Mgombea wa urais katika uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia mapema leo alifika makao makuu ya idara ya uhamiaji kwa amehojiwa kuhusu uraia wake.
Karia ni kaimu rais wa TFF aliwekewa pingamizi kuhusu uraia wake, lakini aliruhuiwa na kamati ya uchagiuzi inayooongozwa na Recovatus Kuuli kuendelea na uchaguzi.
Mratibu na Msemaji wa Idara ya uhamiaji, Ally Mtanda amesema idara yake imemhoji Karia kuhusiana na uraia wake.
"Ni kweli ameitikia wito ni kawaida kwetu, bado tunaendelea na uchunguzi, lakini hatuna mamlaka ya kumtoa kwenye uchaguzi," amesema Mtanda.
Uchaguzi huo ukitarajiwa kufanyika mkoani Dodoma, Agosti 12, wagombea wengine wa nafasi hiyo ya urais ni nahodha wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Ally Mayay na Ofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Shija Richard. Pia wapo Imani Madega, na Fredrick Mwakalebela.
Chanzo: Mwananchi