KESI HII NI MOJA YA KESI AMBAZO TULIOWENGI TUANGALIA MATOKEO ATUANGALI CHANZO.
Issue ya mkufunzi huyu wa makomando, ni moja ya kesi ambazo watu makini hawaipokei kwa kuangalia tu matokeo..kesi hii inaangaliwa kwa jicho pana sana tena pana isivyo zaniwa.
Kwa mwenye ufahamu yoyote yule kuhusu UKOMANDO anajua kuwa Mwanajeshi yoyote yule mwenye ujuzi wa ngazi ya UKOMAMDOO ni daraja kuwa mwanajeshi huyo kwa kumilki ujuzi huo tu tayari bila kuwa na silaha mkononi yeye kama yeye ni silaha hatari kuliko hata angekuwa na KISU, BOMU, AU AK 43 au silaha yoyote ile mkononi.
Kwa ,mwenye kufahamu tu kuwa Mkufunzi wa makomandoo yuko mtaani basi yeye kama yeye ni silaha hatari yenye thamani kubwa ya uzito wa makomandoo kadha wa kadha mkononi.
Zamani ilikuwa ni nadra sana hata kumjua komandoo, labda awe ndugu yako, lakini toka ujio wa mfumo wa kuacha wanajeshi kuishi mitaani kwenye nyumba za kupanga, na kunywa kwenye bar za mtaani kama mkufunzi huyo tayari hitilafu imeshaonekana.
Mkufunzi huyu gharama ya uhai wake ni kubwa sana, kwa kuwa mpaka alipofika hapo thamani yake na ujuzi wake ni mkubwa sana kuliko sie raia [civilian] tunavyomuona.
Kwa wanaojua mifumo ya kijeshi dunia [Komandoo huyu] ni special unit,hivyo hata kwa kuangalia tu hizi sinema tunazoziangalia sie watanzania na kuzipenda chini ya majina ya sinema za kijeshi za marekani za ACTION tunaona MADHALA MAKUBWA ambayo uwa yanaletwa na watu wa SPECIAL UNIT aina ya Mkufunzi huyu wa UNIT zetu Tanzania, kama haya ambavyo Mkufunzi huyu kasababisha.
Sio kuwa si thamini maisha ya raia huyu yaliopotea, la hasha lakini matokeo ya tendo lile kwangu ni WAKE UP CALL kwa watu makini ndani ya mfumo KUTAFAKARI KWA MAPANA madhara ya kuweka majeshi yetu mitaani, na kuchangamana na raia katika sehemu za starehe, wakati wao wanapaswa kuishi kwenye kambi maalumu za kijeshi na MESS zao maalumu za kutumia.Tena huyu Mkufunzi hata tu kwa kuwa ni mtu wa specila unit bado astahiki kuishi kambi moja na wanajeshi wa kawaida anapaswa kuishi ndani ya kambi maalumu ya ujuzi wake wa kijeshi.
EBU TUTIZAME KOSA KAMA HILI:MFANO WA MOVIE YA THE UNITY.
Kwangu mimi matokeo ya tukio la Mufunzi huyu wa SPECIAL UNIT ni swala ambalo ,wenye ufahamu waende mbali kuangalia kama TAIFA kuna mambo hayako sawa katika kuhudumia MAJESHI yetu kwa kuyafanya maisha ya wanajeshi wetu kama ni maisha yanayopaswa kuwa sawa na raia mitaani [Civilian].
Kama baadhi yetu waliopata kuangalia series moja ya kimarekani yenye speacial unit moja THE UNIT, kuna wakati bosi wa UNIT alipomuona mmoja wa vijana wa special Unit ile anamatatizo na mkewe akatumia mwanya ule kumpa Mke wa Afande wake yule pumziko.Lakini mchezo ule jamaa mwenye mke aligundua issue ile wakati fulani wakati unit ile ilikuwa kwenye misuko suko ivo familia za wanajeshi wa UNIT ile wakawa ukimbizini kwa kutafutiwa makazi ya kufichwa.Laula katika box moja la familia la afisa anaetumiwa mke wake na mkuu wa UNIT ikakutwa picha ya Mkuu na mkewe wa Afisa.
