KiFUA KUBANA: Kama nakanyagwa kifuani au nachomwa kisu

KiFUA KUBANA: Kama nakanyagwa kifuani au nachomwa kisu

Old Member (Retired)

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2012
Posts
3,401
Reaction score
1,610
Habari zenu wakuu,
Nina rafiki ambaye amekuwa akisumbuliwa na kifua kubana hasa anapokuwa na msongo wa mawazo(ni kwa muda usiopungua miaka minne sasa), maumivu hayo hayatokei mara kwa mara ila yanapotokea dawa yake huwa maziwa yaani akinywa maziwa maumivu hayo yanapungua taratibu hatimae kutoweka: anasema maumivu hayo ni kama kuna mtu yupo juu ya kifua anamkanyaga au kuna mtu ana kitu chenye ncha kali anamchoma kwenye kifua.

katika kuuliza baadhi ya watu wanasema kuwa inaitwa chembe ya moyo ambayo ni dalili ya mwanzo kabisa ya vidonda vya tumbo(ulcers) hivyo wiki iliyopita alikwenda hospital kupima na hakukutwa na vidonda vya tumbo.
Je? Tatizo linaweza kuwa nini wakuu?
Natanguliza shukrani zangu za dhati kwenu.
 
Back
Top Bottom