Kifo cha Nkaissery: Matiang'i ateuliwa kaimu waziri wa usalama Kenya

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532


Waziri wa elimu nchini Kenya Dkt Fred Matiang'i ameteuliwa kuwa kaimu waziri wa usalama wa ndani kufuatia kifo cha aliyekuwa waziri Meja Jenerali Mstaafu Joseph Nkaissery.

Waziri huyo wa usalama alifariki dunia muda mfupi baada ya kulazwa katika hospitali ya kibinafsi ya Karen jijini Nairobi kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.

Uteuzi wa Dkt Matiang'i umetangazwa na Rais Uhuru Kenyatta baada ya kuongoza mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama wa Taifa.

Rais Kenyatta amesema hakutakuwa na pengo lolote kiusalama nchini kutokana na kifo cha jenerali huyo mstaafu. Rais amesema maandalizi ya uchaguzi mkuu ambao utafanyika tarehe 8 Agosti, mwezi mmoja kuanzia sasa, yataendelea bila kuvurugika.

Bw Kenyatta amewataka Wakenya kuendelea kudumisha utulivu.


Chanzo: bbc swahili
 
Kawa je tena waziri wa usalama? Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.
 
Huku kwetu nafasi ingeachwa wazi hata miezi 8.


Hivi mrithi wa Prof.Muhongo ni yule mbunge Msukuma?
 
Huku kwetu nafasi ingeachwa wazi hata miezi 8.


Hivi mrithi wa Prof.Muhongo ni yule mbunge Msukuma?
Huwezi acha nafasi nyeti ya Waziri wa Ulinzi wazi wakati nchi ina uchaguzi mkuu mwezi ujao
 
Huku kwetu nafasi ingeachwa wazi hata miezi 8.


Hivi mrithi wa Prof.Muhongo ni yule mbunge Msukuma?

Kama ameuwawa strategically, unaiachaje nafasi wazi kwa mfano!! Uwe unatumia hata akili za jirani wakati mwingine!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…