GE2025 Kigoma: ACT Wazalendo wasitisha Kampeni za Ubunge baada ya kukosa Watu kwenye eneo la tukio

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Chama cha ACT WAZALENDO kimeahirisha mkutano wake wa kampeni za ubunge katika jimbo la kigoma mjini chini ya mgombea ZITTO KABWE, uliopangwa kufanyika siku ya jana september 18 mwaka 2025 katika maeneo ya meti sokoni katika jimbo la kigoma mjini.

​

Licha ya maandalizi ya mkutano huo kukamilika, ghafla mkutano uliahirishwa kwa sababu ya kukosa idadi kubwa ya watu waliotarajia kuwahutubia katika jimbo hilo la Kigoma Mjini.

Soma Pia GE2025 - Zitto nyumba kwa nyumba kuzisaka kura za ubunge

Your browser is not able to display this video.
 
Uchaguzi hauna shangwe kabisa huu
HAKUNA UCHAGUZI 2025 NILIWAAMBIA TOKA 2022 KUWA 2025 HAKUNA UCHAGUZI ..PIA NILIWAAMBIA CHADEMA NA WAPINZANI WALIO KUWA WANAJIDANGANYA NA KANYANGA SAMIA BUSHIRI KUWA ATALETA KATIBA NIKA WAAMBIA ILIKUWA RAHISI KUPATA KATIBA MPYA NA NZURI CHINI YA JPM KULIKO HUYU MPUUZI ....NAKUMBUKA NILIPIGWA BAN ZA KUFA MTU KILA WEEK BAN MOD WAKANIITA MCHOCHEZI NAKUMBUKA NILIWAAMBIA SA100 ATAMWAGA SANA DAMU NIKAWA NAPIGWA BAN .
 
Huwezi kuelewa hoja hiyo kwa sababu ipo nje ya uwezo wako.Wananchi huwa wakipiga kura wanachagua aliye na afadhali kiuwezo,kitabia,kielimu na kiuweledi kwa sababu hakuna aliye perfect.Hakuna mkamilifu kuna aliye na afadhali zaidi kuliko wenzake.
 
safi sana!

kumbe hata kwao hakubaliki!

tulishawaambia CCM ikija kwenye uchaguzi ni lijitu la ajabu mkakomaza shingo zenu!

Haya sasa BABA LEVO anavyokwenda kumuaibisha ZITTO asubuhi na mapema hio 29 OKTOBA!
 
Nini chanzo cha kushuka kwa Zitto Kabwe kisiasa..?
Undumila kuwili, unafiki, uzandiki. Jamaa hana nia thabiti ya maendeleo ya Tanzania, huwez amini zile hatua alikuwa anachukua JPM za kuleta maendeleo yeye hakuona chochote ila kwa sasa anaona mtu mwenye akili unaelewa.
Kilichompa kiki huyu jamaa ni zile report za ufisadi ila baada ya hapo akawa anaambatana na misafara ya Msoga nje ya nchi, akatepetq mazima kabakia utapeli wa maneno
 
We katibiwe kwanza unamatatizo ya afya ya akili tukichelewa utaokota makopo inshu hapa ni kigoma we unaleta stori zingine mara ban alafu umeandika kwa jaziba Sana mkuu nenda hospitali samahan ka nmekukosea
 
Uliona mbali sana. Wengi huyu mama alivyoingia, tuliweke matumaini makubwa juu yake, lakini kwa sasa kila mmoja anasema aheri ya mtangulizi wake. Mikono yake imejaa damu za watu wasio na hatia. Mungu wetu amlipe sawa na matendo yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…