Kifo cha raia wa Congo chazua taharuki Brazil

Kifo cha raia wa Congo chazua taharuki Brazil

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Polisi nchini Brazil wamewakamata wanaume watatu kuhusiana na mauaji ya kikatili ya mhamiaji wa Congo mjini Rio de Janeiro.

Mauaji hayo yaliyonaswa kwenye video yamesababisha ghadhabu ya umma.

Jamaa wanasema Moise Kabagambe alishambuliwa baada ya kumtaka bosi wake alipe mshahara anaodaiwa kwa kazi ya siku mbili kwenye kibanda cha ufukweni.

Kanda hiyo ilionyesha akipigwa mara kwa mara na wanaume watatu wenye vilabu na gongo la besiboli.

Meya ya Rio, Eduardo Paes, ametaja mauaji hayo "isiyokubali na ya kuasi".

Mama yake alisema famili yake ilifanikiwa kutoroka ghaisa na machafuko kwao nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo - lakini mwanawe ameishia kutendewa matukio sawa na hayo huko Brazil.
 
Brazili sio nchi ya kwenda, wanatafuta nini huko, wao wenyewe wabrazili njaa inawasumbua......kwanza kabisa huwa wanakaubaguzi/ubinafsi na kujitenga, refer timu ya taifa na club kwa ujumla utajionea
 
Brazil kwenye matabaka ya kibaguzi yaliyoshindikana!
Mcongoman rest in peace, kafa kifo Kibaya sana! Shame
 
Kwa hiyo basi ni madhila yanayoweza kumtokea mtu popote pale, iwe nyumbani, ugenini, ng’ambo, n.k.

Upo sahihi...

Lakini kwa kiasi kikubwa huwatokea Waafrika wawapo ughaibuni, na sio kupigwa au kuuawa tu, bali hata ubaguzi wa rangi...

Ni nadra kwa mgeni toka ng'ambo kufikwa na matatizo kama hayo awapo Afrika...
 
Malipo ni hapa hapa duniani, wamemuuwa mwarabu wa watu huko huko congo, sasa na raia wao ameuawa kwa wabaguzi nchini brazili. Malipo ni hapa hapa duniani
 
Back
Top Bottom