Kifo cha Rais Magufuli: Wanyonge na Walalahoi wanajua walichopoteza

Kifo cha Rais Magufuli: Wanyonge na Walalahoi wanajua walichopoteza

Leslie Mbena

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2019
Posts
207
Reaction score
677
KIFO CHA RAIS MAGUFULI:WANYONGE NA WALALAHOI WANAJUA WALICHOPOTEZA.

Leo 12:20hrs 21/03/2021

Uwanja wa Uhuru umejaa pomoni Wananchi wakija kwa shughuli moja tu kuaga Mwili wa Rais wa tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Hayati John Pombe Magufuli, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mh Godwin Gondwe anawashukuru wananchi kwa kuja Uwanjani na kwa upendo mkubwa wanaouonyesha kwa Baba yetu kipenzi Rais John Pombe Magufuli, geti linafungwa ili watu wa ndani ya uwanja wamalize kuaga ndipo geti la Uwanja wa Uhuru lifunguliwe tena ili wananchi waingie tena kumuaga kipenzi chao Rais wa tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Nimemuona Mzee Mzindakaya akilia hadharani,Mamilioni ya watanzania wameangua kilio kila kona ya Tanzania kwamba sasa mwokozi wao ameondoka,watu wanaendelea kudondoka na kuzimia mbele ya Jeneza, nipo Uwanjani kila ninaekaa nae analia nami kwa hakika nimelia hadharani,Wananchi wa hali ya chini kabisa ndiyo wanaoongoza kwa kilio kinyume na tulivyokuwa tumeaminishwa na Tundu Lissu, Kigogo, Mariam Sarungi kwamba Magufuli alikuwa ananyonga wanyonge!

Kitendo cha hayati Rais Magufuli kuagwa na mamilioni ya watanzania huku wakiangua vilio njia nzima na kutandika kanga barabarani,kutandika mitandio yao chini ili mwili wa Rais wa tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania upite juu ya kanga,vitenge na mitandio hiyo,hii ni heshima kubwa toka kwa Mama zetu, heshima hii imeenda kinyume kabisa na wasaliti wa nchi hii akina Tundu Lisu na genge lake.

Tunapoona vilio hivi vya Watanzania kila kona,Mungu anazungumza jambo kupitia uwingi wa vilio hivi vya Watanzania na wengi vikitokea kwa Wanyonge na Walalahoi, Mungu amemchukua mpendwa wetu Rais Magufuli ili watu waone ukweli na uwongo,watu waone utofauti,watu wajue lawama zao zilikuwa sahihi au si sahihi, watu wamemtuhumu kwa mengi,Mungu anataka watu wajue tuhuma hizo ni kweli juu yake au kuna watu walikuwa wanatumia kivuli chake, kuna somo tunakwenda kujifunza,

Mwenyezi Mungu anayosababu kwa maana ndiye mwenye kujua tunapoelekea na je amwache mpendwa wake aendelee kutukanwa na watu wasio na fadhila au amchukue ampeleke paradiso akapumzike pamoja nae katika Ulimwengu mwingine ambapo atakutana na Rais wa kumi na moja wa Ghana,Prof John Atta Mills,Nabii Eliya,Nabii Musa pamoja na Nabii Enoch,Sasa wanaotaka turudi kwenye shamba la bibi, watafakari kwa makini, na wajue yasije yakawa sababu ya Jina la Chuma, Rais Magufuli kutajwa kila pahala kuwa yeye alikuwa mwamvuli wa watu wa chini na kujikuta jina lake likitawala fikra zao na hata kutajwa sana kwa mema yake kwenye midomo ya watu wanyonge!

Umuhimu wa mtu huthibitika baada ya kufa,Waliokuwa wanashinda mitandaoni wakitukana,kumkejeli na kudhihaki uongozi wake sasa wataanza kumkumbuka kinafiki,Uongozi ni kuwawezesha watu kwa kuwawekea miundombinu ili iwasaidie katika shughuli zao,na Magufuli alifanikiwa kwenye hilo.

Nguvu ya matajiri itakapoielemea serikali hii mpya,wanyonge watalitaja Jina la Magufuli kwa uchungu mkubwa na hakuna atakayewazuia

Pale rushwa itakapowafanya wanyonge,wamachinga, wamama ntilie, bodaboda, bajaji n.k ambao idadi yao ni kubwa mno kwa sasa katika nchi hii kuanza kufukuzwa kwenye maeneo yao ya kazi aliyokuwa amewaruhusu Jembe Lao JPM R.I.P kufanyia biashara zao,

Ndipo sauti zao na Kwa uchungu mkubwa zitasikika, wakimlilia Kwa upya tena John Pombe Magufuli na jina lake litatawala kwa upya kwenye vyombo mbalimbali za habari kote Tanzania na hata duniani,

Pale majambazi ya kupora muda wowote asubuhi mchana na wakati wowote yatakapojitokeza,iwapo Serikali hii haitasimama kiume,sauti za wananchi wengi watakapoanza kumlilia JPM kwa upya, na watu watasema ni bora alipokuwepo Chuma haya yalikoma,

Pale matajiri wakubwa watakapoizidi serikali ujanja aidha kwa rushwa Ili wasilipe kodi, na kodi nyingi kuelekezwa kwa wafanya biashara wadogo wadogo,watu hawa wataanza kumlilia upya Jembe lao,watasema, ni kwa sababu hayupo Rais Magufuli ndio maana tunanyanyaswa?

