Kifungu cha 3.9 cha Muongozo wa Anwani za Makazi kinatumika vibaya

Kifungu cha 3.9 cha Muongozo wa Anwani za Makazi kinatumika vibaya

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2016
Posts
520
Reaction score
2,930
Kifungu hiki nimeakiambatanisha chini kinazuia watu walio katika hifadhi,mabondeni,Pembezuni mwa eneo la Barabara na maeneo mengine yanayoitwa hatarishi kutotakiwa kuwekewa anwani za makazi .Matokeo yake kifungu hiki kimekuwa kikitumiwa vibaya na hivyo hata wakazi wenye haki ya kupewa anwani za makazi wananyimwa sasa.

mfano,
Kitongoji cha Katoto,kata na Kijiji cha Kagerankanda tarafa ya Makere,Wilaya ya Kasulu-Kigoma.Wakazi wa eneo hilo wamenyimwa kuwekewa anwani za makazi eti wapo katika Hifadhi.Ikiwa ni wakazi wa eneo hilo tangu 1942 na huduma za kijamii zipo zinapelekwa kama shule tangu 2003 na usajili wake ni No.E.M 11780.Kuna zaidi ya kaya 834.

Lazima kuwe na utaratibu hata kama Muongozo wa Anwani za makazi unakataa kuwapa Anwani watu waishio katika Hifadhi ila tujiulize ni nani anayeamua kwamba eneo fulani ni hifadhi hivyo wakazi hawapewi Anwani za makazi ni nani anayeamua ?.

Sababu tukiliacha hili kupita maeneo mengi yenye wakazi hawatapewa Anwani za makazi . Jambo hili linapaswa kuangaliwa kwa umakini Mkubwa kuna maeneo ambayo Wananchi wanaishi miaka yote ,unawezaje kusema wapo katika hifadhi .Miaka yote wanaishi hapo tangu 1942 ,huduma za kijamii mnapeleka alafu leo mnawageuka kwamba wapo katika hifadhi ,Mh.nape , Bashungwa naomba hili mliangalie .Mnaweza kudhani zoezi la anwani ya Makazi limeisha kumbe maeneo mengi kutayameachwa .

Mfano,nilimsikia DC wa Wilaya ya Ilemela Mh.Hassani Massala anasema ,Wilaya ya Ilemela zoezi linakaribia kuisha na hakuna shida yeyote, ila sisi ACT wazalendo tulifanya ziara huko Ilemela maeneo ya Kabangaja,kata ya Bugogwa Wilaya ya Ilemela ,tukaenda hadi Igombe na Kayenze moja ya kilio kikubwa cha wakazi wa maeneo haya ni kuhusu kuzuiwa kujenga ,kuendeleza maeneo yao sababu ya hoja ya upanuzi wa Barabara ya Airport -Igombe hadi Kayenze .

Wamezuiwa kuendeleza maeneo yao ni miaka sasa hakuna mchakato wa upimaji, tathimini wala uhakiki .Na hakuna mrejesho au majibu yeyote kutoka kwa serikali juu ya suala hili .

Na zaidi pia wameambiwa hawawezi kupewa Anwani za Makazi . Serikali lazima itoe jibu la uhakika kwa wananchi hawa kuliko kukaa kimya kiasi hiki.

Ninashauri Mh.@nape_nnauye na @innocentbash anzeni kufuatilia maeneo ambayo Wananchi wamenyimwa Anwani za makazi kwa mujibu wa hiki Kifungu cha 3.9 cha Muongozo wa Anwani za Makazi ili kuhakiki na kujiridhisha kama kweli wakazi hao walinyimwa kuwekewa anwani za makazi kihalali au laa.

Abdul Nondo.

IMG_20220520_141935_183.jpg
 
Back
Top Bottom