Kigamboni Wing: Special Thread

Kigamboni Wing: Special Thread

Amalinze

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2012
Posts
6,780
Reaction score
5,305
Habari wadau,

Kigamboni ni peninsular ambayo inapatikana dsm,Tanzania ambayo inawakazi wanaokaribia takribani 200,000 kama wakifanya sense mwaka huu(2015).Kigamboni ipo wilaya ya Temeke ambayo kwa sasa jimbo ili linaongozwa na Dr F. Ndugulile(CCM) alichuana na Mama Komu(CDM).Wabunge waliowahi kuongoza jimbo la kigamboni ni Masoud,Mwinchoum na Kitwana Kondo.

Kigamboni ina mitaa mingi na vitongoji kibao ambavyo,ukianzia ferry kivukoni kupitia barabara ya baharini utakutana na kwanza mtaa wa ferry,tuamoyo,mjimwema,kibugumo,gezaulole,mwongozo,dege,cheka,mbutu,Kimbiji,Gomvu,Mwembe mdogo,Yaleyale Puna,Ungindoni,Kibada,Kisarawe,mwasonga,kwaurasa,Buyuni,Toangoma.Enzi hizo tulikuwa tunawacheka watu waliokuwa wanakaa kibada lakini kwa sasa ukikaa kibada unaonekana unazo.Kigamboni tuliyoanza nayo kiwanja Kikubwa ulikuwa unapata kwa Tsh 180(1979) na Shamba zuri ekari mbili ulikuwa unapata kwa elfu 10(1990).

Kigamboni tulikuwa na vilabu vikubwa vya pombe enzi hizo,tulikuwa na vilabu kikubwa va pombe za kienyeji kama SERENGETI,MGAZA na FOKOLENDI,hapo ni mwendo wa wanzuki,mnazi,ulaka,kangara,pingu,kinibu,gongo,ulanzi,mbege bila kusahau supu ya makongolo na makwasusukwasu(mabaki ya nyama ya ngombe aka mapanki)

Kigamboni ya sasa si ile kigamboni tulioijua sisi ya 70’s-90’s,kigamboni ya sasa mnavuka kwenye pantoni haujuani na mtu hata mmoja.Kigamboni tuliyoikuta sisi kabla ya kuja vivuko hivi tulikuwa tunavuka na ngalawa/mitumbwi ambayo imesababisha vifo vingi sana miaka ya 80’s.Baada ya majanga ya vifo serikali ilianzisha pantoni ambazo za kwanza zilizoanza ilikuwa Mv.Dezo,Mv.Usiwe Kupe,MV Lami,MV Alina,MV Mkombozi,wakazi wengi wa sasa hawajawahi kupanda hayo mapantoni wengi wameanza kupanda haya ya sasa MV Magogoni(1996) na MV Kigamboni(2009).Kwa sasa kigamboni inakaliwa na wakuja wengi kuliko wazawa.Kila uendapo lazima utakutana na mtu mwenye fedha wa eneo husika,kwa kwetu kigamboni tajiri wetu mkubwa ni SCABA SCUBA(source ya utajiri wake ni Hardware,Real Estate,Construction).

Kigamboni ilikuwa na watemi sio watemi wale kama kina isike la hasha hawa kwa sasa wanaitwa wababe.Kigamboni watemi waliotesa enzi hizo waliojizolea umaarufu miaka ya 90’s ni Mtemi SANCHO,huyu jamaa alikuwa hatari alikuwa anaogopeka na wahuni wote wa ferry,jamaa kazi yake ilikuwa ni mvuvi ila inasadikika alikuwa na mshipa wa nguvu ambapo hata wakija askari hata 10 mnaweza mkashindwa kumkamata,kwa sasa ameokaka na anampenda yesu.Watemi wengine alikuwa Fadhili MBICHWA na HASSAN MLINZI,hawa jamaa walikuwa wanashinda sana mikoroshi ya Tiper na Tazama,Ukikutana na Fadhili Mbichwa/Mlinda Hasani lazima uachie Rambo au Fuko lote la korosho.

Kigamboni kulikuwa na viwanda vikubwa sana ambapo wakazi wengi wa kigamboni tulikuwa tunapata ajira za tempo,kulikuwa na viwanda vya Samaki(TAFICO),tulikuwa na kiwanda vya TIPPER,tulikuwa na kiwanda cha TAZAMA enzi hizo za mwalimu,ila kwasasa yamebaki majengo tu.Kigamboni pia tuna kambi kubwa za jeshi,tuna kambi ya Navy na Kikosi cha mizinga.Ukiachilia mbali ya vitu hivyo pia tuna Chuo kikuu cha mwalimu nyerere(CCM College).Kwa viwanja vya michezo tuna viwanja vikubwa ni Kiwanja cha Shababi,Kiwanja cha mpira tipper na Machava.Hivyo viwanja vimetumiwa sana na wachezaji wa zamani wa samba na yanga,kwa mara ya kwanza nilimuona Keneth Mkapa na Salum Kabunda ninja walikuja kufanya mazoezi Kiwanja cha Machava.

