Kigogo TFF ahojiwa na uhamiaji

testa

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2012
Posts
442
Reaction score
180
Mgombea wa urais katika uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia mapema leo alifika makao makuu ya idara ya uhamiaji kwa amehojiwa kuhusu uraia wake.

Karia ni kaimu rais wa TFF aliwekewa pingamizi kuhusu uraia wake, lakini aliruhuiwa na kamati ya uchagiuzi inayooongozwa na Recovatus Kuuli kuendelea na uchaguzi.

Mratibu na Msemaji wa Idara ya uhamiaji, Ally Mtanda amesema idara yake imemhoji Karia kuhusiana na uraia wake.

"Ni kweli ameitikia wito ni kawaida kwetu, bado tunaendelea na uchunguzi, lakini hatuna mamlaka ya kumtoa kwenye uchaguzi," amesema Mtanda.

Uchaguzi huo ukitarajiwa kufanyika mkoani Dodoma, Agosti 12, wagombea wengine wa nafasi hiyo ya urais ni nahodha wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Ally Mayay na Ofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Shija Richard. Pia wapo Imani Madega, na Fredrick Mwakalebela.

Chanzo: Mwananchi
 
Usilolijua ni sawa na usiku wa kiza. Ni vyema akaliweka sawa ili watanzania wafahamu ingawa wengine tunamjua fika tangu udogo na kuufahamu ukweli ulivyo.
Kwa wale waliowahi kuishi barabara ya tano kipande pembezoni mwa Usagara (Karimjii) Sekondari wanamfahamu vizuri sana hasa nasaba za wazazi wake.
Au hata kama uliwahi kuwa shabiki au kuchezea Usagara Shooting utamuelewa vizuri sana. Na wengineo wale waliosoma Popatlal wanamjua sana.
Tusiwalaumu wanamtilia mashaka na pia huu ni wakati mzuri wa kuupambanua vizuri uraia wake.
 
Asante kwa taarifa, tusubiri kinachoendelea tujue hatma yake
 
tusubiri mamlaka zifanye kazi yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…