LGE2024 Kigoma: Kura feki zakamatwa Mwandiga

LGE2024 Kigoma: Kura feki zakamatwa Mwandiga

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
WAkuu,

Kupitia ukurasa wa X wa ACT Wazalendo wameweka taarifa hii, mambo yameanza kunoga mapemaaa!

Kupata matukio yanyojiri kimkoa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ingia hapa: LIVE - LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Screenshot_20241127_084013_X.jpg

Wakati uchaguzi wa Serikali za Mitaa ukianza leo Novemba 27, 2024, tayari kumeanza kuripotiwa matukio yanayotajwa kuashiria kwa namna moja ama nyingine kuvurugwa uchaguzi huo.

Katika kitongoji cha Majengo kilichopo mamlaka ya mji mdogo wa Mwandiga, Jimbo la Kigoma Kaskazini, mkoani Kigoma, zimegundulika zinazodaiwa kuwa kura feki zilizopangwa kutumika katika uchaguzi huo.

Jambo TV inaendelea kufuatilia mwenendo wa uchaguzi huu nchi nzima na tutakuwa tukikuhuisha na taarifa zake kadiri zitakavyotufikia.
 
Ni watu wajinga tu watajitokeza kushiriki kwenye hizi chaguzi za kihuni. Sujui ni kipi ccm haielewi, watu wameichoka lakini inalazimisha tu kuwatala.
Naungana na wewe katika hili, utakuwa mjinga tu endapo utaenda kupanga foleni na kuacha kazi zako.
 
Ni watu wajinga tu watajitokeza kushiriki kwenye hizi chaguzi za kihuni. Sujui ni kipi ccm haielewi, watu wameichoka lakini inalazimisha tu kuwatala.
Hakika, mimi hata zilipoteza mda wangu kwenda kujiandikisha
 
Mambo yanayofanyika kwenye CHAGUZI zetu nchini, yanashangaza kwa kweli..Wajukuu na vitukuu vyetu watakuja kujiuliza kama kweli tulikuwa viumbe wenye akili timamu
 
Ni watu wajinga tu watajitokeza kushiriki kwenye hizi chaguzi za kihuni. Sujui ni kipi ccm haielewi, watu wameichoka lakini inalazimisha tu kuwatala.
Ni watu wachache sana ndiyo watakuelewa. Wengi watakuambia ni bora eti ushiriki, kuliko kujitenga na hayo maigizo yao.

Kimsingi bila ya Katiba mpya ya wananchi na tume huru ya uchaguzi, Watanzania wasitegemee miujiza kwenye uchaguzi wowote ule utakaofanyika chini ya hii katiba mbovu ya 1977.
 
Niliko kura zilishapigwa zamani kinachofanyika nikujaza kwenye masanduku ya kupigia kura,mawakala wa upinzani wanatolewa nje ili kura ziweze kujazwa kwenye masanduku.
 
Back
Top Bottom