Kigogo TFF katika tuhuma nzito!

Kigogo TFF katika tuhuma nzito!

Chwisa

Member
Joined
Oct 13, 2017
Posts
17
Reaction score
8
Makamu Mwenyekiti wa TFF, Michael Wambura anatuhumiwa kufaudu USD 45,0000, zilizotolewa kwa TFF (FAT) ya wakati ule na Marehemu Enock Maganga ili kunisaidia FAT katika maandalizi ya Challenge. Inadaiwa FAT ililipa hela hizo kwa Wambura aliyedai kuwa ni Mkurugenzi wa kampuni ya Jecks Ltd iliyokuwa ya Maganga.Hadi deni linakwisha iliishalipwa 84m.
============================================

Wambura anadaiwa kujilipa Dola za Marekani 45,000 (Dola moja inauzwa Sh 2,240), kwa nyakati tofauti ikiwa ni fedha ambazo Kampuni ya Jecks Systerms Limited iliikopesha iliyokuwa FAT, sasa TFF mwaka 2002 akiwa Katibu Mkuu.

Kwa mujibu wa nyaraka ambazo gazeti hili inazo nakala zake, makubaliano ya mkopo kati ya mmoja wa wakurugenzi wa kampuni hiyo, Enock Maganga (sasa marehemu) na Wambura kama Katibu Mkuu wa taasisi hiyo, yalisainiwa Novemba 29, 2002 ikiwa ni mkopo wa dola za Marekani 30,000 kwa makubaliano ya kurudisha dola 45,000.

Mjane wa Maganga, Irene Maganga aliliambia gazeti hili kuwa kwa vile yeye ndiye msimamizi wa mirathi ya mumewe aliyefariki kwa tatizo la figo nchini India, aliamua kufuatilia deni hilo kwa vile alikuwa alikifahamu, na ndipo alipobaini fedha zao zimelipwa na zimeliwa.

Kwa mujibu wa makubaliano ya mkopo huo, ambapo nyaraka zinadai ulikuwa ni kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya Kombe la Chalenji kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati, FAT ilitakiwa kurejesha na riba ya dola za Marekani 15,000.

“Mimi nimefuatilia sana hizi fedha kwa vile nilikuwa nafahamu hili deni la marehemu mume wangu, lakini uongozi uliopita (wa TFF wa Jamal Malinzi) uliniambia deni lilishalipwa na aliyechukua fedha ni Wambura… naomba uongozi wa sasa unisaidie nipate haki yangu,” alidai mjane huyo wa Maganga.

Habari za uhakika zilizopatikana ndani ya TFF, zimebainisha kuwa fedha hizo zilishalipwa zote kwa awamu kati ya mwaka 2002 na mwaka 2015, na fedha iliyotoka ni zaidi ya kiasi kilichokuwa kikidaiwa na kampuni hiyo.

“Fedha zilikuwa zinalipwa kwa awamu kwa Wambura ambaye baadaye alijitambulisha kama mmoja wa wakurugenzi wa Jecks na mpaka deni hilo linakwisha, zilikuwa zimeshalipwa sh milioni 84,” alisema mtoa habari wetu.

“Malipo ya awali yalifanyika wakati yeye (Wambura) akiwa kiongozi, na kisha baada ya kuingia uongozi wa Leodegar Tenga, hakuna malipo yoyote aliyodai mpaka Tenga alipoondoka madarakani mwaka 2013, ndipo alipokuja kudai tena akidai aliikopesha TFF fedha hivyo anataka alipwe,” kilieleza chanzo chetu.

Kwa mujibu wa nyaraka za malipo zilizosainiwa na Wambura ambazo gazeti hili lina nakala yake, Julai 30, 2004, Makamu huyo wa Rais wa TFF alilipwa Sh milioni 16.5 kwa vocha namba 5324 ambazo malipo yalifanyika kwa fedha taslimu.

Aidha, kwa mujibu wa nyaraka hizo, malipo mengine yalifanyika Agosti 15, 2014, Wambura kupitia kampuni hiyo alilipwa Sh 10,050,200 kwa vocha namba 009647 na hundi namba 02059, Oktoba 2, mwaka huohuo alilipwa Sh milioni 5 kwa vocha namba 00790 na namba ya hundi ni 00848, Oktoba 21 Sh milioni 10 kwa vocha namba 00810 na hundi namba 00319
Kisha malipo mengine yakafanyika mwaka 2015 ambako Machi 16, alilipwa Sh 10,001,930 kwa vocha namba 0011071 na hundi namba 002271, Juni 16 alilipwa Sh milioni 10 kwa vocha namba 001226 na hundi namba 0026, Julai 25 Sh 5,095,424 kwa vocha namba 001187 na hundi namba 002408.

