Maramla
JF-Expert Member
- Jan 8, 2014
- 588
- 648
Kifo cha Mlevi wa Misenyi na Aibu Kwa “Mashine ya Propaganda” ya Chadema
Wachambuzi wengi wa mambo wameonya mara kadhaa kuwa masuala mengi hapa nchini yanayodaiwa kuwa na changamoto ama yanakuzwa au ni sehemu ya uzushi wa “mashine ya propaganda” ya vyama vya upinzani hasa Chadema.
Leo utata huo umewekwa bayana rasmi kufuatia kifo cha Joseph Remigius mkazi wa Misenyi, anayedaiwa kuwa kada wa Chadema ambaye awali alidaiwa kuuawa akiwa ameshachukua fomu za kugombea uchaguzi wa mitaa na eti alikuwa akisubiri kampeni za uchaguzi ndio akauawa katika mazingira tata.
Mficha maradhi kifo humuumbua! Uchunguzi wa Polisi lakini na ushuhuda wa wanakijiji wenzake umethibitisha kuwa anayedaiwa kuuawa kumbe ni mlevi maarufu tena aliyepata umauti huo kwa ajali ya bodaboda!!
“Huko Ufipa walioanza kufyatua mifumo yao ya uongo na uzandiki wametamani ardhi ipasuke wajifiche kwa aibu hii. Mfumo wa sasa wa Serikali na hasa Jeshi la Polisi kutolea ufafanuzi haraka matukio tata umewauma na wamefura,” anasema mwanaChadema mmoja.
Daaa!! haya wachambuzi wa mambo wanatumia suala hili kufanya uchambuzi unaoonesha kuwa kuna mfumo maalum wa propaganda ndani ya Chadema wenye muongozo (script) maalum waliyofundishwa na mawakala wao mabeberu. Iko hivi:
Kwanza, wana watu maalum mitandaoni ambao wanalipwa na mabeberu kusambaza uongo, uzushi na zaidi upotoshaji.
“Wamejipanga na usione wale watu wanaosambaza uongo mitandaoni ukadhani ni wazalendo au wana mageuzi ni mkakati na wanalipwa,” kilisema chanzo kimoja.
Pili, mkakati wao ni kila jambo baya wameelekezwa kuihusisha Serikali ili kuichafua. “Ukifanya uchambuzi, utaona leo hii hata mlevi akikamatwa kwa kosa la usalama barabarani, wao watasema ni kada wao ameonewa. Utaona hata kifo kinachotokana hata na kudra za Mwenyezi Mungu au uhalifu wa kawaida, akiwa anauhusiano tu na Chadema, wataeneza kuwa ni Serikali. Hujiulizi? Haitokei kwa kawaida. Ni mkakati,” kilisema chanzo kingine.
Ni vyema Serikali ikazidi kuwa macho na mikakati hii michafu. Maana kwa staili na mwenendo huu ni wazi kuwa Chadema wako tayari hata kuua ilimradi wapate mtaji wa kisiasa wa kuichafua Serikali.