Back
Top Bottom