Malipo mengine ni Agosti 19 alilipwa Sh milioni 2 kwa vocha namba 001641 na hundi namba 000583, Septemba 14 Sh milioni 3 kwa vocha namba 003601 na hundi namba 00445 na malipo ya mwisho yalifanyika Septemba 30, 2015 ambako zililipwa Sh 12, 352,500 kwa vocha namba 003650 na hundi namba 000497.

Akizungumza na gazeti hili, Irene alisema anachoomba kwa uongozi wa sasa wa TFF alipwe fedha hizo maana tangu mumewe akiwa hai, hawajalipwa chochote.

“Mimi niliteuliwa kuwa msimamizi wa mirathi pamoja na watoto wangu, sasa mpaka nimeamua kuja kwenye vyombo vya habari ni kwamba nimeona fedha za marehemu mume wangu zimekaa muda mrefu bila malipo, na mbaya zaidi nilipofuatilia katika uongozi uliopita wa TFF niliambiwa zilishalipwa, naomba nisaidiwe,” alisema.

Alipotafutwa Wambura kujibu tuhuma hizo alisema hamfahamu mjane huyo “Simfahamu, lakini nyie mambo ya FAT yalishapita siku nyingi mnahangaika nayo ya nini?”.

Kwa upande wake, Rais wa TFF, Wallace Karia alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo za Makamu wake, alisema atafutwe Katibu Mkuu kwa vile ndiye mtendaji.

Alipotafutwa Kaimu Katibu Mkuu, Kidao Wilfred alisema taasisi ina namna yake ya kufanya kazi.

“Hii ni taasisi na haifanyi kazi kupitia vyombo vya habari ina taratibu zake za kufanya kazi,” alisema Kidao.

Chanzo: Habari Leo
 
Hivi karibu tumeshuhudia uchaguzi wa aina yake katika Shirikisho la mpira wa miguu TFF, Ndugu Wallace Karia ameonekana kuaminiwa zaidi na wadau wa soka kuliko kiongozi yeyote kabla yake.

Kama tujuavyo TFF ilikuwa imeoza na inanuka rushwa na ubadhilifu, sasa shombo limeanza tena kwa kasi sana. Makamu wa Rais Ndg. Wambura amefungua dimba na kutia doa uongozi wa Karia.

KIGOGO TFF KATIKA KASHFA NZITO

Chanzo : Habari leo

..........
Wambura anadaiwa kujilipa Dola za Marekani 45,000 (Dola moja inauzwa Sh 2,240), kwa nyakati tofauti ikiwa ni fedha ambazo Kampuni ya Jecks Systerms Limited iliikopesha iliyokuwa FAT, sasa TFF mwaka 2002 akiwa Katibu Mkuu.

Kwa mujibu wa nyaraka ambazo gazeti hili inazo nakala zake, makubaliano ya mkopo kati ya mmoja wa wakurugenzi wa kampuni hiyo, Enock Maganga (sasa marehemu) na Wambura kama Katibu Mkuu wa taasisi hiyo, yalisainiwa Novemba 29, 2002 ikiwa ni mkopo wa dola za Marekani 30,000 kwa makubaliano ya kurudisha dola 45,000.

Mjane wa Maganga, Irene Maganga aliliambia gazeti hili kuwa kwa vile yeye ndiye msimamizi wa mirathi ya mumewe aliyefariki kwa tatizo la figo nchini India, aliamua kufuatilia deni hilo kwa vile alikuwa alikifahamu, na ndipo alipobaini fedha zao zimelipwa na zimeliwa.

Kwa mujibu wa makubaliano ya mkopo huo, ambapo nyaraka zinadai ulikuwa ni kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya Kombe la Chalenji kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati, FAT ilitakiwa kurejesha na riba ya dola za Marekani 15,000.

“Mimi nimefuatilia sana hizi fedha kwa vile nilikuwa nafahamu hili deni la marehemu mume wangu, lakini uongozi uliopita (wa TFF wa Jamal Malinzi) uliniambia deni lilishalipwa na aliyechukua fedha ni Wambura… naomba uongozi wa sasa unisaidie nipate haki yangu,” alidai mjane huyo wa Maganga.

