A
Anonymous
Guest
Wilaya ya Kasulu Vijijini, Kata ya Rungwe mpya, Vijana waliopewa jukumu la kufanya survey na wanaofunga Umeme wanatengeneza mazingira ya Rushwa
Nilifanyiwa usajili wa Meter, taarifa zangu zikawasilishwa TANESCO kwa ajili ya kuja surveyor ili anipimie, lakini ni takriban wiki mbili zimepita bila mafanikio yoyote, ukiwapigia simu wanakuambia wanapangiwa sehemu za kwenda, hivyo kama una elfu 20 wakufanyie mpango upewe Control Number.
Pili, nimeshuhudia kwa ambao wamelipia, vijana hao wakija kukufungia Umeme wanataka uwape elfu kumi, sasa sijui ni utaratibu upi wanatumia.
------------- ---------------------
Jambo lingine linalokera ni kuwa kuna changamoto ya kukatika umeme mara kwa mara katika Wilaya ya Kasulu, imekuwa ni kero kubwa, hali hiyo inaathiri Wafanyabiashara wengi.
Licha ya kuwa TANESCO wenyewe mara kadhaa kutoa taarifa lakini haisaidii sana kwa kuwa athari inayopatikana kukosekana kwa umeme ni kubwa katika mahitaji yanayohitaji umeme.
Umeme unaweza kukatika kuanzia asubuhi hadi jioni, siku ambayo hawakati kwa muda huo wanakuwa wanakata na kurudisha kila baada ya dakika kadhaa hali ambayo ni kama yaleyale tu kwa kuwa athari zinakuwa kubwa ikiwemi kuunguza vitu na kuharibu mitambo inayotumia umeme.