-Je Rais Magufuli alifanya Makosa?

Ndio,mengi sababu Rais Magufuli sio malaika,Rais Magufuli alikuwa binadamu mwenye mwili wa nyama sawa sawa na kila binadamu yeyote yule,hakuna ukamilifu kwenye ubinadamu hadi utakapokufa na mwili kurudi kwenye udongo na roho yako kwenda kwa Mwenyezi Mungu,dakika za mwisho za uhai wako ukitubu na kureconcile na Mungu wako basi anakusamehe na kuipokea roho yako katika ufalme wake,hata Bwana Yesu atakapomaliza kuujenga Mji Mpya wa Jerusalem na kutuita wote tuliohesabiwa haki tuingie uko na kuishi milele bila kifo,Rais Magufuli hadi dakika ya mwisho alikuwa mwenye nguvu hata kuimbisha nyingo familia yake na kupiga maombi na kuwaaga na kuitwa kwake na Mwenyezi Mungu, pamoja na sala kutoka kwa Kardinali Pengo na Mufti Mkuu,Je Mwenyezi Mungu hatamsamehe!? Sasa unayeendelea kumhukumu,imeandikwa ni Mungu pekee ndiye mwenye kuhukumu.

Rais John Magufuli alisimama kwa ajili ya Mwananchi Mnyonge na Mlalahoi na aliitwa Rais wa Wanyonge na masikini,hii ni bond kubwa sana ya Rais Magufuli na Wananchi,Tabaka la watu wanyonge wasio na chochote cha kujisifu nacho mbele za watu ambalo awamu zote limejichokeaga tu sema safari hii katika awamu hii ya tano wenye pesa wanaosemaga unanijua mimi, waliogopa kuwanyanyasa kwa sababu Rais Magufuli angelala nao mbele,tabaka la chini lilimpa kura asilimia 100% Rais John Pombe Magufuli ili aweze kumalizia miaka yake mitano ya mwisho katika awamu yake ya pili kwa sababu alikuwa na muungano na tabaka hilo(bond),na kwa tabaka la kati lenye uwezo wa kula milo mitatu kwa siku, Matajiri, wasomi walimpa kura Rais John Magufuli kwa asilimia 90% Mungu amemuepusha na jambo,akamchukua mpendwa wake, Mungu ndiye aliyetuumba na ndiye anayetupenda kwa dhati na kweli.

Wakati wa Corona,Rais Magufuli hakuweka lockdown kwa sababu aliwafikiria zaidi wananchi wake Wanyonge na masikini,hakutaka Wananchi wateseke,maana kila mwananchi mnyonge wa tabaka la chini anategemea kipato anachopata kila siku aendayo kazini,Rais Magufuli alisimama akiitetea Tanzania na Afrika kwa ujumla, alitaka Afrika irudi kwenye sauti yake na nguvu zake kama wakati wa Mandingos,Ufalme wa kwanza duniani uliopatikana Afrika nchini Mali, Wakati wa utawala huo wa kifalme wa kabila la Mandingos ulipokuwa unavuma ndipo walipoweza kujenga chuo kikuu cha kwanza duniani, ambacho kilifanya tafiti mbalimbali za kisayansi na kufundisha vijana wengi waliotoka nchini Mali na nchi za jirani. Wakati huo nchi za ulaya bado hazijaamka zipo nyuma sana, tukumbuke maendeleo ya wazungu yameanzia Ugiriki na Hispania ambayo yameanza kwenye millennium ya pili wakati hii tuliyokuwa nayo sasa ni ya tatu; vyuo vikuu vya ulaya vya mwanzo vilianza kujengwa karne ya 16 wakati huo utawala wa kifalme wa Mandingos umeshavuma karne nyingi zilizopita na umeshaanza kusambaratika na Wazungu walifanya hivyo kwa kuingiza Utamaduni wao wa kustaarabika kulikofanya sisi Waafrika kujichukia hatimaye wazungu wakatutawala.

Rais Magufuli ametumia Mali asili zilizopo Tanzania na ameiingiza Tanzania kwenye nchi ya kipato cha kati,ukichukua miradi yote aliyoitekeleza,miundo mbinu yote aliyojenga,pato la Taifa na kodi aliyokusanya ukijumlisha hivyo na kugawa kwa population ya Watanzania Milioni sitini unapata kipato cha mtu mmoja mmoja ambacho kimetuingiza kwenye uchumi wa kati,ni lazima wazungu wamchukie kwa mafanikio hayo,na lazima mafisadi yamchukie kwa alibana mianya yao ya wizi na kutumia fedha hizo kujenga miundo mbinu,Rais Magufuli alikuwa Mwanaume kweli kweli,Chuma,

