Paul Pogba, kiungo wa Juventus, amepunguziwa adhabu yake ya miaka minne hadi miezi 18 baada ya Rufaa kufanikiwa katika Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (Court of Arbitration for Sport).
Pogba alipewa adhabu hiyo baada ya kupatikana na hatia ya kutumia madawa ya kusisimua misuli, kufuatia uchunguzi uliofanyika September 2023 ambapo alikutwa na viwango vya juu vya metaboliti za Vichicheo vya testosterone.
Awali, adhabu hiyo ilikuwa inamzuia Pogba, mwenye umri wa miaka 31, kucheza hadi Agosti 2027, lakini baada ya Rufaa kusikilizwa, kipindi hicho kimepunguzwa, Pogba sasa atakuwa nje ya uwanja kwa miezi 18 badala ya miaka minne, na anatarajiwa kurudi mazoezini na Juventus ifikapo Januari 2025.
Iwapo kila kitu kitaenda vizuri, Pogba anatarajiwa kurejea kwenye michezo rasmi kufikia Machi 2025, akiungana tena na wenzake katika mechi za ushindani baada ya kipindi cha kusimamishwa kwa matumizi ya dawa za kusisimua misuli.