Habari za uhakika zilizopatikana ndani ya TFF, zimebainisha kuwa fedha hizo zilishalipwa zote kwa awamu kati ya mwaka 2002 na mwaka 2015, na fedha iliyotoka ni zaidi ya kiasi kilichokuwa kikidaiwa na kampuni hiyo.

“Fedha zilikuwa zinalipwa kwa awamu kwa Wambura ambaye baadaye alijitambulisha kama mmoja wa wakurugenzi wa Jecks na mpaka deni hilo linakwisha, zilikuwa zimeshalipwa sh milioni 84,” alisema mtoa habari wetu.

“Malipo ya awali yalifanyika wakati yeye (Wambura) akiwa kiongozi, na kisha baada ya kuingia uongozi wa Leodegar Tenga, hakuna malipo yoyote aliyodai mpaka Tenga alipoondoka madarakani mwaka 2013, ndipo alipokuja kudai tena akidai aliikopesha TFF fedha hivyo anataka alipwe,” kilieleza chanzo chetu.

Kwa mujibu wa nyaraka za malipo zilizosainiwa na Wambura ambazo gazeti hili lina nakala yake, Julai 30, 2004, Makamu huyo wa Rais wa TFF alilipwa Sh milioni 16.5 kwa vocha namba 5324 ambazo malipo yalifanyika kwa fedha taslimu.

Aidha, kwa mujibu wa nyaraka hizo, malipo mengine yalifanyika Agosti 15, 2014, Wambura kupitia kampuni hiyo alilipwa Sh 10,050,200 kwa vocha namba 009647 na hundi namba 02059, Oktoba 2, mwaka huohuo alilipwa Sh milioni 5 kwa vocha namba 00790 na namba ya hundi ni 00848, Oktoba 21 Sh milioni 10 kwa vocha namba 00810 na hundi namba 00319
Kisha malipo mengine yakafanyika mwaka 2015 ambako Machi 16, alilipwa Sh 10,001,930 kwa vocha namba 0011071 na hundi namba 002271, Juni 16 alilipwa Sh milioni 10 kwa vocha namba 001226 na hundi namba 0026, Julai 25 Sh 5,095,424 kwa vocha namba 001187 na hundi namba 002408.

Malipo mengine ni Agosti 19 alilipwa Sh milioni 2 kwa vocha namba 001641 na hundi namba 000583, Septemba 14 Sh milioni 3 kwa vocha namba 003601 na hundi namba 00445 na malipo ya mwisho yalifanyika Septemba 30, 2015 ambako zililipwa Sh 12, 352,500 kwa vocha namba 003650 na hundi namba 000497.

Akizungumza na gazeti hili, Irene alisema anachoomba kwa uongozi wa sasa wa TFF alipwe fedha hizo maana tangu mumewe akiwa hai, hawajalipwa chochote.

“Mimi niliteuliwa kuwa msimamizi wa mirathi pamoja na watoto wangu, sasa mpaka nimeamua kuja kwenye vyombo vya habari ni kwamba nimeona fedha za marehemu mume wangu zimekaa muda mrefu bila malipo, na mbaya zaidi nilipofuatilia katika uongozi uliopita wa TFF niliambiwa zilishalipwa, naomba nisaidiwe,” alisema.

Alipotafutwa Wambura kujibu tuhuma hizo alisema hamfahamu mjane huyo “Simfahamu, lakini nyie mambo ya FAT yalishapita siku nyingi mnahangaika nayo ya nini?”.

Kwa upande wake, Rais wa TFF, Wallace Karia alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo za Makamu wake, alisema atafutwe Katibu Mkuu kwa vile ndiye mtendaji.

Alipotafutwa Kaimu Katibu Mkuu, Kidao Wilfred alisema taasisi ina namna yake ya kufanya kazi.

“Hii ni taasisi na haifanyi kazi kupitia vyombo vya habari ina taratibu zake za kufanya kazi,” alisema Kidao.
 
Huyo mtu si mwaminifu hata kidogo. Apambane na hali yake.
 
Huyo wambura hana kazi nyingine anayojua hapa nchini zaidi ya tff wamfunge kama wale wa simba
 
Back
Top Bottom