Kigogo wa TFF afungiwa maisha kwa kosa la kuiba na kughushi

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411

Kamati ya Maadili iliyokutana Jumamosi Agosti 25,2018 Makao Makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) imemfungia kutojishughulisha na soka Mbasha Matutu.

Matutu ambaye ni Msimamizi wa kituo cha Shinyanga na Mjumbe wa Kamati kuu TFF, amefungiwa kwa kwa makosa matatu ya kushindwa kutekeleza majukumu yake, ubadhirifu, kughushi na kuiba kinyume na kanuni za Maadili na Ligi Kuu.

Kiongozi huyo kwa sasa amefutwa rasmi wadhifa wake ndani ya Shirikisho hilo akiwa kama Mjumbe wa Kamati Kuu na sasa hatohusika tena na masuala ya soka nchini.

Maamuzi hayo yametolewa na TFF leo kupitia Makao yake yake yaliyopo Ilala, Karume baada ya kuitisha kikao na Waandishi wa Habari.

Kamati ya Maadili iliyokutana Jumamosi Agosti 25,2018 Makao Makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) imemfungia kutojishughulisha na Mpira wa Miguu maisha aliyekuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF na msimamizi wa kituo cha Shinyanga Mbasha Matutu

Chanzo: Bongo 5
 
USANIII UBADHIRIFU NA WANA USHAHIDI SIWAENDE MAHAKAMANI WAKAWASHATAKI
 
Huko naona watu wanapanga safu zao za uongozi na allies.. Haiyumkini huyu ni wa kambi nyingine..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…