Kigamboni yatoa milioni 300/- kwa vikundi 88

Kigamboni yatoa milioni 300/- kwa vikundi 88

elivina shambuni

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2018
Posts
461
Reaction score
295
MANISPAA ya Kigamboni imetoa mkopo yenye jumla ya Sh Milioni 300 kwa vikundi 88 vya wanawake, vijana pamoja na watu wenye ulemavu kwa ajili ya kujiendeleza katika shughuli mbalimbali za ujasiriamali.

Fedha hizo ambazo zimekabidhiwa kwa vikundi hivyo juzi, kiasi cha Sh Milioni 200 zimetokana na marejesho ya mikopo iliyopita na kuifanya jumla ya mikopo iliyotolewa na manispaa hiyo kwa vikundi hivyo vyenye wanachama wapatao 880 hadi sasa kufikia kiasi cha Bilioni 1.3.

Akizungumza wakati wa utoaji wa mikopo hiyo Mkurugenzi wa manispaa hiyo Ng’wilabuzu Ludigija alisema fedha hizo ni utekelezaji wa sera inayozielekeza kila manispaa kutenga asilimia 10 ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya wanawake na vijana pamoja na watu wenye ulemavu.

Alisema katika kuhakikisha wanaviinua kiuchumi vikundi hivyo, manispaa hiyo imeona vyema kuweka mazingira mazuri ya kuviwezesha vikundi kwa wakati huku akivipongeza kwa matokeo mazuri hususani katika urejeshaji wa mikopo hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Sara Msafiri aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, mbali na kumpongeza mkurugenzi wa manispaa kwa utekelezaji mzuri wa sera ya utoaji wa mikopo kwa vikundi hivyo, alisema ni wajibu wa vikundi hivyo kuhakikisha wanazitumia fedha hizo vizuri ili kujiinua kiuchumi.

Chanzo: Habarileo
 
Back
Top Bottom