Binafsi nina furaha sana kuhusu mbunge wangu kuwemo humu jamvini na kujadili matatizo ya jimbo letu letu moja kwa moja lakini tatizo kubwa linalozungumziwa hapa sidhani kama ni la kigamboni peke yake liko maeneo mengi sana nchi kwetu na linakera sana ila naomba kuchangia hoja hii kwa mtindo tofauti kidogo, kwanza ingependa mbunge alichukulie hili jambo kama hoja ya kitaifa badala ya kuangalia maeneo ya kwetu tu maana mara nyingi hawa wanakatisha safari hujadiliana na walioko kwenye daladala na kurudia mji mwema au ungindoni na wale wanaotaka kuja upande wa mjini hupata adhabu kubwa sana ila kwa kuna matatizo makubwa sana kigambo nzima kwa ujumla hasa masuala ya viwanja, maji, elimu na afya nadhani kuna matatizo ya ki utawala maana hata ukingalia utofauti wa shule za msingi mji mwema na maweni utaona tofauti kubwa wakati ni shule majirani kuna mengi ya kujadili kuhusu jimbo letu tena ya maana ni vizuri sisi tuliopata ka nafasi haka ka kujadiliana na mbunge wetu tujenge hoja za msingi na tuziwakilishe kwa mheshimiwa mbunge kwa ajili ya kuzitafutia ufumbuzi badala ya kushambuliana humu jamvini.