Kigamboni: Hivi Kwanini Mwendokasi Wanazikataa N-CARD?

Kigamboni: Hivi Kwanini Mwendokasi Wanazikataa N-CARD?

Marumeso

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2009
Posts
1,410
Reaction score
1,325
Hizi kadi za kielektroniki zililetwa kwa mbwembwe nyingi na ilielezwa zitatumika maeneo mengi ya kufanya malipo ikiwa pamoja na mwendokasi.

Lakini cha ajabu leo hii kadi hizi zinatumika kwenye mpira wa ligi kuu na kule kwenye vivuko/pantoni za kuvukia kigamboni tu basi. na ukifika maeneo haya mawili hawakubali njia nyingine yoyote ya malipo zaidi ya hizo kadi. Sasa kichekesho ukifika kule mwendokasi hawataki kabisa kusikia wala kuzitambua hizo kadi. Wao wanataka pesa keshi mkononi!

Hii kitu inaleta usumbufu sana tena usio wa lazma kwa wananchi. Unajaza pochi na kadi kibao lakini unatumia kwenye maeneo machache tu huko vivukoni na huko kwingine hawazitaki.

Yani wananchi wanakuwa kama wapo kwenye jamhuri mbili tofauti wakati ilitakiwa mtu unajaza tu hela yako kwenye kadi moja unazunguka huko kote kwa hela ya kwenye kadi. mbunge NDUGULILE libebe hili kama ulivyobeba swala la daraja wananchi wako wanataabika uku.
 
hapo lazma jamaa wa mapantoni na hao wenzao wa mwendokasi kila mmoja anatetea kesho yake kwanza japo ilibidi waelewane tu asilimia za mgao maana wote ni serekali
 
mwendokasi kuna upiga... kadi itapunguza urefu wa kamba
 
Back
Top Bottom