Nakubaliane nawe kuwa SK alishakuwa amekufa the moment Lulu alipotoka chumbani! Sababu ya kifo uchunguzi utaonyesha tu...iwe kusukumwa au kupigwa na kitu, kujigonga kwa bahati mbaya, cardiac arrest nk.
Kwa msiofahamu taratibu za kipolisi/kiuchunguzi....Lulu yuko kwenye matatizo makubwa kuliko mnavyofikiri. Kwanza ni lazima sababu ya yeye kuwa pale ithibitike kwamba kwa siku ya tukio Lulu alikuwa kwa SK na nia nzuri tu yaani kutoka out....hilo litathibitishwa pamoja na mambo mengine na behaviour yake (Lulu) ilikuwaje baada ya SK kuanguka kufuatia ugomvi...je ni mtu aliyekuwa nalengo la kusaidia au la? au ni kweli alipanic hakujua la kufanya kabisa? kwa kifupi kuna maswali mengi ambayo majibu yake anayo au yatatokana na maelezo ya Lulu. Lets wait (Assumption ni kuwa Polisi watafanya kazi ya ucgunguzi Professional)Mkuu Pasco heshima yako.. Pamoja na uchambuzi wako mzuri kuhusu yaliyotoke baada ya kuwa amedodondoka kuonekana kama ni uzembe wa kumpatia huduma ya haraka, lakini huku hakuwezi kuziba wala kuondoa wajibu mkuu wa Lulu kama shukiwa namba moja. Nikweli kabisa yule kijana hakutumia busara sana kuanza kumpigia simu Dr wake na kumfuata badala ya kutafuta namna nzuri ya kumuwahisha marehemu hospitali kwanza Lakini kisheria kinaangaliwa zaidi chanzo na si aftermath, hoja yako ina hoji zaidi yaliyojiri baada ya tukio Inawezekana kabisa LULU hajafanya kitendo kile kwa kukusudia, ilikuwa ni ugonvi wa kawaida tu ambao naamini watu wengi tu wanafanya na wenza wao Lakini sasa inapokuja kuwa bahati mbaya matokeo yakawa mabaya hadi kupelekea yaliyotoke basi LULU ni lazima atawajibika kwa mujibu wa sheria kuprove yaliyojiri Binafsi simlaumu LULU hata kidogo but when it comes kwenye mambo ya kisheria Lulu ni suspect no one, ni wajibu wa Lulu kuthibitisha yaliyojiri na yaendane na ripoti ya Dr. Maana ni yeye pekee walikuwa na marehemu chumbani tena katika hali ya ugonvi
Point...Walitakiwa waziamuru hospitali kutowatoa wagonjwa baada ya kupatiwa tiba kama kuna dalili ya ugongwa kusababishwa na kudhuriwa.
Sio hii mtu mahtuti kwanza ikasakwe PF3
.....na huu ni uzembe uliopitiliza ila watendaji wameufumbia macho.
Kwenye 'ajali' every minute counts...
Internal injuries, kwa kitaalamu hauruhusiwi kumsogeza mgonjwa kwa namna yoyote
kuepusha irreversible damages... Unless mgonjwa atakuwa anahudumiwa na qualified 1st Aider, au
unamsaidia under instruction toka kwa mtaalamu..
kwa nchi za wenzetu ukijipendekeza kumgeuza majeruhi waweza jikuta kizimbani...
kwa nini lulu na mdogo'ake kanumba wasingesaidiana kumpa huduma ya kwanza? Lulu hakwepeki kwenye hizo lawama, iweje atoe tu taarifa na kukimbia asitoe ushirikiano kumpatia msaada kanumba! Mimi nasema lulu hawezi kujinusuru ktk hzo lawama.
Point...
Maana kama relevance ni kutaka kumchukulia hatua za kisheria muhusika hiyo ingekuwa njia mbadala tu na ambayo haihatarishi maisha ya mdhurika....
Mtu unamaumivu upite kituo cha polisi, waanze kutafuta karatazi na kalamu ziko wapi...nani asiyejua sharau za wenzetu hawa, hawana sense of agency wao, waanze kuwarushia na maneno, mtu anaangamia tu hapo.