Kigamboni tumejaaliwa kuwa na beach za kutosha kama Mikadi Beach,The Hunters,Beach Kimba(Ya walalahoi),Chadibwa,Ng’onda Beach,Kipepeo,Baracuda,Sunrise na South Beach.Pia kigamboni tunayo Sehemu za kutalii na kutembelea watoto kama Fun City iliyopo toangoma na DSM Zoo iliyopo Mwasonga.

Kigamboni tumejaaliwa kuwa na mastars waliotingisha katika fani mbali mbali kuanzia mpira,bongo fleva,radio n.k.Miongoni mwa mastars wakazi halisi wa kigamboni(Si wakuja) tunaye Producer BIZMAN wa Sound Crafeters,Tunae Producer anayetingisha kwa sasa MAN MAJI(MAN WATER),pia tunae Z-Anto na JOS Mtambo na Da Joh,Katika anga za Radio tunae Fundi Mitambo maarufu wa RTD ndugu RANDO Mabura na Sara Dumba(RC).Katika Medani za Soka tunao wachezaji waliowahi kuchezea yanga kama kina Deo Lukasi na Deo Flani(Jina nimelishahau).Mbali na hao wana Kigamboni ha hasili pia tunao stars ambao kwa sasa wanakaa kigamboni kama Kitenge(wa EATV Juke Box),Tunae Monalisa Bongo movie,Tunae Mpoki(Tajiri la Kihaya Zecomedy) na Dokii.
Hayo ni machache ninayoyajua,najua na wewe una mengine si mbaya nawe uka-share.
 
Daa ndugu kama umemaliza ivi kweli wewe ni wakigamboni lakini shule za msingi kama kigamboni,ufukoni ,tungi ,vijibweni,mawenzi,mjimwema,gazaulole Nk
Time za mpira wamiguu
Shababi,navy,bafanabafana,kk,fanja,tuamoyo,nanga,
daaa tulikuwa tukikutana kwenye panton lazima tujuane si sasaivi
Nawasilisha nkikumbuka ntaendelea
 
Daa ndugu kama umemaliza ivi kweli wewe ni wakigamboni lakini shule za msingi kama kigamboni,ufukoni ,tungi ,vijibweni,mawenzi,mjimwema,gazaulole Nk
Time za mpira wamiguu
Shababi,navy,bafanabafana,kk,fanja,tuamoyo,nanga,
daaa tulikuwa tukikutana kwenye panton lazima tujuane si sasaivi
Nawasilisha nkikumbuka ntaendelea

Mkuu heshima kwako nimeacha mengine muendelee kujazilizia,nimeona umetaja timu kubwa,KK nlikuwa nishaisahau ndugu ila nimeikumbuka kuna KSC pale AJAX,Timu ya Nanga ilikuwa ni noma,na pia usisahau Kupitia kwa Mzee ANKOL au MUSHI Kucheki Luninga wakitoa Nje hahaaaaaaa.
 
Mkuu heshima kwako nimeacha mengine muendelee kujazilizia,nimeona umetaja timu kubwa,KK nlikuwa nishaisahau ndugu ila nimeikumbuka kuna KSC pale AJAX,Timu ya Nanga ilikuwa ni noma,na pia usisahau Kupitia kwa Mzee ANKOL au MUSHI Kucheki Luninga wakitoa Nje hahaaaaaaa.

Pale maeneo ya hospitali kuu ya kigamboni panaitwaje???
 
Pale maeneo ya hospitali kuu ya kigamboni panaitwaje???

Panaitwa Kigamboni hivyo hivyo,Hiyo hospital ipo karibu na Kituo cha polisi pamoja na Club kakala....Ukienda Kulia kwenye ile njia unaelekea Kwa Chagani,ukienda kushoto unaelekea Tuamoyo.
 
Narudi home baada ya Mishe Mishe Zangu.
MV kigamboni.jpg
 
Ofisi ya Serikali ya mtaa wa kigamboni-Hii Picha ilichukuliwa mwaka 2009.Hapo kwenye makuti ndio pamejengwa CLUB KAKALA.
CCM KAKALA.jpg
 
Hapa ni Mjimwema,njia panda ya kibada,lami upande wa kushoto ni njia ya kwenda Kibugumo,mwongozo mpka kimbiji.
MJIMWEMA.jpg
 
Panaitwa Kigamboni hivyo hivyo,Hiyo hospital ipo karibu na Kituo cha polisi pamoja na Club kakala....Ukienda Kulia kwenye ile njia unaelekea Kwa Chagani,ukienda kushoto unaelekea Tuamoyo.

Karibu na magengeni maarufu kwa "urasa"
 
Hizo picha inaonekana zimepigwa siku nyingi au?mbona kule vijibwen panapojengwa daraja na road la kisasa kumekucha sana
 
Kigamboni,tungi kwa mpalasinge.
MAPALASINGE.jpg
 
Back
Top Bottom