Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
Kifungu hicho kinasema kuwa mbunge akikosa kuhudhuria vikao vya bunge mara tatu mfululizo bila ruhusa ya Spika basi mbunge huyo anapoteza ubunge wake. Kifungu hiki hakijatumika nchini hapa ila tu kwenye bunge hili la 12 ambapo wabunge wawili wa chama cha upinzani cha CHADEMA tayari wameshanyang'anywa viti vyao.
Kifungu hiki, kama ambavyo vifungu vingi vya katiba yetu vilivyo, kina mapungufu makubwa sana yanayomruhusu Spika kumnyang'anya kiti mbunge yeyote ambaye kwa sababu zozote atashindwa kuhudhuria vikao vitatu. Hakuna maelekezo ya kikatiba jinsi gani Spika atatoa ruhusa hiyo; kwa mfano iwapo mbunge ni mgonjwa kama ilivyo kwa Tundu Lisu, lakini Spika akachelewa au akakataa kujibu maombi ya mbunge huyo kutohudhuria vikao hadi ikafikia mbunge ameshakosa vikao vitatu, basi bado spika huyo huyo ndiye atakayeamua kumnyang'anya mbunge kiti chake. Kwa maoni yangu, kifungu hicho kinaweza kuboreshwa kwa kusomeka kama ifuatavyo:
(c) where a Member of Parliament fails to attend three consecutive meetings of the National Assembly for unacceptable reasons as determined by the Parliamentary Committee on Power, Ethics and Privileges of the Parliament.
======
71.-(1) Mbunge atakoma kuwa Mbunge na ataacha kiti chake katika Bunge litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo-
(a)ikiwa litatokea jambo lolote ambalo, kama asingekuwa Mbunge lingemfanya asiwe na sifa za uchaguzi au apoteze sifa za uchaguzi au asiweze kuchaguliwa au kuteuliwa kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii;
(b)ikiwa Mbunge huyo atachaguliwa kuwa Rais;
(c)ikiwa Mbunge atakosa kuhudhuria vikao vya Mikutano ya Bunge Mitatu mfululizo bila ya ruhusa ya Spika;
(d)ikiwa itathibitishwa kwamba amevunja masharti ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;
(e)ikiwa Mbunge ataacha kuwa mwanachama wa chama alichokuwamo wakati alipochaguliwa au alipoteuliwa kuwa Mbunge;
(f)iwapo Mbunge anachaguliwa au anateuliwa kuwa Makamu wa Rais;
(g)kwa Mbunge ambaye anatakiwa kutoa taarifa rasmi ya mali kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 70, ikiwa atashindwa kutoa hilo tamko rasmi kwa mujibu wa masharti ya hiyo ibara ya 70 katika muda uliowekwa mahususi kwa ajili hiyo kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge,lakini iwapo Mbunge hatakoma kuwa Mbunge kwa mujibu wa jambo lolote kati ya mambo hayo yaliyotajwa na kama hatajiuzulu au kufariki mapema zaidi, basi Mbunge ataendelea kushika madaraka yake kama Mbunge mpaka wakati Bunge litakapovunjwa kwa mujibu wa ibara ya 90, bila ya kuathiri haki na stahili zinazotokana na ubunge wake.
(2) Bunge laweza kutunga sheria kwa ajili ya kuweka masharti yatakayomwezesha Mbunge kukata rufaa, kwa mujibu wa sheria kupinga hukumu ya kuthibitishwa kwake kuwa ni mtu mwenye ugonjwa wa akili au kupinga adhabu ya kifo au kufungwa gerezani, au kupinga kupatikana kwake na hatia kwa kosa la aina iliyotajwa kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (5) ya ibara ya 67 ya Katiba hii na sheria hiyo yaweza kueleza kwamba hiyo hukumu iliyopingwa na huyo Mbunge haitatiliwa nguvu kisheria mpaka umalizike kwanza muda utakaotajwa katika sheria hiyo