Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Kabla ya ujio wa wakoloni wahenga walikua wawindaji. Wenye nguvu waliwinda wanyama na wengine wakitembea kutafuta mizizi na matunda. Matunda ya asili yalikua ni pamoja na matango.
Wawindaji waliacha mitego usiku na waliamka alfajiri kuangalia mawindo. Mnyama aliyepatikana alichinjwa na kwakua maini, figo na moyo viliiva haraka hivi vilitengenezwa haraka kama kifungua kinywa.
Familia zilikula pamoja, walioleta matunda pia yaliwekwa kusindikizia kifungua kinywa. Enzi hizo waliopata wanyama kwa chakula ndiyo walioa wake wazuri. Huna haja ya kuhonga iPhone 11, wewe unahonga mguu wa nyati na unapata heshima ukweni.
Milo ya nafaka ililetwa na wakoloni. Walianza kuwapa babu zetu uji wa mahindi ili wapate nguvu ya kuwabebea mizigo yao.
Vyakula vyetu vya asili vilitulinda na magonjwa mengi. Nafaka si nzuri hasa katika kudhibiti sukari ya mwili.