Mwanakijiji, hayo yote au mengi ya uliyoyasema na kuyataja yanahusu Tanzania. Je, ina maana na kwingineko Afrika hususan kusini mwa sahara (black Africa) na kwenyewe tatizo lao ni uongozi mbovu?
Jibu langu ni ndiyo; yote yanaanzia kwenye uongozi na wale wanaowapa watu uongozi. Siyo sawa hasa kusema uongozi mbovu lakini zaidi ni uongozi usiona uwezo (si kwamba umeharibika).
Kama ni hivyo ina maana uongozi mbovu ni common denominator Afrika nzima kusini mwa jangwa la sahara. Sasa kwa nini kote huko kuwe na uongozi mbovu? Ndivyo Tulivyo kuwa hatuwezi uongozi? What is it? Maana mimi siamini kabisa kuwa hizo nchi zingine za Kiafrika zimetuzidi kihivyo. Nimeshabahatika kutembela baadhi ya nchi za Kiafrika na sikuona lolote la ziada tulilozidiwa.
Hapana siyo Tanzania tu.. suala la uongozi linahusu sehemu nyingi duniani; siyo za watu weusi tu bali hata za watu weupe. Kinyume na unavyofikiria utaona kuwa hata hizo nchi za weupe si zote zimepiga hatua kubwa za maendeleo. Bado kuna watu wanaishi katika umaskini katika baadhi ya nchi hizo. Ukienda Bulgaria, maeneo ya Georgia, Ukraine, Urusi n.k bado kuna sehemu watu wanatumia jembe la mkono na huwezi kuamini! Hiyo china yenyewe pamoja na "maendeleo" tunayoyaona Beijing, Shanghai na Hong Kong bado inamaeneo watu wanaishi kama wako Kyela! Lakini katika Afrika hii hii utaona kuna nchi ambazo zinapiga hatua zaidi pole pole na ndio maana wengine tunaangalia ka nchi kama Rwanda kana potential ya kufanya kile ambacho nchi kama Uganda, Kenya na Tanzania zimeshindwa. Na Kagame amejifunza sana kwa Mwalimu; as a matter of fact anacopy program zile zile za Mwalimu wakati wa Uhuru lakini sitoshangaa akija Rais mwingine huko Rwanda ikajikuta inaelekea huku huku tulikofikia sisi.
Kama ufisadi hata Cameroun upo.
Hata Marekani, Japani, Ujerumani na UK ufisadi upo! Kipimo hakiwezi kamwe kuwa ufisadi. Kama uhalifu upo Detroit kama ulivyo Dar, kama wizi wa magari upo Miami kama ulivyo Nairobi; so hatuwezi kuweka kipimo kiwe uhalifu. Kama ni uchangudoa basi upo mitaa ya Ohio Dar kama ilivyo barabara ya nane hapa Detroit; hatuwezi kutumia uchangudoa kama kipimo.
Kama vya kupenda vya Ulaya basi hata Niger wanapenda vya Ulaya.
Hata wamarekani wanapenda vya Ulaya, na Wajapani wanapenda vya Marekani, na Wa Korea wanapenda vya US; hatuwezi kutumia kupenda vya ulaya kama kipimo.
Sasa nisichoelewa ni kwa nini Afrika nzima kusini mwa sahara ni sehemu iliyo ktk kundi la nchi za ulimwengu wa tatu. Sielewi kabisa hili. Inakuwa kuwaje eneo kubwa kama hili kiwango cha maendeleo kinakuwa kimefanana sana?
Ni uongozi; uongozi; uongozi;. Damu ya mzungu ni nyekundu kama ilivyo damu ya mfipa; mtandao wa mfumo wa fahamu wa Mjerumaini umetandazwa mwili kama ulivyotandazwa mfumo wa fahamu wa Mmakua! Ukienda kwa wazungu utaona kuwa makundi yao ya damu ni sawa kabisa na yale ya wanyaturu! Ndio maana utaona kuwa katika sayansi watu weusi, wachina, wahindi, wazungu, wajapani, waarabu n.k siyo species tofauti za binadamu! Sisi sote tuko specie moja tu. So hakuna sababu ya kibaiolojia wala ya kigenetic inayoweza kumfanya mtu wa Afrika kushindwa kufanya kile ambacho kinafanywa na mtu mwingine.
Ni kutokana na hilo usishangae wapo Waafrika ambao wameweza kusomea na kufanya yale ambayo tulidhania ni ya "wazungu". Tunaendesha magari yao, tunachezea kompyuta zao, tunajifunza fizikia yao na kufanya vizuri kama wao kama siyo zaidi n.k I do not believe in the INFERIORITY THEORY OF BLACK PEOPLE.
Bara la Ulaya sio nchi zote zilizoendelea saana kihivyo. Hakuna uniformity ya maendeleo. Huwezi kulinganisha kwa mfano maendeleo ya Ujerumani na Uholanzi na yale ya Romania. Lakini hata hao Romania wameendelea kuliko nchi karibu zote kama sio zote kabisa za Afrika,
Sasa hapa ni lazima tuangalie kitu kingine cha tofauti sana; ni kwamba huwezi kuelewa kutoendelea kwa haraka kwa Afrika bila ya kuangalia historia ya Afrika. Kwa kiasi kikubwa unaposema kuendelea kwa Europe unataka kujaribu kukutenganisha na kutoendelea kwa Afrika. There is an inversely relationship between the development of Europe and the underdevelopment of Africa. The two can not be taken singularly.
Sasa huu uongozi mbovu ina maana upo Afrika nzima? WTF.....
the answer again is Yes! unless we change the nature of our leadership and how we are governed we are doomed to perpetual underdevelopment. Africa suffer from an acute shortage of inspiring, daring and robust leadership. It is a sort of leadership anemia.