Kifo cha Karume na muungano wetu

Kifo cha Karume na muungano wetu

Ramark

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2015
Posts
1,989
Reaction score
1,447
Ndugu zangu

Leo nikiwa natafakari kwa kina juu ya kumbukizi ya miaka 48 ya kifo cha mwanamapinduzi jabali wa siasa za kisiwa na Rais wa kwanza wa Zanzibar, nikapitia pia nyaraka mbali kabla na baada ya kifo chake.

Nikiamini kuwa, wapo wanajf mbalmbali wamewahi kuzungumzia kifo hiki katika mazingira hayo na Yale.

Wazanzibar walianza kuuchukia muungano baada ya kifo cha Karume, kuunganishwa kwa ASP na TANU kutokana na harakati zilizoendelea ndani ya ccm na hata Mbele ya umma dhidi Muungano.

Hata ilipoundwa katiba ya JMT ilionekana kuwa na mapungu iliyopeleka mabadiliko ya mapema pia ikasababisha wazanzibar pia kuona haja ya kuwa na katiba 1984.

Suala la serikali tatu lilitoka kwenye vinywa vya wanazanzibar na hata leo inaaminika ni hoja yao.

Utengano wa unguja na Pemba pia ulizaliwa na CCM ukiachilia historia ya Zanzibar kwani tayari walikuwa wameshazika baadhi ya tofauti.

Tunajua inawezekana ni ubabe wa Karume kwa watu weupe na wenye nasaba na weupe kama mbinu ya kuimarisha mapinduzi kulingana na falsafaa ya mwalimu ya Azimio la Arusha, ni sehemu ya kusambaza chuki lkn isingeweza kufika huko.

Tanganyika pia kulikuwa na hali ya kuroridhishwa na hali wakijaribu mapinduzi kadhaa yaliyoshindwa.

Ni maelezo mafupi yanayolenga tupate swali fikirishi.

Lengo la kifo cha Karume ni kweli ni kisasi cha Mahmoud au ni Urais?

Lengo la kifo cha karume ni urais au simanzi ya wazanzibar kupitia jeshi?

Lengo la kifo cha Karume ni kuimarisha muungano? Kama Karume angeishi Muungano wetu husingeishi mpaka leo?

Tunaweza kuwa katika sintofahamu lakini tukawa watu wenye fikra mpya.

Nimefikiri hivi kutokana na ukweli kuwa kero za Muungano asili yake si Tanganyika, hivyo inawezekana muungano huu hauna mizizi isipokuwa unaishi kama Maua rose yanayoishi baada ya kukatwa.

Fikra mpya zinaweza saidia kuimarisha muungano, kwani uimarishaji unaanza na kuhisi ukweli.

Fikra mpya hata kama ziliwahi kuishi leo zitaitwa mpya na kuendelea.
 
Nikafir, kama muuaji na mauaji hayakupangwa kama zinavyosema nyaraka mbalimbali kwa nini ulinzi ulikuwa butu?

Muuaji alianza kumimina risasi toka nje aliposhuka kwenye gari mpaka anaingia ndani hadi anamimina risasi nane shingoni na kifuani kwa karume.

Kiswandui siku hiyo hali ya usalama ilidhohofu kama ilivyokuwa dhohofu kwenye kamati kuu yaCCM pale lumumba kupelekea Mangula kulazwa na badaye kuthibitishwa kupewa sumu. Ndani ya Majengo ya vyama hali ya kutokuwa makini kama hiyo,

Hatuwezi kuamini hizi ni incidents zilizopangwa?
 
Rais hawezi kufa bahati mbaya hasa rais aliyepo madarakani labda kama ameugua muda mrefu otherwise kuna namna na always zinabaki siri za vyombo vya ulinzi na usalama.
 
Lakini hali hii ilionekana dhahiri miaka 1980-84
Wanaochukia muungano siyo wazanzibari ni chokochoko za chadema tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Miaka hiyo watu wengi walifukuzwa ccm na ikazaliwa uunguja na upemba wa hadharani.
Lkn pia chadema haikuwepo.

Wapo waliodai CUF ndiyo chanzo cha chokochoko kutokana na kuwa na watu waliofukuzwa ccm(maalim seif na wenzie) mwaka 2000 hali ilizidi hasa baada ya mauaji yale, ambapo rais na wajeshi WA Tanganyika wakalaumiwa na kuchukia.

Labda Mkuu, utisaidie je, ni kwa nini watanganyika hawauchukii Muungano?
 
Back
Top Bottom