Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda.
Ni kufuatia kuyumba kwa uzalisha na viwanda kuzalisha chini ya kiwango, baada ya Tanesco kutangaza mgawo.
Dar es Saam. Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda alisema kuwa moja ya changamoto nchini ambayo inarudisha maendeleo nyuma hasa ya viwandani ni tatizo la kutokuwapo kwa umeme wa uhakika.
Akizungumza jana Dar es Salaam katika uzinduzi wa Kiwanda cha Kutengeneza Juisi cha Wabantu kilichopo mkoani Tanga, Kigoda alisema kuwa Serikali inatakiwa kuhakikisha kuwa nishati ya umeme inakuwa ya uhakika ili kufikia lengo.
Kigoda alisema kuwa ili kuweza kufikia lengo kwa kiwanda hicho kipya, lazima nishati ya kueleweka na itakayowezesha ufanisi kwa haraka iwapo kwani mitambo inayotumika ni ya kisasa hivyo ni Serikali lazima itilie mkazo suala zima la umeme.
"Ni matumaini yangu mna malengo ya kufika mbali,lakini nijuavyo mimi umeme katika viwanda ni changamoto kubwa, hivyo tutahakikisha Serikali inatilia mkazo hasa kwenye nishati ya umeme ili muweze kufika panapostahili," alisema Kigoda.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho, Zahor Rashid alisema kuwa lengo la kuanzisha kiwanda hicho ni kukuza pato la taifa kwa kutengeneza juisi nzuri yenye kiwango ambayo itauzwa mikoa yote nchini, baadaye Afrika Mashariki hatimaye kuvuka mipaka hadi kupata soko la Afrika kwa ujumla,
Alieleza kuwa kiwanda hicho kimeanzishwa mkoani Tanga kwa sababu ndipo kwenye matunda mengi ya kila aina hivyo ni rahisi kupata matunda yenye kiwango na kwamba kiwanda hicho kitakuwa na vituo kila mkoa wenye matunda kwa wingi ili kuendelea kutengeneza juisi nzuri zaidi
"Tutajitahidi kuweka kituo kila mkoa unazalisha matunda kwa wingi ili kuhakikisha tunayatumia ipasavyo badala ya kuyaacha yaharibike," alisema Rashidi.Kigoda akiri umeme kikwazo cha maendeleo - Biashara - mwananchi.co.tz