kigezo cha uzalendo kitumike kutatua swala la ajira

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2018
Posts
2,490
Reaction score
3,584
Habari waheshimiwa!

Kuna kauli moja au msemo mmoja wa waswahili unasema mla nawe ndio mfa nawe.

Nawaomba waheshimiwa kwa nafasi zao walizoteuliwa na kuchaguliwa wasije kuwasahau vijana waliopigwa na mvua na jua na kukesha mpaka kunakucha kuakikisha ushindi unapatikana huwe wa goli la kichwa au la mguu.

Moja ya changamoto ya vijana kwa sasa ni ajira, viongozi mliopata nafasi nendeni mkabuni na mkatutengeneze ajira mpya.

Kuna vijana wazalendo waliowapigania naomba na nyinyi muwape vipaumbele muwapiganie ili kesho ijayo wawapiganie tena, ila msije kuwaona kama mbwa wa mawindo ambaye baada ya kukamata windo hana thamani tena.

Itakuwa fedhea sana mukiwaacha vijana wazalendo wanatanga tanga harafu ajira wakapewa wale wengine ili kesho waje kuitukana serikali, naomba uzalendo utumike kama kigezo cha kutoa ajira.
 
Maybe una point nzuri. Ila uzalendo bila qualification ni hoax.

Huwez mpa mtu position flani wkt hana qualification au experience flani just oin the name of uzalendo.

Uzalendo uambatane na qualifications.
 
Mfumo wa kuwabaini wazalendo uliingia mdudu pale tu wakuu wa shule walipoambiwa wajaze form maalum. Pale watu waliokua home tu walijipeleka kwenye vituo ili wawe registered, wengine walihonga kwa wakuu wa shule ili waandikwe ndiomaana serikali ikaona bora itumie utaratibu wake tu.

Sent from my TECNO-C8 using JamiiForums mobile app
 
Hao wakuu wa shule nao wamepoteza sifa za uzalendo,hizo nafasi zao za ukuu inabdi wawapishe watu wenye uzalendo ..!
 
Habari waheshimiwa!

Kuna kauli moja au msemo mmoja wa waswahili unasema mla nawe ndio mfa nawe.

Nawaomba waheshimiwa kwa nafasi zao walizoteuliwa na kuchaguliwa wasije kuwasahau vijana waliopigwa na mvua na jua na kukesha mpaka kunakucha kuakikisha ushindi unapatikana huwe wa goli la kichwa au la mguu.

Moja ya changamoto ya vijana kwa sasa ni ajira, viongozi mliopata nafasi nendeni mkabuni na mkatutengeneze ajira mpya.

Kuna vijana wazalendo waliowapigania naomba na nyinyi muwape vipaumbele muwapiganie ili kesho ijayo wawapiganie tena, ila msije kuwaona kama mbwa wa mawindo ambaye baada ya kukamata windo hana thamani tena.

Itakuwa fedhea sana mukiwaacha vijana wazalendo wanatanga tanga harafu ajira wakapewa wale wengine ili kesho waje kuitukana serikali, naomba uzalendo utumike kama kigezo cha kutoa ajira.
hivi waache kuwapa watoto zao na ndugu zao wakupe wewe sasa wakishakupa wewe ajira watamtumia nani..
 
Back
Top Bottom