Rais Magufuli aliamini katika bara la Afrika ndio maana amefariki akiwa hapa hapa Tanzania, Magufuli alionyesha utawala shirikishi na mwananchi,kila mwananchi aliguswa kwa kizungu utawala huo unaitwa (People driven-driven leadership that continues to inspire the Mwananchi,Rais Magufuli demonstrated a selfless but people- driven leadership,He had progressive vision,He had principle-centred vision,Rais Magufuli aliamua kuwa Msemaji wa kweli wa Afrika.Rais John Pombe Magufuli aliipenda Tanzania kwa dhati ya moyo wake na furaha kubwa moyoni mwake kwa bara la Afrika,Rais Magufuli alifurahia kuwa Mwafrika na kuwa tayari kufa kwa ajili ya Tanzania na Afrika.

Nawausia Watanzania wote tuwe kama Magufuli,Vyombo vya habari vya Ulaya nadhani vimeona upendo mkubwa wa Watanzania kwa Rais wao John Pombe Magufuli,Good Night President Magufuli,you were not only a President but God marked you as a President with a difference,Mwenyezi Mungu amekutofautisha na Marais wote,Neno la Mungu linasema yupo anayeishi maisha mafupi na moyo wake ukatosheka kwa kutosheleza mamilioni ya Wananchi na watu wa Mungu,lakini yupo anayeishi maisha marefu hasitosheke yeye na mamilioni ya Walimwengu kwa kuwa hawapo kwenye njia ya Mwenyezi Mungu.

Shujaa wetu amelala ila naamini mawazo yake, imani yake, na maono yake ndo yanachipuka kwa kasi hivo ni imani yangu Rais Magufuli bado anaishi mioyoni mwetu tulio wengi.Na ataendelea kuishi miaka mingine zaidi ya 50 kwa sababu kazi zake tukufu zinatangaza moyo wake wa kizalendo na wa kujitolea hata kufa kwa ajili ya taifa letu la Tanzania,Usiku mwema Rais wa tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Rais John Pombe Magufuli, Mungu ibariki Tanzania,

Mungu mbariki Rais wa sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Rais Samia Hassan na umpe maono kama ulivyofanya kwa Rais John Magufuli.Mioyo yetu imesononeka sana kiasi cha kuvuja damu kwa kuondokewa na mwanamapinduzi John Pombe Magufuli,Mungu amemuita kwa wingu dogo kushuka na kumchukua, kiroho hiyo ni mapokezi mema ya kukaribishwa Mbinguni,a warm welcome to heaven.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
075507885

-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Wanyonge tutakukumbuka sana raisi JPM lakini pia Mama samia hatotuacha solemba

Mjumbe hauwawi Mjumbe hauwawi
Tundu hatokaa awe raisi Tz daima na milele naombeni mjue hilo Kama nakosa nisameeni Sina lengo la kuwaumiza bali kuwataarifa,
 
Hiyo namba yako ya simu bora ukaitoa tu! Haina kazi tena usawa huu!! By the way, mimi kama mtumishi wa umma nakuhakikishia sina nilicho poteza baada ya kifo cha Mh. Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli.

Kama binadamu mwenzake, namtakia tu pumziko la milele.
 
1:Wewe na ukoo wako wote ndiyo WANYONGE.

2:Wewe na ukoo wako woote ndiyo WALALA HOOOIII.

Naona utafurahi kuwa kwenye hayo makundi maana umeyapenda sana.

Huwezi kuniita mnyonge na mlala hoi wakati hujui nakula nini wala navaa nini.
 
Karibuni China wamejipongeza kwa kuondoa umaskini(poverty)kabisa.
Wewe bado unapenda kuiba mamilioni bado wapo!
RIP JPM
 
Ni kweli ukiangalia watu wanavyo ruka mageti, huwezi kuamini kuwa kuna jamaa fulani anadhihaki juhudi zake, Ina maana hawa maelf na mamilioni wanaolia na kuzimia wote wameshikiwa akili?
 
Wanyonge tutakukumbuka sana raisi JPM lakini pia Mama samia hatotuacha solemba

Mjumbe hauwawi Mjumbe hauwawi
Tundu hatokaa awe raisi Tz daima na milele naombeni mjue hilo Kama nakosa nisameeni Sina lengo la kuwaumiza bali kuwataarifa,
Ila Tundu Lissu anachekesha sana,nasikia anasema yeye ndio Rais wa 7 wa Jamhuri,Mwana kulitafuta.
 
Msimshambulie sana jamani,watu wanatafuta kazi hapo,hamuoni Cv hapo na namba ya simu?
 
Hivi mtu mzima kama wewe ambaye probably una watoto wanakuita "baba" hujishtukii na kuona aibu kujiita "MNYONGE"???

Bruh, you only live once!
 
Ni kweli ukiangalia watu wanavyo ruka mageti, huwezi kuamini kuwa kuna jamaa fulani anadhihaki juhudi zake, Ina maana hawa maelf na mamilioni wanaolia na kuzimia wote wameshikiwa akili?

Hiyo kuzimia ni acting tu.
 
Back
Top Bottom