Mmmmmh kwa michuzi blog ...anasema marehemu hanywi wala hamung'unyi!!!na ww unasema alikuwa amelewa chakari...which is which now???RIP Steve.Kanumba alikuwa amelewa chakari! Kuna mtu wa nne alikuwa ndani ya nyumba! Ajabu hatajwi. Lulu alipigwa sana na marehemu. Tusimuhukumu Lulu Kosa la marehemu kuendekeza ulevi
Kibaya zaidi ni ili kitendo cha LULU kukimbia wakati mwenzake yuko kwenye hali mbaya kiasi kile tena usiku wa manane,
Hii inaashiria kabisa anajua lichofanya hata kama ni kwa bahati mbaya, but she knows she's the cause
Lakini mdogo wake Kanumba si alimkuta anatoa povu na kugaagaa chini? au wafu wa siku hizi wanatoaga povu na kugaagaa?
Kwa msiofahamu taratibu za kipolisi/kiuchunguzi....Lulu yuko kwenye matatizo makubwa kuliko mnavyofikiri. Kwanza ni lazima sababu ya yeye kuwa pale ithibitike kwamba kwa siku ya tukio Lulu alikuwa kwa SK na nia nzuri tu yaani kutoka out....hilo litathibitishwa pamoja na mambo mengine na behaviour yake (Lulu) ilikuwaje baada ya SK kuanguka kufuatia ugomvi...je ni mtu aliyekuwa nalengo la kusaidia au la? au ni kweli alipanic hakujua la kufanya kabisa? kwa kifupi kuna maswali mengi ambayo majibu yake anayo au yatatokana na maelezo ya Lulu. Lets wait (Assumption ni kuwa Polisi watafanya kazi ya ucgunguzi Professional)
Hii kiti inabidi utaratibu ubadiike.
Ni mara yangu kwanza kabisa kutoa hoja. ingawa hili nalo sio suala la msingi kuwa ni mara ya kwanza.Kwa ufahamu mdogo nilionao nafahamu kuwa, kama utasababisha kifo cha mtu katika hali yeyote ile,kujilinda wewe au mtu mwingine, you must be liable for that.ni kwa nini ulifanya hivyo, ndio kitakachopeleka mahakama kukupunguzia adhabu. for this issue, hakuna ubishi kama kulikuwa na ugomvi na ni wa watu wawili tu.kama alimsukuma katika kujiitetea ameua bila kukusudia, lakini mpaka idhihirike kuwa katika kujitetea alimsukuma na ndicho kilichopelekea kifo cha KN. wote walio baki wanalaumiwa kwa kushindwa kuchukua hatua baada ya tukio na sio kabla.ila sijui kama majirani walisikia na kama walisikia na hawakuja,je?ilikuwa ni kawaida yao kugombana?Mkuu Pasco,
Katika hili mie sina haja ya kutafuna maneno!! Hata kama nimehuzunishwa na kifo, bado napinga kwa nguvu zote huyu binti kuhusishwa na hiki kifo! Ikumbukwe kwamba, Kanumba kwa Lulu ni Kama Daud kwa Golliath ..!! Sina shaka yoyote kwamba, kutokana na wivu wa kimapenzi, Marehemu alianza kumshushia kisago Lulu! Bila shaka, kwa jinsi wanaume tulivyo, asilimia kubwa ya wengi wetu tungechukua uamuzi wa marehemu wa kuanza kumshushia binti kipigo!
Kwa upande mwingine, Lulu alikuwa na haki ya kujitetea! Kama nilivyosema hapo awali, Lulu kwa Kanumba ni sawa na Daud kwa Golliath! Ninachomaanisha, asingeweza kuchapana nae hivyo suluhisho pekee kwake ilikuwa ni kujinasua toka mikononi mwa marehemu! Kama chumba kisingekuwa kimefungwa (may be kilifungwa ili kichapo kitolewe sawasawa na asiwepo wa kukimbia) basi suluhisho la Lulu lingekuwa kutimua mbio! Lakini kwavile mlango ulikuwa umefungwa, Lulu alilazimika kwanza ,kumsukuma marehemu ili apate nafasi ya kutimua mbio na kufungua mlango! Jambo hili, lingefanywa na yeyote yule with exception of very few! Hata ningekuwa mimi, nisingekuwa na njia mbadala zaidi ya hiyo ya kumsukuma Kanumbe ili nipate uchochoro wa kutimua mbio! Hivyo, vyovyote iwavyo, Lulu hakuwa na namna zaidi ya hiyo ingawaje ni bahati mbaya hatua yake ya kujiokoa imezaa mauti kwa mwenzake!
