Kifungo Cha Paul Pogba Kimepunguzwa, Atarajiwa Kurudi Uwanjani Machi 2025

Kifungo Cha Paul Pogba Kimepunguzwa, Atarajiwa Kurudi Uwanjani Machi 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Kifungo cha miaka minne cha Paul Pogba kutojihusisha na soka baada ya kudaiwa kutumia dawa za kusisimua misuli kinyume na taratibu za soka, kimepunguzwa hadi miezi 18 baada ya kufanikiwa kukata rufaa katika Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo.
IMG_0058.jpeg

Pogba sasa ataweza kurejea tena kuichezea Juventus kuanzia Machi 2025 na kuendelea baada ya kufungiwa kujihusisha na masuala ya soka hadi Agosti 2027.
photo-output.jpeg
 
Paul Pogba, kiungo wa Juventus, amepunguziwa adhabu yake ya miaka minne hadi miezi 18 baada ya Rufaa kufanikiwa katika Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (Court of Arbitration for Sport).

Pogba alipewa adhabu hiyo baada ya kupatikana na hatia ya kutumia madawa ya kusisimua misuli, kufuatia uchunguzi uliofanyika September 2023 ambapo alikutwa na viwango vya juu vya metaboliti za Vichicheo vya testosterone.

Awali, adhabu hiyo ilikuwa inamzuia Pogba, mwenye umri wa miaka 31, kucheza hadi Agosti 2027, lakini baada ya Rufaa kusikilizwa, kipindi hicho kimepunguzwa, Pogba sasa atakuwa nje ya uwanja kwa miezi 18 badala ya miaka minne, na anatarajiwa kurudi mazoezini na Juventus ifikapo Januari 2025.

Iwapo kila kitu kitaenda vizuri, Pogba anatarajiwa kurejea kwenye michezo rasmi kufikia Machi 2025, akiungana tena na wenzake katika mechi za ushindani baada ya kipindi cha kusimamishwa kwa matumizi ya dawa za kusisimua misuli.

IMG_1410.jpeg
 
Bora maana hiyo ndio ajira yake
Arudi na pale kwenye french team maana viungo hata hawajulikani wanaunga Nini ni kama wale wa Simba
 
Back
Top Bottom