Afisa mwenye mke kwa taaluki alichotaka kufanya ilikuwa ni kumtafuta mkuu wake na kumaliza tena kwa kutumia special silaha ya UNIT aliyopewa.Mungu mkubwa mwenzie kwenye UNIT akagundua mabadiliko ya Afisa mwenzie na kuamua kuhakikisha hafanyi jambo baya mpaka pale atakapoona jambo lile linafika kwa timu ya maafisa wenzie na watafute jibu la HUKUMU dhidi ya BOSI WAO.
Issue ile ilipofika kwa kikosi maalulumu [THE UNIT] walikaa na kutafuta hukumu ya kosa la mkuu wao dhidi yao ya kuwasaliti kwa kumtafuna mke wa askari wake anae muongoza.Wote askari wa UNIT kwa umoja wao walipiga kura ya KIFO kwa mkuu wa wao.Na makubaliano hayo yalikwenda kwa KIAPO.Kwa kila mmoja wa askari wale kulusha kisu chake cha kazi kwenye duara waliyokuwa wamechora kama eneo lao la kiapo cha utiifu.
Hivyo TSK FORCE ile ilitafuta njia ya kutekeleza kifo cha AFANDE wao MKUU wa UNIT, yani mfano mzuri ingekuwa ni afande wetu huyu kama mkuu wa specila force alivyo aukumumiwe kifo na wanafunzi wake.Mkakati ulipangwa kuwa auwawe kwenye mission.Mkuu wao yule alikuja gundua piwa kijana wake kesha jua, kilichomuokoa na kifo ambacho nae alijua kuwa uenda wkati wowote atakuwa marehemu kwa syndicate ya vijana wake kwa kosa ambalo alishaafiki kupokea hukumu hiyo lakini hakujua lini utekelezaji wake utafanyika.
Kilichomwokoa ni tendo jema la yeye kuyatoa maisha yake kumuokoa binti ya afande wake anaengoza unit kwenye field.Ilipofika wakati wa hukumu itekelezwe TASK UNIT ilimuachia mwenye mke kutekeleza hukumu hiyo ya kifo.Mkuu alipigwa kifo cha paka mwizi isingekuwa ni mtu wa kikosi kazi [chukulia angekuwa raia kama marehem wetu wa uraiani] basi angekuwa marehemu zamani sana.Alipata msamaha kwa kupima jinsi alivyojitolea kumuokoa binti ya mwanatask force wake.
KILICHOTOKEA.
Ikiwa tu mtu kamshika mtu ugoni mtaani uwa inakuwa heka heka, sembuse afande huyu ambae yeye binafsi alivyo tayari ni silaha, aaahaa si swala la kuchezea.
Yaliopita hapo ni mengi sana kuna maswala ya fani ya muuaji, saikolojia ya tukio, mazingira ya tukio kuwa ni kwenye ulevi, na aina ya kosa la muhusika, WASWAHILI WANASEMA MKE WA MTU MZIGO WA MAVI, UKIUBEBA UTAKUNUKIA TU.
Kamanda aludishwe kwenye majukumu yake ya kutengeneza askari maalumu, tujisahihishe na ria tujifunze kuheshimu raia mwingine..WAHENGA WALISHASEMA USIMDHARAU USIE MJUA, MAREHEMU ALIMDHARAHU MKE WA KAMANDA na kumshika sika ovyo bila hiari yake huo ni utovu wa nidhamu. na ni kosa la jinai.
Mtenda kosa ni mtu ambae sheria zinanazoendesha maisha yake ya kila siku ni sheria tofauti na za marehemu ivo kesi hii si bora kuwalizisha raia lakini itumike kuwafungua raia kutambua kuwa WANAJESHI wana SHERIA ZAO zinazoendesha maisha yao ya kila siku.
Na ndio maana hata ASKALI wa majeshi yetu wanapostaafu na kuamia uraiani bado uwa ni SONGOMBINGO basi MUNGU saidia kwa kuwa ni kaka zetu, shangazi zetu, baba etu, wajoba zetu, uishi kuvumiliana laikini wote uishi KUTAMBUA MIJI YA WANAJESHI wetu kitaani....tena uwa tuna majina kwa kuita KWA MWANAJESHI.
Taifa litoe ASKARI MTAANI, na RAIA wapewa ELIMU YA URAIA.