Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,540
Kifo cha TRC :Wahujumu Uchumi na Mafisadi wamehusika na kuneemeka
Waswahili husema temba ujionee. Enzi za enzi, malori yalikuwa ni Mwanamboka na Superdoll, Kugis na Wachaga wachache.
Leo hii mtiririko wa Malori ni mkubwa mno na unatisha. Nimeona malori mengi sijapata ona katiba vijibarabara vyetu. Katika umbali wa kilometa 60, pale Saranda mpaka Isuna Singida ambako hakuna lami, nimekutana na malori 300+ katika kipindi cha dakika 90! Barabara mbovu, bado ya kokoto na mchanga, malori ni makubwa mno na mazito.
Nikakum buka foleni ya maloriniliyoiona KIbamba, Mlandizi, Chalinze, Morogogoro na Gairo. Nikajiuliza imekuaje Tanzania kuna malori mengi kiasi hiki?
Nikajiuliza, kwani hatuna reli kusafirisha mizigo, iwe ni makontena, mafuta hata marobota ya pamba?
Jibu lake ni kuwa TRC imekufa baada ya Serikali kuamua kuwaleta Rites waiendeshe na wala si wale Wajerumani.
La zaidi baada yakuongea na wafanyabiashara wengi, nikaambiwa zaidi ya asilimia 50 (50%) ya malori ya mizigo, ni mali za viongozi wa Serikali, Polisi na watumishi wa Umma!
Wale wadudu wa Mukichwa wakaunganisha moja jumlisha moja ni Uhujumu!
Sasa siku nyingi nilikuwa nikidhamiria kuwalaumu Rites, ambao hawakwepi lawama kwa kutuhukulia mabehewa yetu na kutuletea vihiyo kuongoza kampuni yetu. Lakini wao walikuwa ni wepesi kuhongeka na si Mjerumani na ndio maana Serikali ikakimbilia kuileta Rites na si ajabu kama Richmond, walikuwa na bei Poa!
Kilivhotokea ni kujihujumu wenyewe na wala tusielekeze vidole kwa Rites, wao lawama kwao na kuwajibika kwa ni matokeo ya nia na vitendo vyetu.
Ama kweli Tanzania itajengwa na wenye Meno! Ikiwa wakubwa wanadiriki kulihujumu Taifa kwa kuzamisha utendaji wa Shirika la Reli ili wao wapate pesa kutokana na malori yao, swali linakuja, kwanini basi tusiwaongezee makosa ya kuharibu barabara zetu, kuharibu mazingira, kuongeza uagizaji wa vipuli vya magari na ongezeko la ununuzi wa mafuta?
Mnakumbuka ule mkasa wa Elisante Muro kutaka kujenga bomba la mafuta ambalo alipewa Richmond, na sasa mtu mwingine? Kama Muro alikuwa na pesa na kila kitu kujenga bomba kama la Tazama kutoka Dar mpaka Mwanza, hatuoni kuwa tusingekuwa na haja ya kuwa na matenka ya mafuta ya mita kumi yakiongozana barrabarani huku yakididimiza lami yetu na kuleta msongamano?
Hivi hawa wahujumu, ni wajinga kiasi gani kuwa hawaoni dhamira zao kwa kuhujumu kimoja jinsi kinavyohujumu vingi , mengi na wengi?
Wengine wao wamediriki hata kutafuta watu wakangoe mataruma ya Reli kwa makusudi kabisa ili Reli isipite, sasa siku Reli ya Rwanda ikianza kazi sijui itakuweje!
Labda tuwape semina hawa viongozi wetu tuwafundishe nja za ujasirimali na uzalishaji mali ambazo hazitaleta hujuma!
Poleni Wahindi wa Rites, mnabeba msalaba mzito kwa kuwa mliingizwa mkenge!