LGE2024 Kigoma: Abdul Nondo, Mwenyekiti wa Vijana ACT Wazalendo ajiandikisha kwenye daftari la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

LGE2024 Kigoma: Abdul Nondo, Mwenyekiti wa Vijana ACT Wazalendo ajiandikisha kwenye daftari la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Abdul Nondo, Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ACT Wazalendo Taifa, ameonyesha mfano wa uongozi kwa kujitokeza kujiandikisha katika daftari la mkazi, akijiandaa kwa uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba mwaka huu.

Soma pia: Lindi: Mbunge wa Mchinga, Salma Kikwete ajiandikisha kwenye daftari la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Akiwa katika mtaa wa Livingstone, kata ya Kasingirima, jimbo la Kigoma mjini, Nondo alisisitiza umuhimu wa vijana wote nchini kutumia fursa hii ya mwisho kujiandikisha, akiwataka wajitokeze leo Jumapili, Oktoba 20, 2024.

Nondo.png

Nondo libainisha kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa ni nguzo muhimu ya uwajibikaji na maendeleo, na kuwahimiza vijana kushiriki kikamilifu katika mchakato huu wa kidemokrasia.

Source: Jambo TV
 
Back
Top Bottom