Tukija kwa mdogo wake Kanumba, huyo ndie mpuuzi kuliko wote .!!! Nazani ujinga kama sio upumbavu aliofanya ni kutaka kujaribu kuifunika hii issue kwavile aliona ingekuwa skendo kwa kaka yake!! Bila shaka, wakati akichelea kuchukua hatua ya kumpeleka hospitali au kuita majirani (ili kuficha skendo) kumbe ndo alikuwa anakaribisha kifo kwa kaka yake! Na hata hiyo hatua yake ya kuanza kwanza kumuita daktari wa Kanumba ilikuwa na lengo lile lile la kuficha skendo!
WASWAHILI WANASEMA, MFICHA MARADHI KIFO UMUUMBUA hiki ndicho kilichotokea kwa Mpendwa wetu Kanumba!!
Foundation, asante kwa hoja hii. Mimi naamini katika kweli daima, na ni kweli siku zote ndio husimama. Haka kabinti katatakiwa kusema kweli. "Lulu should tell nothing but the truth" na kwa kutumia hii kanuni "Seek the truth and the truth will set you free" katakuwa huru!.Suala la kuchelewesha Kanumba kwenda hospitalini au kumpa huduma ya kwanza linajulikana kwa Kanumba tu kwa sababu tulikuwa tunamjua. Ukweli ni kwamba Watanzania tuna tatizo hili. hata zinapotokea ajali mara nyingi huwa tunawachelewesha majeruhi kwenda hospitali mwisho wake ni kilio.
Mimi sio daktari wala polisi ila siamini kama Lulu anahusika kwenye kifo cha KN,hapa najiuliza Lulu ana nguvu gani mpaka amsukumize Kanumba adondikee Kisogo, nakumbuka KN alihojiwa na mikasi siku moja na akaulizwa anacheza karate/judo akasema ameshacheza sana na akasema mtu asije kichwa kichwa. Hapa nitaamini kama KN alikuwa amelewa na aliteleza au kuna nguvu ya ziada ambayo Lulu aliipata bila kujua. Lakini mpaka sasa naamini Lulu ana bahati mbaya ambayo huwezi kuilinganisha hata iliyowahi kumpata marehemu Ditoplie. Ingawa sisemi kama Ditopile naye alifanya makusudi, najua kwamba kuna wakati sisi wanadamu tunakumbwa na hali ambayo baadaye inakufanya ujute kwa nini tulifanya vile.Hapa ndipo nasema Dunia ni pana kuliko tunavyoichukulia. Hata mim,wewe na yule yanaweza kutukuta, ndio maana nasema ni bora tuzidi kumuomba Mungu ili Yeye atuepushe na Kikombe hicho. Ni vizuri pia wakati tukimuomba Mungu tuache pia starehe za dunia kama Ulevi, uzinzi na kwenda kwenye starehe najua ni gumu lakini ndio ukweli wenyewe.
Binafsi naamini Lulu kakibeba Kikombe hicho bila kukusudia,kutegemea au kujua na hii ndio mitihani ya Dunia hii, hii husababushwa na mengi sana aidha kama ni fundisho baada ya kuonywa sana na wanadamu au Upana wa Dunia yetu.
Masikini lulu,nahisi she has a curse,namuonea huruma sana huyu mtoto,ana bahati mbaya sana
Watunga sheria hawajali maana wao huwa wanatibiwa wakisema tu "Mimi mbunge" hawaoni umuhimu wa kusawazisha sheria
Sijui mantiki gani inayotusukuma watanzani kutaka PF3 kwanza kabla ya tiba....
Sisi si wazima kichwani