Pumzika kwa amani mama.
Saratani ya matiti inaua sana, ninawafikiria kina mama mamilioni ambao hawana uwezo wa kufika hospitali ya wilaya, achilia mbali Ocean Road.
Moja ya mikakati inayowafanya wenzetu waweze kufanikiwa katika vita dhidi ya gonjwa hili (na mengine mengi ya aina hii) ni kutazamwa mapema kama wana uvimbe na dalili nyingine, kansa hii inaweza kuzuilika kabisa kama ikigundulika mapema.
Naomba tufikirie kidogo kuhusu uwezekano wa kuongeza huduma za kupima mapema na kuliwahi gonjwa hili katika hatua ambazo linaweza kuzuiwa kuchukua maisha ya kina bibi, mama, dada na binti zetu.