Wakuu hali mbaya ya kiuchumi inaonyemelea kampuni tanzu ya Business Times Limited. Taarifa za ndani zinasema kwamba wafanyakazi wake hawajalipwa tangu mwezi wa kwanza mpaka leo. Kisa family interference into operations. Kwa mujibu wa mfanyakazi huo chama cha wafanyakazi tayari kimetangaza mgogoro na mwajili huyo. This is the shame nakumbuka majira miaka hiyo na Business Times miaka ile. Du kweli la kuvunda halina ubani.....Correspondent wenyewe hawajalipwa kwa miezi mitano.. je tunaelekea wapi......
Kwani mzee (mmiliki) si alishafariki...at that time alikuwa ni mbunge wa kulee, labda kaondoka na mali zake.
Hata mimi sishangai kusikia Business Times ina hali mbaya. Nina muda mrefu tangu nilipojiondoa katika kampuni hiyo. Lakini nasikia sasa mambo hayaendeshwi kitaalamu. Ukishakuwa mtoto wa mwenye kampuni inatosha kupata nafasi ya kazi. Ukiacha GM ambaye baadhi tu ya wafanyakazi wanasema ana busara na msikivu, kuna mwingine ambaye wafanyakazi wenzake wanadai hawamwelewi kwa sababu haeleweki. Nasikia ingawa huyo mwingine wanayemwita Immma hana taaluma yoyote ya uandishi na wala hajawahi kuandika makala au habari yoyote, yeye sasa ni mhariri mkuu wa gazeti la Darleo. Mtu mmoja akaniambia anahudhuria pia vikao vya jukwaa la wahariri. na sijui kama wahariri wanaokutana wanaulizana taaluma zao. kama yote hayo ni ya kweli, kwanini nishangae ninaposikia BTL iko taabani wakati inaendeshwa na watu wasiojua wanachokifanya? kama ninayosikia ni ya kweli, kuna siku mhariri mkuu wa majira atakuwa mtoto wa mwenye kampuni, na kisha magazeti mengine kama spoti starehe na business times lenyewe. sasa wameanza na darleo, mengine yatafuata. sishangai kila nikisoma majira nakuta halina mhariri bali lina kaimu wake. anayekaimu nafasi hiyo ni John Mapinduzi. Yeye asubiri mhariri mkuu wa Majira atakapokuja kutoka familia ya mwenye kampuni. Nikifikiria hayo hata nikiambiwa nirudi business times nitakataa. Na tangu nilipoondoka 2006 sijajuta. Hiyo ni kazi ya familia. Kama bado kampuni itakuwepo mabadiliko yake yatakuwa hivi: Mkurugenzi wa Business Times Ltd, Baba Mbuguni. Meneja Mkuu, Mtoto Mbuguni, Mhariri Mkuu Majira, Family3 Mbuguni. Mhariri Mkuu Darleo, Family4 Mbuguni, Mhariri Spotistarehe, Family5 Mbuguni, Mhariri Mkuu Business Times, Family6 Mbuguni. Meneja Mkuukiwanda cha uchapaji, Mr1 Mbuguni, nk, nk. Vikao vyote vya utawala vitafanyika nyumbani na maamuzi kufanyika huko huko. Halafu mnashangaa kampuni isife!!!!!!!!!!!!!!!!????????????
Inasikitisha sana habari hii. Hii ilikuwa ni moja ya makampuni yenye kuletea wazawa heshima kubwa. Tuwaenzi waanzilishi kwa kuwasaidia. Nawashukuru sana mliotua taarifa hii ya kusikitisha. Mchangu wangu kama mtaalam mshauri wa biashara.
Kwanza kuna tatizo la governance au uongozi. Siyo siri kwanza watanzania wengi wetu hatuna mchakato wa kurithishana biashara na mambo wa maana kitaalam. Pili hatuna uwezo wa kujua ni kitu gani cha msingi katika mambo yetu. Tunapenda sifa kuliko kufaidi mambo ya maana. Kwani kuna tatizo gani mtoto wa Tajiri akapata chake na akawa nje ya ofisi.
Nashauri ili yasitokee mambo kama ya Kwacha Transport, Zainabs bus service, Scandinavia, Milo Construction, na wale jamaa wa ujenzi wakina LUKUWI Waliohusika sana na PPF Towers na miradi mingi ya waswahili iliyokuta wafanye mambo yafuatayo. Wenye kuwajua wana familia ya Business times wawaunganishe nami ili kwanza tuwape tiba ya kisaikologia, pili tuweoneshe faida za kampuni kuendeshwa kitaalam, tatu tuwapange ili wafanye kazi kitaalam.
Kwa bahati mumewahi kabla hawajafilisika kabisa. Washauri wenzangu tuwasiline tuwasaidie wazalendo la sivyo hakutakuwa na faida ya JF. Watafanikiwa kwa kufuata kanuni za bishara na kushirikisha wataalam tu. Mbona Mzee Mfugale na Hoteli zake anaonekana anafanya vizuri? Naamini, anafanya kazi na wataalam.