Kigamboni kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa makundi maalumu, wanawake watakiwa kutumia fursa ili kujiimarsha kiuchumi

Kigamboni kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa makundi maalumu, wanawake watakiwa kutumia fursa ili kujiimarsha kiuchumi

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Kigamboni imekuwa ikitenga asilimia kumi ya mapato ya ndani ili kuwawezesha Wananchi kiuchumi kupitia vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu sambamba na kutoa mikopo yenye Riba nafuu kwa Wajasiriamali wadogo wadogo Ili iweze kuwainua kiuchumi.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Bi. Halima Bulembo wakati wilaya hiyo ikiadhimisha Siku ya Wanawake Duniani ambayo Kitaifa itafanyika mkoani Arusha Tarehe 8 Mwezi March 2025 juku mgeni rasmi akitarajia kuwa Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Nao baadhi ya wakazi wa Wilaya Ya Kigamboni wakiwemo Wajasiriamali wamezungumzia umuhimu wa maadhimisho hayo huku baadhi yao wakazungumzia Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia.

 
Back
Top Bottom