Kigamboni Kisota vs Kibada, Wapi pako poa?

Kigamboni Kisota vs Kibada, Wapi pako poa?

Msomaji2

Member
Joined
Feb 28, 2022
Posts
17
Reaction score
38
Habari wapendwa, niliwahi uliza kati ya Goba & Kigamboni wapi pako poa.

Kutokana na uwepo wa jamaa zangu wengi maeneo ya kigamboni, nimeamua kwenda huko.

Sasa kisota na kibada ndo napawaza maana bei maeneo hayo zinaonekana hazipishani sana

Kwa uzoefu wenu kisota na kibada wapi panaFaa zaidi?

1. Changamoto & faida za kila eneo tajwa hapo, ili nione wapi patafaa zaidi.

Natanguliza shukrani[emoji120]
 
Mimi nitakwambia Kisota kwa sababu zifuatazo:

- Eneo halikai maji (sio la tope tope) na ardhi yake iko very stable (kwa vile ina mchanganyiko na mawe)

- Kwa nilipojenga ni eneo la mawe mawe kwa hivyo nilipokuwa nachimba kifusi nilipata mawe na kifusi kingi sana ambacho nilikitumia katika ujenzi
 
Issue kama usalama, huduma za kijamii, na vipi kuhusu migogoro ya ardhi n.k
..
 
Kuhusu usalama kuna maeneo yana ulinzi shirikishi. Kuhusu migogoro ya ardhi nunua katika maeneo yaliyopimwa ili uwe na uhakika. Kabla hujanunua ni vyema ukenda Wizara ya Ardhi kuhakikisha jina la mwenye kiwanja.
 
Mchango mzuri sana, nimeona wanaweka lami njia ya kisota, japo kule shangwe nimeenda wameJenga mno
 
Sqrm wana range elfu45 hadi 60 ( yani maeneo tofauti ila bei zinaendana).
 
Habari wapendwa, niliwahi uliza kati ya Goba & Kigamboni wapi pako poa.

Kutokana na uwepo wa jamaa zangu wengi maeneo ya kigamboni, nimeamua kwenda huko.

Sasa kisota na kibada ndo napawaza maana bei maeneo hayo zinaonekana hazipishani sana

Kwa uzoefu wenu kisota na kibada wapi panaFaa zaidi?

1. Changamoto & faida za kila eneo tajwa hapo, ili nione wapi patafaa zaidi.

Natanguliza shukrani[emoji120]
Mikwambe kuna mtaa wa kishua unaitwa Changanyikemni karibu na nyumba za NSSF , pale ni bomba sana.
 
Kisota ni bora zaidi, kwa sbbu mpangilio wa nyumba upo vizuri, eneo ni tambalale, barabara za mitaa imepangiliwa vizuri kama mbezi, ni rahis kufika kigambon, au darajanj, hakuna uswahili

Sent from my M2010J19SI using JamiiForums mobile app
 
Habari wapendwa, niliwahi uliza kati ya Goba & Kigamboni wapi pako poa.

Kutokana na uwepo wa jamaa zangu wengi maeneo ya kigamboni, nimeamua kwenda huko.

Sasa kisota na kibada ndo napawaza maana bei maeneo hayo zinaonekana hazipishani sana

Kwa uzoefu wenu kisota na kibada wapi panaFaa zaidi?

1. Changamoto & faida za kila eneo tajwa hapo, ili nione wapi patafaa zaidi.

Natanguliza shukrani[emoji120]
Kisota ambapo bei ni sawa na kibada basi chukua Kibada. Ka sababu Kisota bei itakuwa juu na panahitajika sana.
Ila kama una mchuma, chukua Gezaulole beach plot, bei karibu sawa ila wanao wataenjoy.
 
Habari wapendwa, niliwahi uliza kati ya Goba & Kigamboni wapi pako poa.

Kutokana na uwepo wa jamaa zangu wengi maeneo ya kigamboni, nimeamua kwenda huko.

Sasa kisota na kibada ndo napawaza maana bei maeneo hayo zinaonekana hazipishani sana

Kwa uzoefu wenu kisota na kibada wapi panaFaa zaidi?

1. Changamoto & faida za kila eneo tajwa hapo, ili nione wapi patafaa zaidi.

Natanguliza shukrani[emoji120]
Aisee..
Nami nachukua data
 
Kisota advantage ni kuwahi kwenda mjini....kuna access na kwenda mjini zaidi kuliko kibada halafu hakuna maji ...
Kibada usinunue eneo bila kwenda wakati wa masika......

Kisota pia kulipimwa mwanzo kwahiyo wale wazee wa Kigamboni WA mwanzo wote wapi hapo au Wana nyumba hapo...
 
Kisota Bei zimesimama ila unaweza kujenga fasta ukahamia Kuna mitaa ukijenga nyumba ya ovyo utahisi aibu mwenyewe ..Watu Wanafungia mijengo kweli na viwanja vile vikubwa ni Bei ndefu sana .

Usalama Kuna mitaa kumepigwa mageti makalio kinoma hata panyaroad hawezi kusogea anaweka kupiga bastola maana wapo matajiri kwa sana
 
Kote uko pazuri..angalia uwezo wako wa kujenga pia...uwe na uwezo wa kujenga ghorofa...sio majirani zako wana maghorofa wewe unakakibanda...
 
Back
Top Bottom